Tunakoelekea kuoga na Sabuni Pia tutaambiwa ni dhambi

Tunakoelekea kuoga na Sabuni Pia tutaambiwa ni dhambi

Waliteswa, wakafa, wakazikwa kisha wakafufuka pamoja na Kristo katika mauti yake.

Leo hii wako ndani ya Kristo. Na Kristo ameketi mbinguni kwa Mungu baba.
Maana yake wao wapo Mbinguni ndani ya Kristo, ndio maana ya Kuokolewa na Kristo.
Usipotoshe watu,Kristo atakuja kuwachukua walio hai na wafupi watafufuliwa Kwanza.Hakuna mahali kwenye Biblia kwamba ukifa kwa matendo mema unaenda Mbinguni au mabaya inakuwa motoni!
 
Baada ya Mchungaji Mch. Abiud Misholi Kutamka adharani kwamba ni Ushetani mkubwa Mlokole kushabikia mpira Mwimbaji wa nyimbo za injili na SHABIKI mkubwa wa Yanga African @Ann_annie kafunguka ya moyoni na kusema....

"Kuna Max Nzengeli na Kennedy Musonda wameokoka sasa na wanacheza mpira itakuwaje??

Mabasi yenyewe tunayopanda ni ya washirikina biashara nyingi tunakoenda kununua vitu wawekezaji ni hao hao washirikina, sadaka tunazotuma kwa wachungaji tumezipata kwa hao hao washirikina na cha ajabu wachungaji hawazikatai hizo sadaka ... Niseme tu ni Yesu tu anayetulinda".

Hivi ndivyo alivyofunguka mwimbaji wa gospel, nimemuelewa vizuri kabisa, ila mchungaji Misholi sijamuelewa kabisa.

Bila shaka tunakoelekea, hata kuoga na sabuni ya GSM tutakuja kuambiwa ni dhambi 🤔
NZENGELI ni msabato, hajaokoka.
 
Matendo yako mema hayawezi kukuokoa.
Kiuhalisia mtu anaokolewa muda huohuo atakapo amini kufa na kufufuka kwa Kristo... Matendo yetu hayana mchango wowote kwenye wokovu katika Kristo.

Waefeso 2
4. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;
5. hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
6. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;
7. ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
8. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9. wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
 
Usipotoshe watu,Kristo atakuja kuwachukua walio hai na wafupi watafufuliwa Kwanza.Hakuna mahali kwenye Biblia kwamba ukifa kwa matendo mema unaenda Mbinguni au mabaya inakuwa motoni!
Kristo gani unayemsubiri kuwa atakuja?

Kristo baada ya kupaa mbinguni alisema ataleta msaidizi atakayeweka wazi na kufundisha mambo yote.

Cha msingi ni kuwa huyo roho wa Mungu ndiye Kristo mwenyewe aliye ahidi atakaa ndani yetu.

Sasa sijui unamsubiri Kristo gani, wakati yeye amesema yumo ndani yako?
 
Y
Yule jambazi aliyesulubiwa na Yesu mbona alipita kiulaini tu.. Future tense ilihusika hapo?

Ukijipanga kutetea msimamo hutokuja kuelewa maandiko ndugu.

Jambazi anabahatika kuwa na Yesu mwenyewe Wakati anaumaliza mwendo.

Sasa Wewe upo mbwinde na majirani zako ni kina Asha ngedere na Mwajuma ndala ndefu unaokokaje hapo? Wewe subiri hukumu tu..!

Ndo Maana ile sala aliyofundisha Yesu mwenyewe mwishoni anamalizia usitutie katika vishawishi...! Vishawishi ni vingi unatakiwa uvishinde kwanza!
 
Labda wewe. Mi kinyume chake.
kupunguza kiwango cha testosterone mwilini ni faida?
Kuchoma maini ni faida?
Kusinyaa kwa ubongo ni faida?
Kisukari ni faida?

Anyway not my business, good luck!
 
Nilichogundua kwako ni hiki.... "hujui lolote kuhusu TOBA na hujui pia anayetoa msamaha hapangiwi la kufanya".

Jambazi alikwenda mbingu, hata wewe unaweza kwenda hata kama umetenda madhambi mengi I siku ukitubu utasamehewa na utaenda mbinguni.
 
kupunguza kiwango cha testosterone mwilini ni faida?
Kuchoma maini ni faida?
Kusinyaa kwa ubongo ni faida?
Kisukari ni faida?

Anyway not my business, good luck!
Wali na Ugali ni vyakula vya wanga vinavyochangia sehemu kubwa ya kupata kisukari na Magonjwa ya Moyo.

Baadhi ya mihogo inasumu ya Cyanide inayoweza kuua kama ikizidi.

Fanta na Mirinda zinakiwango kikubwa cha sukari kinachoweza kuathiri hormones na Enzymes zinazohusika katika uchakataji wake.

Kila kitu kina madhara hasi.
 
Hivi ndivyo alivyofunguka mwimbaji wa gospel, nimemuelewa vizuri kabisa, ila mchungaji Misholi sijamuelewa kabisa.
Siyo kila Mchg ni mjumbe wa Mungu, wapo wengine ni wahuni kama wahuni wengine ila tu ni kwamba wana karama ya kutapeli
 
Back
Top Bottom