..katika nchi za wenzetu ukiwa INTOXICATED hutakiwi kabisa kuonekana eneo la kazi.
..sasa huyu mwenzetu kalewa chakari anapewa ruhusa ya kufanya uchunguzi wa kifo cha mtu.
..inasikitisha lakini, MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!!!
JokaKuu,
Siyo wee peke yako umekaa nchi za wenzetu. Juzijuzi nilikuwa nimetembelewa na jamaa yangu anayeishi nchi za watu na yeye ni Dr. na tukaanza kuongelea juu ya ulevi wa Shaba. Akasema kuwa hata yeye sehemu anayofanyia kazi, yule Boss wa hiyo sehemu ya maiti, siku zote akimsogelea huwa anaisikia harufu ya Pombe.
Shaba hakuwa anatibu watu ila kuchunguza kisa kilichosababisha kifo. Hivyo hakuna pressure kuwa atakosea mtu afe mara ya pili au afufuke. Na maadamu alikuwa akifanya kazi yake bila shida bila kujali kalewa namna gani, walikuwa wanamuelewa mazingira ya kazi anayofanya na kwamba kama una akili timamu, huwezi kudumu pale, labda wee ni Zombe.
Pili, lazima ujuwe kuwa Shaba na pombe zake, kafanya kazi hadi nje ya Tanzania. Alikuwa akikaribishwa kwenye mikutano na semina nyingi sana miaka hiyo. Ingelikuwa ni Dr. wa kawaida ni kweli kabisa kwamba wakinusa pombe tu, na hii bila ya kujali wewe ni ni Dr au laa, so longer uko kazini, wanakuitia Polisi na unapimwa palepale kama umelewa.
Hivyo kusema Miafrika hapa, unapatumia sipo kwani una uhakika sehemu za maiti, kwa mataifa mengine hao wahudumu wao huwa wako katika hali gani? Je umeshatembelea mataifa yote sehemu za maiti au unakisia tu? Hebu ondoeni hizo Complex zenu. Wazungu nao kuna wajinga wengi, masikini, ombaomba, waosha maiti, vibaka, walevi, homeless nk. Kama kuiba na wao wanaiba na tena wanaiba hasa. Sasa hiyo tofauti kubwa ya kwao na sisi iko wapi? Wao kinawasaidia tu kwamba wamepitia mengi hadi ikabidi waanze kuweka sheria kali sana ili viongozi wao wasiwe vibaka, maana wangelikuwa na sheria kama sisi, basi wangelikomba hadi.......
Hebu angalia huyu Rais wa RUSSIA, nchi ambayo wakati huo ilikuwa na silaha kubwa za kutisha na huku ikiwa nchi pekee iliyojenga Space Station (MIR) akifanya vitu vyake na huku kalewa. NA Russia hiyooo, ipo tu inadunda.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=R-z9wfueMAw&feature=related"]YouTube - Boris Yeltsin's finest moments[/ame]