real life skills
JF-Expert Member
- Jul 16, 2021
- 233
- 238
Acha uongo wa mchana kweupe wewe!Tulisaidie Taifa kwa maombi au kwa njia yoyote inayofaa. Awamu iliyopita Gachuma alikamatwa kwa tuhuma mbalimbali na kufikishwa mahakamani Kisha kunyimwa dhamana.
Wakati tukiwa kwenye sintofahamu kuhusu uhalifu aliotenda, Serikali ile ile, chama kilekile na watu walewale leo hii wameteu mtu yuleyule kwenda kwenye bodi nyeti ya Tanesco.
Naomba kujua kwanini hatuna utaratibu wa kuweka vigezo kupata watu kwenye taasisi nyeti na maeneo nyeti?
Kwamba wakati wa awamu ya Tano alionewa na kudhalilishwa bila hatia au imekaaje?
Gachuma hajawahi kukamatwa wala kutuhumiwa kwa lolote.
Nikukumbushe,yeye ndie alikuwa mwenyekiti wa kamati ya ukarabati wa kituo cha televisheni CHANEL TEN. Mwaka jana,Hayati Magufuli alimpongeza kwa kazi nzuri aliyofanya katika jukumu hilo wakati wa uzinduzi wa studio mpya za kituo hicho.
Acheni uongo na chuki zenu kwa serikali hii na kuanza harakati za kichafua watu bila sababu.