Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Naomba nichangie kidogo kwa hatua iliyofikiwa leo kwa Maalim Seif kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwanza niseme mimi ni muumini wa maridhiano na ninaunga mkono "dhana" ya maridhiano iliyofikiwa leo pale Zanzibar.
Lakini ninapinga maridhiano haya yasiyo weka wazi msingi wa Maridhiano. Ninasema haya kwakuwa hadi sasa ACT na CCM hawajatueleza msingi wa maridhiano haya ni nini na hawajatuambia matunda yamaridhiano ya nyuma nini na kitendo cha leo kuweko maridhiano tena ni tafsiri ya kuwa maridhiano ya nyuma hayakuzaa matunda.
Nimesikiliza hotuba ya Maalim Seif leo, ni nzuri lakini haijajibu hoja za msingi za sisi tunaohoji msingi wa maridhiano haya. Imekuwa ni hotuba ya jumla zaidi inayo tulazimisha tufute machozi bila kutueleza kuwa kesho hatutalia kwasababu ya hili na lile.
Moja ya kichaka cha hoja wanachojificha wanaotetea ACT kujiunga na CCM ni hiki kinachoitwa "Siasa za Zanzibar zina namna yake". Hivyo hata tukihoji kwamba sababu zilizofanya 2015 wagomee zimetatuliwa ndipo wameingia tena au laaa? Wao wanatuziba kwa kujificha kwenye kichaka kinachoitwa historia ya siasa za Zanzibar.
Tumehoji hapa kwamba ni makubaliano gani ambayo ACT na CCM wameyaweka mezani hadi kufikiwa maridhiano ya leo ili kesho yasijirudie haya? Bado hatujibiwi tunarudishwa kwenye kichaka kanakwamba sisi hatujui historia ya Zanzibar.
Mfano Chadema imeweka mezani msingi wa maridhiano ya kitaifa kati yake na CCM ambayo ni 1. Kutambua kuwa uchaguzi ulikuwa batili, 2. Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, 3. Mchakato wa Katiba Mpya ya Warioba kuendelea
Pengine kuna wanachoshindwa kusema wazi kuwa maslahi ya Maalim na Wenzake yamezingatiwa kuliko malengo ya Wazanzibar ya kupata nchi yao ambao ndio msingi ulioasisiwa na CUF ya Maalim. Nani leo mtetezi wa Wazanzibar??
Jibu liko Pemba na Unguja!
_______________
Nakukumbusha, ni mwezi wa Sikukuu, Watu watano watapata ZAWADI ya kitabu cha Ujasusi kwa 20,000 tu popote ulipo badala ya 80,000.
Lipia 20,000/= kwa
TigoPesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
Airtel Money 0788887887
HaloPesa 0624452045
(Yericko Nyerere)
Tuma majina yako na ulipo
(Dar ni free delivery)
Nje ya Dar nauli 8,000/=
Instagram Follow @yerickonyerere