Tunakumbushana tu kuwa leo ni tarehe 1 July, 2023

"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu"

Huu mstari unanifikirisha sana, anyways tutafute hela.
Kuna mstari mwingine unaosema...

Tujifunze kuzihesabu siku zetu za kuishi duniani
 
Mwenyezi Mungu alitaka tuishi japo miaka 120.
......
Mwanzo 6:3
Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
......
Ila kutokana na uhalibifu wetu tunaishia kuishi miaka 70.
......
Zaburi 90:10
Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara.
 
Kasome na muhubiri sio ndefu soma yote tu " Mtume anasema yote ni kujilisha upepo maana maana wote mwisho wetu ni chini"
 
Tatizo ni misambwanda, hela inapukutika hatar mara paaap mwaka umeisha ukicheki unamiliki pumb tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…