Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu


Jokakuu,
Nashukuru umeliona hilo. Mie naanza sasa kuwa mpinzani wa hilo neno "Miafrika...." na zaidi nimeandika huko nyuma. Juu ya ulevi kazini nafikiri hapa tupo pamoja sana na mfano mzuri ni mtoto wa Makamba ambaye nasoma kuwa kafukuzwa kazi kwa ulevi. Ulevi si kitu cha kujivunia na unaharibu sana maisha ya watu. Kuna kipindi nilifikiri nitamzika mdogo wangu kwa ulevi ila Mungu bariki kaacha.

Siku tulionana ilikuwa kama vile namuona AMEFUFUKA. Hapa hakuna kusema tume-disagree. Tunapishana tu kuwa kuna watu inabidi tuwatreat kama special case. Narudia tena, mengine yotee, tuko pamoja kabisa. Kama ulivyosema, TURUDI KWA SOKOINE.
 
Jokakuu,

Lazima ujuwe kuwa kesi ya Shaba haijaanza leo. Shaba alikuwa mtu wa mkoa wa Mara kama Nyerere na wakati Katibu mkuu wa Rais ni Mzee Timothy Apiyo na yeye akiwa mtu wa hukohuko. Wawili hawa wasingeliruhusu ndugu yao aadhirike namna hiyo.

Check your facts sir.Prof Shaba SI MTU WA KUTOKA MKOA WA MARA.
Prof Shaba na kaka yake Austin Sahba asili yao ni Kusini nafikiri Mtwara na Prof alisomea shule kule Nyanda za juu Kusini Mbeya Tukuyu shule inaitwa Mpuguso, wakati kaka yake akifanya kazi Makandana Hospital ,Tukuyu!!
 
Last edited:

Mkuu nimekuelewa sana tu,ila umejibu posting yangu bila kunielewa mimi moja kwa moja,nadhani umeelezea vizuri lakini lengo halisi la swali langu lilikuwa ni tofauti.

Nimekulewa sawia uliposema kuwa kutokana na lack of expertise especially miaka ya nyuma ndio maana tukabaki kusikiliza everything wanachosema wataalam hao bila hata kuuliza kwasababu ndio the only available,na moral and ethical issue hazikupewa kipaumbele,hayo ni matatizo ambayo hata wenzetu walikuwa na bado wanapambana nayo na ushahidi kwamba sisi bado tunapambana nao upo hapa kwenye thread hii.

Kwa kifupi ni kwamba,bado hata sisi generation mpya tunakubali kumwamini Profesa huyo kwenye issue muhimu kama upasuaji ambao unahusiha life or death decision making,ama hata kuwafundisha wanafunzi ambao ndio the back bone of our country kuanzia utawala hadi utaalam na all kinda of couriers and professionalism za namna ya kuiendeleza jamii nk.
Kwamba wakifanya hayo yote chini ya ulevi wanakubalika,lakini wakisema kitu kama flani alipigwa risasi then tunachukulia ni just "Ulevi" Licha ya kwamba risasi hiyo aliyoitaja bado ilhusiana na kazi ake inayoheshimika...Sijui umenipata?
Otherwise nimekupata from your point of view in general.
 

Inawezekana.

Unajua hizi mara nyingi zinakuwa ni habari za kuambiwa.

Pia angalia mtu kama Asha Rose Migiro, alizaliwa Songea. Yeye na dada yake mama Malale, waliolewa na kuchukua majina ya waume zao. Hivyo Migiro waweza dhani ni mtu wa Morogoro na Mama Malale ni Mnyamwezi. Ila ukweli ni kwamba wote ni WAPARE.

Kinana alikuwa naibu waziri wa Ulinzi na kumbe MSOMALI. Ntagazwa alikuwa Waziri na kumbe sijui Mrundi? Kumbukumbu yangu inaniambia kuwa kaolea Uchagani na kwao ni mkoa wa Mara. Anyway, wajuvi wa mambo watatupa data kamili na ASANTE kwa kunirekebisha.
 

Mkuu,

Hiyo niliyoiwekea rangi nyekundu inaweka bayana kuwa hakuna ambaye anaelewa kabisa ni ufanisi wa kiasi gani uliokuwa unapatikana wakati Prof. akiwa amelewa. Huenda alikuwa anaandika vile alivyoona inafaa kwa wakati ule kwani hakukuwa na jinsi.

It is a remarkable observation!
 

Sikonge:

Nashukuru sana kwa maelezo yako na umetoa inputs kubwa sana. Tumekuwa na side shows nyingi katika thread hii.

Hivyo ngoja nirudi kwenye mada yenyewe na matamshi ya Dr. Shaba. Watanzania pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojua kusoma na kuandika, bado sisi ni watu wa Oral traditions.

Mara nyingi tunachukua story tulizosimuliwa na kuzimulia kama za kwetu na bila ya ku-verify source au kusimulia bila ya kuongeza chumvi.

Ukiwapanga watu kumi katika mstari na mtu wa kwanza apewe taarifa ya kumsimulia mtu wa pili kwa maneno yake. Na mtu wa pili amsumulie mtu wa tatu kwa maneno yake. Na process hii iendelee mpaka mtu wa mwisho. Ukweli ni kuwa mtu wa mwisho atakuwa na ujumbe tofauti kuliko uwe aliopokea mtu wa kwanza kutoka katika source. Na hili zoezi linaweza kufanyika katika chini ya muda wa dakika kumi tu lakini linabadilisha ujumbe wote.

Kifo cha Sokoine kilitokea miaka 25 iliyopita. Watu wanapeana ujumbe kwa kutumia maneno yao na sio maneno ya source yenyewe. Hivyo uwezekano wa kuwa Dr. Shaba alisema kitu kingine kabisa ni mkubwa sana kwa sababu tunasimuliwa kwa maneno ya msikilizaji.
 

Kumbukumbu zangu zinanionesha kuwa marehemu Austin Kapera Shaba alizaliwa Malawi na alihamia Tanganyika akiwa mdogo wakati huo wazazi wake (baba) wakuja Tanganyika kwa ajili ya kufanya kazi katika maeneo ya Mtwara / Masasi. Sasa kama Austin na Prof ni ndugu you can link the dot.
 

Jmushi1:

Nimekupata kuhusiana na hoja ya kupigwa risasi. Na kufafanua maelezo yangu ngoja nijaribu kutumia nadharia ya information propagation. Hili information iweze kufikia destination ni lazima vyanzo vya kutunza information na njia zinazopitia kusafirishia ziweze kutunza exactly copy of the original information.

Mpaka sasa hatuna uhakika kuwa chanzo chenyewe (Dr. Shaba) kilisema. Na kama kweli kilisema kilikuwa chakari. Njia zinazotumika kutuletea ujumbe bado zinaongeza chumvi au kushindwa ku-reproduce the exactly copy.

Kuna njia tatu tu za kumaliza majadiliano haya. Ya kwanza, ni kumpa Dr. nafasi ya kutoa maelezo yeye mwenyewe. Ya pili, kama kuna hard copy, itolewe. Ya tatu ni kufanyia tena uchunguzi mwili wa marehemu.

Zaidi ya hapo, kuna watu watasoma habari zilizopo JF na kuzisimulia kama vile walikuwepo wakati professor analonga.
 

Nani Mtanzania?

We!
 
Ahsante mkuu, Austin na Prof ni mtu na mdogo wake.Mimi nina habari kuwa wamekulia/kufanya kazi maeneo ya Tukuyu na Prof huwezi kumsengenya kwa kinyakyusa!!!
 
Sio kweli kwamba Arcadoga Chiledi alikuwa gari moja na Sokoine naona hapa mtuma ujumbe anapotosha watu. yeye allikuwa kwenye gari lingine akisoma Novel na sio kweli alikuwa gari moja na Sokoine huu ni upotoshaji.Japo mada yako inawezekana ikawa ajali ya kupanga ni possible kwaani kipindi hiko kulikuwa na vita ya wahujumu nchi naliyesababisha ajali ni msouth Afrika Dumisan Dube.
 
Katika safari ndefu, kiongozi anakuwa peke yake , mlinzi na dereva. Nyuma ya gari yake kuna escort na baada ya escort huwa kuna gari la kubebea wasiadizi wake km private secretary, press secretary.
Sokoine alifariki kwa sababu hakuwa amevaa mkanda (safety belt). Dreva na milinzi wake walipona kwa sababu walikuwa wamevaa mikanda.
Tukirudi kwenye hizi conspiracy theories, kama kuna mtu/watu walifanya hila na kumua Sokoine, ni kitu gani kinacho washinda ku msilence Shaba?
Wale wote waliyokuwa kwenye msafara je nao ni part and parcel ya huo mpango?
Hakuna siri zaidi ya mtu mmoja!
 
Nani Mtanzania?

We!

Wee Sura ya kwanza. Unafikiri hii dunia ni ile imeandikwa kwenye sura yako ambayo Mungu akampa ardhi Adam na Eva? Nani Mmarekani? We!
Sasa nenda USA kichwa kichwa uone. Pipa hilo, nenda hata South Africa uone kazi. Nafahamu watu kibao waliozaliwa Tz na ndugu wote wako Tz ila kwa sababu alibadili makaratasi, kila anapotua Kipawa, basi analipia viza dola 100. Nani Mtanzania!!!!!
 

At one point, Mwalimu JKN aliwahi kutoa maagizo Prof. Shaba apelekwe nje na akapelekwa ili kujaribu kumsaidia kutatua tatizo la ulevi. Nakumbuka aliweza kuacha pombe kwa kipindi fulani lakini baadaye akarudia tena kunywa. Katika watu waliobarikiwa kuwa na akili mingi kichwani Prof. Shaba ni mmojawapo. Labda ndio maana hata akilewa hatetereki anafanya kazi yake kikamilifu na akitoka bar hakosei njia anarudi kwake bila taabu!

Kuhusu Acadoga Chiledi, nakubaliana kabisa kwamba ajali ya Waziri Mkuu Sokoine ilimchanganya akili! Acadoga alikuwa mtu wa karibu na Sokoine, na Sokoine alimpenda ndio maana aliweza kumchagua kuwa mmoja wa wasaidizi wake/Mwandishi wake wa Habari. Acadoga aliona fahari kubwa kwa uteuzi huo na kamwe asingeliweza kumuua boss wake.

Nasikitika kusikia Acadoga kumbe alifariki. May his soul rest in eternal peace.
 
At one point, Mwalimu JKN aliwahi kutoa maagizo Prof. Shaba apelekwe nje na akapelekwa ili kujaribu kumsaidia kutatua tatizo la ulevi.

Yaani hata hili linahitaji kupelekwa nje? Hehehehehe...Miafrika never cease to amaze me!!
 
Mbona imani za jadi haziingii katika mjadala huu, wakati wengi hapa mnaamini kuwa alilogwa na ghost lake lilikuwa linaonekana kwenye ukumbi wa bunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…