Rogojin The Idiot
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 2,969
- 3,392
Miaka 40 sasa bila majibu
Ipo siku ukweli utajulikana. Hakuna anayeweza kuufunika ukweli wala interest zake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Miaka 40 sasa bila majibu
Muwe na umri wa kujua sio mambo ya kusikia uzushiKwa kweli ni bora alipotezwa, maana nyerere alishajua ameboronga, na alikuwa anatafuta pa kutokea, lakini hii kenge ikataka kuharibu mipango yake, akaona isiwe tabu
Kama vile karume alivyokuwa anapiga mikwara na kuvua koti, nyerere alikuwa ni mnyama
Nimeiona miaka ya 70 na 80Muwe na umri wa kujua sio mambo ya kusikia uzushi
Kwa mema yepi?Leo ni miaka 23 tangu Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine atutoke ghafla na kuacha simanzi na wingu la huzuni. Siku ile ya machozi na majonzi imebakia katika kumbukumbu za Watanzania wengi kama vile jana. Mfano wake ni kumbukumbu ya Wamarekani waliposikia habari za kuuawa kwa Rais John F. Kennedy.
Kila mtu aliyekuwa mtu mzima wakati ule anakumbuka vizuri siku hiyo alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini. Je pengo aliloliacha marehemu limeanza kuzibwa?
Je, kuna kiongozi yoyote ambaye anakaribia sifa na utendaji kazi wa Marehemu Sokoine? Leo tunamkumbuka Edward Sokoine.
Pata kidogo chini hapa toka kwa mkuu Kyoma:
AsaLeo ni miaka 23 tangu Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine atutoke ghafla na kuacha simanzi na wingu la huzuni. Siku ile ya machozi na majonzi imebakia katika kumbukumbu za Watanzania wengi kama vile jana. Mfano wake ni kumbukumbu ya Wamarekani waliposikia habari za kuuawa kwa Rais John F. Kennedy.
Kila mtu aliyekuwa mtu mzima wakati ule anakumbuka vizuri siku hiyo alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini. Je pengo aliloliacha marehemu limeanza kuzibwa?
Je, kuna kiongozi yoyote ambaye anakaribia sifa na utendaji kazi wa Marehemu Sokoine? Leo tunamkumbuka Edward Sokoine.
Pata kidogo chini hapa toka kwa mkuu Kyoma:
Leo ni miaka 23 tangu Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine atutoke ghafla na kuacha simanzi na wingu la huzuni. Siku ile ya machozi na majonzi imebakia katika kumbukumbu za Watanzania wengi kama vile jana. Mfano wake ni kumbukumbu ya Wamarekani waliposikia habari za kuuawa kwa Rais John F. Kennedy.
Kila mtu aliyekuwa mtu mzima wakati ule anakumbuka vizuri siku hiyo alikuwa wapi na alikuwa anafanya nini. Je pengo aliloliacha marehemu limeanza kuzibwa?
Je, kuna kiongozi yoyote ambaye anakaribia sifa na utendaji kazi wa Marehemu Sokoine? Leo tunamkumbuka Edward Sokoine.
Pata kidogo chini hapa toka kwa mkuu Kyo
japokuwa sikuzaliwa wakati wa utawala wake na kifo chake. Anastahili pongezi mpaka hivi leo. Nifahari ya Africa na TANZANIA
This means moreNdugu Mwanakijiji shukrani kwa kutuwekea Kumbukumbu ya Bwana Edward Moringe Sokoine,Ambao waliwahi kufanya kazi na huyu mtu watakubaliana nami kwamba alikuwa mtu wa watu na asiyependa makuu.
Siku ya Msiba wa Mzee Sokoine naikumbuka vizuri!,wengine tulikuwa ndio tunaanza utumishi serikalini, tulikuwa tupo Dodoma kwenye vikao vya Bunge ambapo Mzee Sokoine aliondoka mchana kuwahi majukumu mengine Dar, baada ya vikao vya Bunge.
Kwa maelezo ya wasaidizi wa Marehemu walipofika Dumila wilayani kilosa ndipo lilipotokea gari lililokuwa linaendeshwa na Mkimbizi Dumisani Dube na kuligonga gari la Marehemu.
Habari za ajali ya Waziri Mkuu zilifika Dodoma mapema,na watu wote waliondoka Dodoma kuwahi Morogoro ambako Marehemu Sokoine alikimbizwa kwenye Hospitali ya Mkoa.Nakumbuka majira ya saa mbili za Usiku aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (Mama Anna Abdalah), akifuatana na Spika wa Bunge Chifu Sapi Mkwawa (marehemu) na Daktari wa Mkoa Dr Msimbe (Marehemu) walidokeza viongozi wa Mkoa kwamba PM amefariki.
Mwalimu JK alilihutubia Taifa usiku huo huo, na kutangaza wiki moja ya maombolezo! Jamani nakumbuka ilikuwa siku ya Hudhuni mkubwa, Nchi nzima ilizizima kwa kuondokewa na kipenzi cha watu.
Tumkumbuke Marehemu Sokoine kwa kuimarisha Uongozi Bora na kujali Matakwa ya wengi! Tufuate nyayo zake kwa kuwajibika kwa Dhati na kuwa Watumishi wa kweli wa Umma wa wa-Tanzania.