Tunakosea tunaposema mazuri aliyofanya hayati Julius Nyerere huku hatusemi mabaya aliyofanya na yametugharimu kama taifa

Mada nyingine ni za ajabu kweli: Kushiriki katika ukombozi limekuwa kosa? Kama nchi imeshindwa kutumia turufu ya ushiriki huo kunufaika, hilo kosa la Mwalimu Nyerere?

Na huo uchumi unaosema aliuharibu, ilikuwa lini ulipokuwa mzuri hadi uharibiwe. Nchi zipi zilizokuwa zinafanana na Tanzania ambazo unaweza kutolea kama mfano wa uchumi ambao haukuharibiwa?
 
Mkuu huna data sahihi wewe, wasema hakukuwa na viwanda wala chuo kikuu???
Hebu tuwekee "data sahihi" ulizonazo wewe, mkuu Allency!

Yaani hata kujuwa Chuo Kikuu inakuwa shida?
 
Biblia inasema mpende jirani yako. Tumemsaheme alitenda vema kuliko kuiba na kunemeesha familia yake.

Hata kukataa kuitwa mh. Nyerere bali Mwalimu ni sadaka yakini.
 
Nyerere aliacha viwanda je marais waliofuata waliviendeleza? Zaidi ya kuuza mashirika ya umma na ufisadi wa kutisha wakafanya kina mkapa.
 
Yeye alifanya kwa nafasi yake katika harakati za ukombozi wa nchi za Afrika akaondoka, je sisi tuliobaki tumelifanyia nini Taifa liweze kuendelea kama siyo kufikiria kuiba tu
 
Nyerere ni marehemu anayeogopwa hadi leo..

Ingawa kwa mazingira ya wakati huo si blame chochote alijitahidi sana. Sema alikosa washauri wazuri zaidizadi alizungukwa na machawa..
 
Wakati Mwalimu alikaa hadi foleni na Marais wengine wanakalia viti vya kanisani kwa adabu, kuna Paka special linasafirisha na kukalia kiti maalum👇🐒🐒🐒
 
Na tukishasema hayo mabaya yatatuvusha hapa tulipo kwenda nchi ya ahadi?
Tuwe na Utamaduni wa kusema mazuri na mabaya ya mtu mwanadamu sio kumlamba makalio tu kwa nyimbo na ngonjera.
 

Chuo kikuu kilianza kama sehemu ya College of London mwaka 1961. Nyerere alikikuta hicho chuo kikuu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…