GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
DAR ES SALAAM; Msanii wa muziki wa kizazi kipya Faustina Charles ‘Nandy’, ameibuka kwenye mkutano na wanahabari akiwa ametinga vazi analosema ni kama mtindo wa nguo za Rais Samia Suluhu Hassan.
Nandy aliyekuja kuzungumzia tamasha lake litakalofanyika Mwanza kesho, alikuwa amevaa ushungi mweusi na vazi la suti nyekundu aina ya Kaunda.
Baada ya kuulizwa kuhusu uvaaji wa vazi hilo ikiwa ni mara yake ya kwanza akiwa katika muonekano huo, amesema anavutiwa sana na uvaaji huo wa Rais Samia, kiasi cha yeye kuamua kuiga akisema ni vazi zuri kwa wanawake.
“Rais ametupa vazi letu la kipekee ambalo ni zuri na wanawake kwa sasa wanavaa, nikaona na mimi niwakilishe. Nitaenda kwenye tamasha la Nandy kisamia,”amesema. Mwingine aliyevaa vazi kama hilo ni Yasirun Yasin ‘Yammi’
Ametaja baadhi ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Maya Christinah Xichavo ‘Sho Madjozi’ kutoka Afrika Kusini, William Lyimo ‘Billnas’, Saraphina Michael ‘Saraphina’, Stamina Sharobwenzi ‘Stamina’, Young Lunya na Yasirun Yasin ‘Yammi’
Amesema katika tamasha hilo litakalofanyika kwenye viwanja vya Elevante atatambulisha msanii mwingine wa kimataifa kama ‘surprise’.
Kwa upande wake William Lyimo ‘Billnas’, amesema amejipanga vizuri kufanya kazi sio kama mume bali msanii mwenye mkataba kama wengine na atahakikisha anaimba na bendi.
Chanzo: habarileotz
Ameanza Kuvaa tokea alipokuwa Makamu wa Rais mbona huko nyuma hatutukuona Ukijipendekeza Kwake na Kumsifia juu ya Uvaaji wake?
Hovyoo na ndiyo maana Unaishi kwa Matumaini.