Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tunakaribisha maoni mbalimbali na hata mawazo tofauti kati ya wanachama na viongozi wetu. Kama chama cha kidemokrasi, Chadema tunaona suala la kutofautiana na kulumbana juu ya hoja mbalimbali ni fursa muhimu sana ya kuonesha demokrasia yetu na pia kukua na kuimarika kifikra.
Wanachama wote wa Chadema jengeni hoja makini katika mitizamo yenu juu ya masuala mbalimbali mathalani uchaguzi 2025, muungano, nk. Msisahau kuwa mijadala na malumbano ya hoja ni sehemu muhimu ya chama chetu na bila hivyo chama kitakosa uchangamfu na ukomavu, na pia chama sio Mbowe, Lissu, Mnyika, au yeyote yule bali chama ni sisi sote tukiwa na tofauti zetu katika hoja mbalimbali.