Zanzibar 2020 Tunakubaliana na maridhiano, lakini Maalimu Seif na ACT Wazalendo lazima muwajibu Watanzania haya

Zanzibar 2020 Tunakubaliana na maridhiano, lakini Maalimu Seif na ACT Wazalendo lazima muwajibu Watanzania haya

Mkuu katiba iliweka utaratibu baada ya maridhiano sio kabla.

Utaratubu wa kikatiba sio maridhiano bali ni sheria...
Baaada ya wapinzaniii kuishiwa hoja, kwa sasa tumebakiwa na vyama vya ubishi na wanachama wote, mumebakiwa na ubishi tu.

Siasaa hamzijui mumebakia kudandia dandia mambooo. Wenye akili kubwa kama akina malimu seifu ndo wanaoelewa tukio muhimu walilofanyaa. Wengine hamjui kituuuu kabisaaa.
 
Ulitakiwa kwa maoni yangu uongeze
4. Kutotambua matokeo ya uchaguzi.
5. Kurudia kwa mchakato mzima wa uchaguzi. Hapo ningeona kweli Chadema wako serious.
 
Mimi siungi mkono maridhiano hayo na wala sitayaunga mkono hata nikiwekewa bunduki kichwani .

Liwalo na liwe
Tupo wengi sana kwa hili halikubaliki kabisa,lkn siku zote nimekuwa nikisema kuwa upinzani wa Zitto unatia mashaka sana hapa Tanzania.
 
Chadema na siasa zenu kali mtaishia mitandaoni, wanasiasa makini hutanguliza maslahi mapana ya nchi.Kwa akili zenu hizi mtakosa vyote.Ndiyo maana HAlima & co wamewatosa
Aliye mtosa mwenzake ni yupi kati ya Mdee na CDM? Cdm ni taasisi kubwa kuliko hao wachumia matumbo yao kina Mdee na tushawafukuza na kuwavua uanachama.

Hutaki kajinyonge.
 
Mkiambiwa CCM hamna akili mkubali sio tusi ndivyo mlivyo

Hivi wewe unaweza kukutana tu na mtu barabarani mkariadhiana kwenda kula chakula cha mchana pamoja?

Bila ya kuwa na sababu ya msingi itayo pelekea kwenda kula chakula pamoja ?

Jibu ni kuwa lazima kutakuwa na jambo fulani litakalo pelekea tukio hilo na huo ndio msingi wa maridhiano ...

Unaposema neno maridhiano lazima lije swali mmeridhiana nini au maridhiano ya nini? Jibu lake ndio litakua msingi wa maridhiano hayo

Hivyo basi ili maridhiano yawepo lazima viwepo vitu mtakavyo ridhiana kwa pande zote husika na lazima vitu hivyo viwepo kabla ya maridhiano yenyewe

Bogus ndio mana kutwa mnaletewa wapinzani kushika uongozi CCM ninmapimbi kwelikweli
Hongera sana kwa comment yenye uzito unaojitosheleza
 
Kwani we Nani kwanza Unalipi hasa
Yaani Hata Nyuma ya Mtaa wenu hawakufahamu
Mnajipa Ujiko tu kumbe Makopo Matupu
Wewe una nini?kuanzia hapa dsm hadi kwenu mwandiga una nini cha kujivunia?

Hadi nyumbani kwenu mwandiga napafahamu huna lolote.


Wacha kuanzisha vita ya mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo,utaumbuka bure
 
Zitto Kabwe , Maalim Seif na Act Wazalendo hata uwape miaka mitano hawana majibu ya haya maswali na walichokifanya zaidi ya usaliti .
Nivizuri sasa watanzania ndiyo watamjua vema Zitto kuwa yeye anatanguliza tumbo lake mbele na maslahi ya watanzania ni baada ya yeye kushiba.


Alifukuzwa cdm kwa tamaa zake za kutaka madaraka kwa papara
 
CHADEMA mnazidi kupotea, mnazidi kupoteza uhalali na kukubalika kisiasa. Watu huwa hawaishi kwa uhasama miaka yote ingawa uhasama wenu ni wa kimaslahi pia.

Wazanzibari wameona hawawezi kuishi kwa kununiana wakati wanaweza kuunganisha nguvu na kujenga nchi yenye kufanya shughuli za kimaendeleo zenye kupiga hatua haraka.

CHADEMA mnayo changamoto ya kupata uongozi mpya wenye maono mapya kabisa, huu wa sasa umeshapoteza muelekeo.
Hauna ujuwalo wewe zaidi ya kupalilia mrija wako usizibwe
 
Maalim ni mzee wa miaka 77 mnataka aendelee kuishi kwa uhasama mpaka lini?.

Tafuteni kiongozi mpya Mbowe keshashindwa mazima.
Mbowe hatoki cdm mkitaka nendeni mkanywe sumu maana hamna faida kwa taifa hili.
 
Mimi siungi mkono maridhiano hayo na wala sitayaunga mkono hata nikiwekewa bunduki kichwani .

Liwalo na liwe
Teh teh teh 🤣 kwani mkuu hata usipounga mkono kwani ni tatizo kwao?
 
Naomba nichangie kidogo kwa hatua iliyofikiwa leo kwa Maalim Seif kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwanza niseme mimi ni muumini wa maridhiano na ninaunga mkono "dhana" ya maridhiano iliyofikiwa leo pale Zanzibar.

Lakini ninapinga maridhiano haya yasiyo weka wazi msingi wa Maridhiano. Ninasema haya kwakuwa hadi sasa ACT na CCM hawajatueleza msingi wa maridhiano haya ni nini na hawajatuambia matunda yamaridhiano ya nyuma nini na kitendo cha leo kuweko maridhiano tena ni tafsiri ya kuwa maridhiano ya nyuma hayakuzaa matunda.

Nimesikiliza hotuba ya Maalim Seif leo, ni nzuri lakini haijajibu hoja za msingi za sisi tunaohoji msingi wa maridhiano haya. Imekuwa ni hotuba ya jumla zaidi inayo tulazimisha tufute machozi bila kutueleza kuwa kesho hatutalia kwasababu ya hili na lile.

Moja ya kichaka cha hoja wanachojificha wanaotetea ACT kujiunga na CCM ni hiki kinachoitwa "Siasa za Zanzibar zina namna yake". Hivyo hata tukihoji kwamba sababu zilizofanya 2015 wagomee zimetatuliwa ndipo wameingia tena au laaa? Wao wanatuziba kwa kujificha kwenye kichaka kinachoitwa historia ya siasa za Zanzibar.

Tumehoji hapa kwamba ni makubaliano gani ambayo ACT na CCM wameyaweka mezani hadi kufikiwa maridhiano ya leo ili kesho yasijirudie haya? Bado hatujibiwi tunarudishwa kwenye kichaka kanakwamba sisi hatujui historia ya Zanzibar.

Mfano Chadema imeweka mezani msingi wa maridhiano ya kitaifa kati yake na CCM ambayo ni 1. Kutambua kuwa uchaguzi ulikuwa batili, 2. Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, 3. Mchakato wa Katiba Mpya ya Warioba kuendelea

Pengine kuna wanachoshindwa kusema wazi kuwa maslahi ya Maalim na Wenzake yamezingatiwa kuliko malengo ya Wazanzibar ya kupata nchi yao ambao ndio msingi ulioasisiwa na CUF ya Maalim. Nani leo mtetezi wa Wazanzibar??

Jibu liko Pemba na Unguja!

_______________

Nakukumbusha, ni mwezi wa Sikukuu, Watu watano watapata ZAWADI ya kitabu cha Ujasusi kwa 20,000 tu popote ulipo badala ya 80,000.

Lipia 20,000/= kwa

TigoPesa 0715865544
M-Pesa 0755865544
Airtel Money 0788887887
HaloPesa 0624452045
(Yericko Nyerere)

Tuma majina yako na ulipo

(Dar ni free delivery)

Nje ya Dar nauli 8,000/=

Instagram Follow @yerickonyerere

View attachment 1644809
Kila chama kina aina yake ya maridhiano, hayo maridhiano ambayo nyie chadema mnayataka hayawezi kutokea until Jesus comes back

Wao ACT wana Aina yao ya siasa, sio mambo ya kususa...

Wamepata platform mzuri ya kupata ruzuku na kuingia kwenye baraza Mlitaka wasuse then wao kama wanasiasa wafanye kazi gani?

Nyie chadema endeeni kususa, endeleeni kudai Ben saa nane yuko wapi, endeleeni kudai waliompiga Lisu risasi,
 
Msingi wa uanzishwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ilikuwa ni nini?

CCM na ACT-Wazalendo walichofanya ni kutimiza takwa la Katiba ya Zanzibar 1984.

Kama ndani ya katiba kuna maridhiano basi walichofanya ni kutekeleza kilichoko ndani ya katiba.

Inanishangaza ulipoandika ''Mfano Chadema imeweka mezani msingi wa maridhiano ya kitaifa kati yake na CCM ambayo ni 1. Kutambua kuwa uchaguzi ulikuwa batili, 2. Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi, 3. Mchakato wa Katiba Mpya ya Warioba kuendelea''

CHADEMA mnataka maridhiano na nani? Kwa lipi? Kwa msingi wa katiba ipi?
Katiba ya Tanzania inasema, the winner takes all. Kwa Tanzania bara uchaguzi umeisha!

Ninajua baada ya muda CHADEMA wataanza kupokea ruzuku za serikali lakini pia watapeleka wabunge wa viti maalum bungeni hata kama sio kina Mdee na kundi lake!
Ruzuku tayari wameshapokea
Hili la wabunge wanajipanga kufuta aibu yao kwanza

Ila nao mwisho wa siku Watashindwa tu
 
Back
Top Bottom