Mada nyingine ni za ajabu kweli: Kushiriki katika ukombozi limekuwa kosa? Kama nchi imeshindwa kutumia turufu ya ushiriki huo kunufaika, hilo kosa la Mwalimu Nyerere?Kweli alipambana akasomesha wananchi wake na akahakikisha kuwa taifa linakuwa na umoja na mshikano.
Lakini ukweli kuwa aliharibu uchumi wa taifa na kuliacha masikini huwa hauwekwi wazi.
Hayati Nyerere alisahau kupambania uchumi wa taifa lake. Akabaki kupigana vita kuzikomboa Uganda, Zimbabwe na Mosambiqui bila kusahau Afrika kusini.
Vita vya ukombozi alivyoshiriki vilisababisha taifa kubakia kuwa masikini mpaka leo hii.
Na huo uchumi unaosema aliuharibu, ilikuwa lini ulipokuwa mzuri hadi uharibiwe. Nchi zipi zilizokuwa zinafanana na Tanzania ambazo unaweza kutolea kama mfano wa uchumi ambao haukuharibiwa?