Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Sikonge,
..hii posting yako imenishtua kiasi cha kunilazimisha kupitia posting zangu kujua ni kwanini tumefika hapa.
..nadhani nilikosea kutumia ule msemo maarufu wa "Miafrika..." kwa msingi huo basi naomba radhi kwa hilo.
..lets agree to disagree kwenye suala la Prof.Shaba, badala yake turudi kwenye mada kuu inayohusu kifo cha Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine.
Jokakuu,
Nashukuru umeliona hilo. Mie naanza sasa kuwa mpinzani wa hilo neno "Miafrika...." na zaidi nimeandika huko nyuma. Juu ya ulevi kazini nafikiri hapa tupo pamoja sana na mfano mzuri ni mtoto wa Makamba ambaye nasoma kuwa kafukuzwa kazi kwa ulevi. Ulevi si kitu cha kujivunia na unaharibu sana maisha ya watu. Kuna kipindi nilifikiri nitamzika mdogo wangu kwa ulevi ila Mungu bariki kaacha.
Siku tulionana ilikuwa kama vile namuona AMEFUFUKA. Hapa hakuna kusema tume-disagree. Tunapishana tu kuwa kuna watu inabidi tuwatreat kama special case. Narudia tena, mengine yotee, tuko pamoja kabisa. Kama ulivyosema, TURUDI KWA SOKOINE.