Tunakoelekea kuoga na Sabuni Pia tutaambiwa ni dhambi

Hapana sio mchungaji ila ninaongea uhalisia uliopo kuhusu wakristo na mpira, siku za mpira wa simba na yanga hata ibada huwa zinaharakishwa kwa baadhi ya makanisa unafikiri ni kwa nini?
Ikiwa wewe sio mchungaji u nani... Mzee wa kanisa,or shemasi?

Naona unajenga hoja kama ya mtu anayeathirika na mahudhurio duni katika Ibada siku watani wa jadi wanapokiwasha
 
Ikiwa wewe sio mchungaji u nani... Mzee wa kanisa,or shemasi?

Naona unajenga hoja kama ya mtu anayeathirika na mahudhurio duni katika Ibada siku watani wa jadi wanapokiwasha
Najaribu kukutafakarisha namna mpira ulivyo na ushabiki wake, na ulivyopewa umuhimu kuliko Mungu mwenyewe, si ajabu ukakuta wakristo hao hao wanatokanana wengine kuweka uadui kisa mpira. Wala siathiriki na mahudhurio kwa sababu sina kanisa wala sio shemas kama unavyowaza ni muumini kama ulivyo wewe pengine
 
Kuelewa kwa jambo fulani ama kutokuelewa ni maamuzi ya muhusika anaeeleweshwa, unazani ni jambo rahisi kumuachisha au kumkataza mtu jambo ambalo liko kwenye damu.
 
Mchungaji yuko sahihi,alichokisema ninkweli,na hii ndio injili inayotakiwa ya kuhubiria watu waache DHAMBI ZOTE wajisafishe matendo yao wawe watakatifu hapa duniani ili wakifa waweze kuingia mbinguni,Mbingu ni ya watakatifu.Kama si mtakatifu mbinguni huwezi kuingia.
2)Katika dunia ya leo Injili ya kweli mahubiri magumu kama haya hayahubiriwi ,wqchungaji ama kwa kujua au kwa kutokujua au kwa kuogopa kupoteza waumini,au kuwakwaza wauminwao hawahubiri kwa msisitizo unaotakiwa juu ya watu kuacha dhambi zote ,baadhi ya dhambi zilizozoeleka katika jamii na kuonekana kama ni kawaida WANAZIFUMBIA MACHO hawazikemei ,dhambi hizo ni kama
a)USHABIKI WA MICHEZO kama mipira,ngumi,mieleka n.k
na vingine vya DUNIA hii kama sinema filamu ,series,miziki ya dunia na baadhi inayoitwa ya gospel ila ni ya kidunia,sinema filamu za katuni,
b)MAPAMBO na KUJIREMBA hasa wanawake mawigi,kusuka nywele,urembo wote kwa ujumla na mengine yanayofanana na hayo kama mavazi ya kiume suruali kuvaliwa na wanawake na wanaume kuvaa nguo za kike,mavazi ya kubana na mavazi ya aibu,mashindani ya urembo umiss n k
c)POMBE VILEVI,sigara madawa ya kulevya ,na matumizi ya vinywaji/vyakula visivyo pombe ila vina madhara kwa afya kama energy drinks,vinywaji vya sukari n.k maana miili yetu tumepewa tuitunze sinkuharibu afya,kuvaa milegezo,FASHIONI za nguo na urembo za dunia
c)VITU VYA UPAKO mafuta ya upako,maki ya upako,chumvi,keki,n.k
d)TELEVISION YAKO nyumbani sio kila kinacho oneshwa kwa TV kina afya kiroho kwako na familia yako ,ni vipindi vichache vya kuangalia na tv stestheni chache za kuangalia nyingine
e)UNYAKUO WA KANISA(RAPTURE) watu wawe tayari kwa ajili ya unyakuo na unyakuo umekaribia,DHIKI kuu imekaribia
f)ROHO MTAKATIFU watu wajazwe ROHO mtakatifu atakayewasaidia na kiwafunfinulia baya na jema hata haya mnabishana hapa kwamba je ushabiki wa mpira ni dhambi au siyo dhambi,UKIWA NA ROHO Mtakatifu atakushihidia moyoni mwako ili ujue usahihi na uhalali wa jambo na mapenzi ya Mungu kwako.
na kadhalika ni mengi ambayo hayahubiriwi zaidi ya kuhubiri SADAKA michango mavuno ambalo pia ni jambo jema sadaka ikitolewa vyema kwa kujua misingi na namna ya kutoa hiyo sadaka hufanyika baraka.
mhubiri mengine yanayohubiriwa ni ya KUPOKEA VITU baraka za mwilini mambo ya mafanikio ya mwilini ambapo pia si jambo baya kama BARAKA hizo zikianzia kwanza ROHONI zikajidhihirisha mwilini .
HITIMISHO.
1)TUSI IPENDE DUNIA ukiipenda dunia kumpenda Mungu hakuko ndani yako,nyie sio wa ulimwengu huu nyie ni watu wa miliki ya Mungu hapa safarini njiani ,mtawala wa dunia hii ni shetani ,huwezi kutumikia mabwana wawili,ukiipenda dunia unafanyika adui wa Mungu
Mambo ya dunia ni anasa za dunia hii ikiwemo hayo maushabiki ya namna na fasheni za dunia hii
2)TUSISHIRIKI IBADA ZA SANAMU ibada za sanamu ni pamoja na anasa za dunia hii
3)tujisafishe matendo yetu tuwe watakatifu hapa duniani..tiketi ya kuingia mbinguni ni UTAKATIFU KWELI 100%
4)TUMTAFUTE ROHO mtakatifu kuliko kutenda dhambi kwa kutegemea uwepo wa neema ,ila Roho mtakatifu atusaidie kuomba,kutuongoza matendo
5)LINDA SANA MOYO WAKO mana huko ndiko zitokako chem chem za uzima wako
 
Sawa mkuu nimekusoma
 
Hiyo ya mapambo ya kujiremba yaashida gani mkuu, ukiweza na andiko itakuwa njema
 
Muulize Mchungaji ni halali kutoa zaka maana agano jipya Wala mitume hawakuwahi kupokea zaka ya mtu,, na hata Sadaka zilizoletwa waligawana wote Kwa kadiri ya Kila MTU alivyohitaji Wala hawakumpa mtume Paulo au Yohana Ili akazitumie mwenyewe,, siyo dhambi kula Sadaka pekeake akiwaacha waumini wengine wakiwa na mahitaji??
 
Ila Kiboko ya wachawi na akina Tito ndo wanampa MUNGU utukufu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…