Tunalaani uwanja Chato, nchi hii upendeleo ulianza zamani Wachaga mkiongoza

tunamlaumu kwa kutumia rasilimali na kodi zetu vibaya!
Si unawaona hata levo ya chama wanavyoiga kuwa wakubwa? Ukiona mkuu wa chama cha upinzani hataki kukosolewa, anaajili walinzi, hsogelewi hovyo na anatoa amri za kufukuza wanachama, ujue akiwa rais ni tatizo bial kiwango. Hii ni wote. Hata CHADEMA, UDP ya Cheyo wakati ule na Jidulamabambasi, CUF ya Lipumba, TLP ya Mreman, nk. Wote hao wanapenda ukubwa wa kiwango hicho. Hawana sifa za kukosoa wenzao.
 
Kuna mambo uliyoyaandika ni upuuzi na ujinga mkubwa.

Hivi uwepo wa ongezeko la mikoa kama Katavi, Geita, Simiyu na Njombe ulikuwa ni upendeleo wa Pinda? Unajua umbali wa kutoka Sumbawanga mpaka Kigoma? Ni karibia 550km. Kutoka Mza mpaka Shinyanga ni 164km. Nitajie ni mikoa gani ambayo makao yake makuu yana umbali kati yao ya kiwango hicho.

Uwanja wa ndege wa Songwe haukujengwa kijijini kwa kiongozi yeyote, ulijengwa Mbeya mjini. Mbeya ni makao makuu ya centre kuu ya kibiashara kwa kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Utailinganisha vipi na kijiji cha Chato?

Lakini tukiwa wakweli kulazimisha ujenzi wa majengo makubwa Chato kama vile majengo ya ghorofa kama yale ya CRDB wakati wateja ni kiduchu, majengo ya TRA wakati walipa kodi ni kiduchu, bohari kuu ya madawa ya kanda, uwanja wa kimataifa wa ndege, n.k. ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa. Jambo hili linastahili kukemewa, kulaaniwa na kupingwa na yeyote aliye mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu na anayetii dhamira ya ubinadamu wake.

Chato inastahili huduma kama ilivyo sehemu nyingine zote lakini kwa kuzingatia mahitaji halisi. Kuna baadhi ya hivyo vitu vilivyopelekwa Chato, hakuna ambaye angelalamika kama vingepelekwa Geita au Mwanza.

Mwanza CRDB hawana hata jengo moja la ghorofa lakini limeenda kuwekwa Chato. Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza ulioanza wakati wa Kikwete, unasuasua mpaka leo haujakamilika lakini wa Chato umejengwa kwa muda mfupi na kukamilika kwa muda mfupi. Hata sisi wa Mwanza hatufurahishwi na jambo hili. Kwa walio mbali wakisikia kila wakati kuwa yupo Mza wanaamini kuwa Mza inapendelewa lakini siyo kweli. Inaypondelewa ni Chato wala siyo Geita, Mwanza au Kagera. Hakuna chochote kikubwa kilichofanywa Mwza labda mradi wa usambazaji maji unaoendelea. Kila mara anasikika yupo Mza lakini ukweli haya ni mapitio ya kwenda kwake. Anapokwenda kwake anatafuta kitu kidogo kilichopo Mwza au anakizindua au anakitembelea ili itangazwe kuwa yupo Mza kikazi.

Ukweli ni kuwa tuseme wazi kuwa UBAGUZI na UPENDELEO hatuutaki kwa sababu mbegu hiyo ikimea itaangamiza Taifa.
 
Umeandika vizuri hayo yote yangefanyika kwa kuzingatia mahitaji halisi sio ishu ila yamefanyika kwa viwango vikubwa sana unless Chato iko mbioni kuwa makao makuu ya mkoa na bahati mbaya rais anafanya bila hata aibu sijui kwa nini
 
Pole
 
Mkuu upo vizuri
 
Our politician do not think locally ndio maana wanashindwa kuwasaolidia wananchi wanaowawakilisha. Hawajui mahitaji halisi ya wananchi. Wanawaza na kuwapelekea Vitu vya kifahari. Wananchi wa majimbo ya vijijini kama Chato wanahitaji Shule nzuri, maktaba za kusomea, nyumba nzuri na maji. Wakipewa elimu haitaoza na hakuna atakayeweza kupuuzia. Hivyo vingine, akiondoka tu kiongozi anayepush vinabaki kuwa magofu.
 
Kwani CHATO hawaishi watu na hawastahili kuwa na Hivyo vitu?

Kwanini huulizi KIA, ?

RAIS MAGUFULI JENGA UWANJA SIYO HUO TU, BALI TUJENGEE MWINGINE WILAYA YA NZEGA BOMBADIA ITUE NZEGA.

KODI TUNALIPA WOTE,

NZEGA TUMESAHAULIKA SANA
 
Nilichogundua Ni kwamba, Wachaga hawataki Makabila mengine yale keki ya taifa, na Wasukuma wanapindua meza, kuakikisha Chaga Empire inakwama. Sisi Waluguru tunawatakia ligi njema. Magufuri baba, tukumbuke na sisi Moro, wachaga wametutesa sana.
 
Kwani CHATO hawaishi watu na hawastahili kuwa na Hivyo vitu?

Kwanini huulizi KIA, ?

RAIS MAGUFULI JENGA UWANJA SIYO HUO TU, BALI TUJENGEE MWINGINE WILAYA YA NZEGA BOMBADIA ITUE NZEGA.

KODI TUNALIPA WOTE,

NZEGA TUMESAHAULIKA SANA
Atatujengea tu mkuu usiwe na shaka anatekeleza ilani ya chama chetu pendwa. Hawa wanabwabwaja ni wivu tu unawasumbua
 
Mimi nadhani swala kubwa hapa ni "upendeleo na ubaguzi" kwa misingi ya umaeneo, kabila au ukanda. Nimepitia majibu mengi humu kama si yote nimesikitika. Sijaona hata mmoja aliye tayari kukemea tabia hiyo. Ninacho ona ni makundi mawili:-
  1. Wanaofurahia hali hiyo,
  2. Wanao kerwa sasa na hali hiyo.
Wanaofurahiya hali hiyo wanaendeshwa na mambo mawili:-
  • Siasa (political affiliation) wapo katika upande unao tawala.
  • Ukanda; wale wanaodhani sasa wapo kwenye ukanda unaopendelewa, yaani nao zamu yao kutesa kwa zamu.
Wanaokerwa sasa na hali hiyo:-
  • Siasa (political affiliation), wako upande pinzani kisiasa.
  • Ukanda; wale wanaodhani sasa ukanda wao haupewi kipaumbele.
Kwa kweli wote hawa hawana tofauti, na maoni yao yatakuwa yakibadilika kutokana kwa wakati huo wanajiona katika fungu au kundi lipi!

Nashuhudia, humu wale wanaokerwa sasa hawako tayari kukiri na kukubali upendeleo waliopata na walau kusema neno moja la kuonesha japo lilifanyika kwao wakati huo halikuwa jambo jema; bali wanatetea na kutafuta uhalali wa kukemea hili la sasa.

Kadhalika, wale wanaofurahia, nao wapo tayari kulaani upendeleo uliofanyika maeneo yasiyo yao wakati huo (kama kweli ulikuwepo) laki hawawezi kukemea upendeleo unaosemwa sasa (kama kweli upo).

Wengine wapo tayari kukemea upendeleo kwa sababu unaonekana kufanywa (kama kweli upo) na kundi wasiloliunga mkono kisiasa, huku wengine wakiunga mkono kutokana upendeleo huo (kama kweli upo) unafanywa na kundi lao kisiasa.

Kwa hiyo wote hawana tofauti ni swala tuu la fursa ndo msingi wa kelele zao na si msukumo wa uadilifu. Niyo wale wasemao ukikipata tumia ukikikosa jutia; kutesa kwa zamu.

Dunstan Buberwa
 

Sahihisha na hii:
When someone is low, when they have no credibility, no honesty, no elevation of their private self, they seek to lower all others with their creation of a false reality in which they aren’t failing — everyone else is. In fact, the most common survival method of insecure narcissism is to flip undesirable traits in themselves onto those that created those feelings, then attach some other magnanimous and likely untrue quality to themselves.

Any location within URT is Tanzania. Hayo ya Uchaggani na Chato yatabaki kuwa parochial perception surported by other equally pathetic souls. Get this, TRIBALISM has no locus in here, be Chato or elsewhere. T
 
Umeeleza ukweli mtupu, na atakayekupinga ni Mbaguzi namba 1
 
Subili msumari wa moto uingie. Vumilia tu
 
Ukweli mchungu huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…