Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Ndugu yangu watu hapa are discussing the "circumstances" how Sokoine died, because always there is no clear explnation; and those who know it were not given opportunity to explain. Note that he was a Prime Minister, na mie sielewi, kwa nini Prime Minister agongwe na gari na kufa kirahisi rahisi hivyo.
Vile vile nakushangaa sana unavyo-compare ati wanao-discuss hii thread na "fortune tellers/horoscope"; I always respect ideas, but I sometimes question on superstitious thinking; kwa mfano you're among the people who do not believe that Ballali is dead; you're more superstitious!!

IO

msamiati mpya kuhoji ni sawa na kuagua kwa wenzetu hawa. Kwa kuwa tu wanataka kila hoja walete wao tu wakileta wenzao lazima watafute vijineno vya kuiua hiyo hoja.
 
mchonga aliuwa wengi tu, huyo mzee sijui hata kwanini tuna mtukuza kiasi hiki, yeye ndio sababu kubwa ya wa bongo kubaki mbumbumbu na masikini, kila kitu alibana wakati yeye akitesa na mademu wa kizungu huku akipata champagne, cha maana alichofanya ni hakuiba, si mnaona familia yake ilivyo choka.

yani alikua roho mbaya hata kwake binafsi, huwezi kuwa raisi halafu ukafa masikini, hiyo ni laana ya mwenyezi mungu. hii nchi asinge chukua mwinyi basi mpaka leo kungekua tunavaa nguo za vitenge na bata shoes.
 
Hata kama mtu ulikuwa na issues na JKN, kumsingizia kifo cha sokoine is wierd. JKN alikuwa tayari kuachia madaraka na kwake yeye succession was more important than anything. Ndo maana akatoa idea ya kung'atuka pamoja na wafuasi wengi wanafiki kumuomba aendelee alijua kuwa ni unafiki tuu.

Kifo cha Sokoine ilikuwa ajali tu?? Kwa kiwango kikubwa ajali nyingi zikishatokea huwa kuna mysteries sorrounding the environment especially kwa watu ambao conspiracy is their thinking. Ajali ndo maana inatokea. Dreva hawezi kuelezea ukweli hata siku moja especially inapokuwa yeye amefanya kosa.

Lakini wale tunaoendesha magari bara bara za Dar tunaona jinsi madreva wa serikali walivyo reckless katika driving. We kasimame along morogoro road anywhere after Ubungo towards Mbezi uone ST's, SU's na SM's zinavyopambana na madala dala kufanya dangerous overtaking, kupita kushoto pembeni mwa bara bara na kuchomekea!! These people who drive these cars are really MAD na siku wakilichomeka Shangingi mtaloni tunasingizia wabaya wetu. It is disguisting!!

Back to kifo cha Sokoine. JKN hakuwa na motive ya kumuua sokoine. Na hao wengine wote wanaotajwa (Kawawa, Msuya, Jumbe, ... sijui nani) naona ni watu wenye damu za kunguni tuuu! Hawaishi kusingiziwa mambo. Lakini I tell you kama mwalimu angejua mmoja wapo aliyeshiriki au kama ni wote alikuwa na uwezo wa kuwasambaratisha wote na kuinua wengine kipindi kile kile. Ndo maana watu baada ya kuona mwalimu hakumwangushia rungu mmoja wao wanahamishia lawama zao kwake. Mwalimu aliujua ukweli na asingemsingizia mtu. Time will always prove mwalimu was innocent.

Kuendelea kupeta kwa watu hao baada ya kifo cha EMS ni ushahidi tosha kuwa mwalimu hakuwasuspect. Sidhani kama kuna mtu alikuwa more informed than JKN wakati huo. Na sidhani kama kuna mtu alikuwa na mikono ndani ya UWT kama JKN. Sidhani kama mchezo mchafu kama huo ungechezwa na JKN asijue au akajua akaamua kukaa kimya tu na kuendelea kula sahani moja na watu ambao wamemuua mtu aliyemuamini vile.

Hizi theory zote zinagonga mwamba. Inabaki moja tuu, mwalimu mwenyewe!! Which is absurd given the timing. Jambo moja linalobaki plausible na ambalo hatulitaki ni hili tuu, AJALI WAS REAL.

Na huyo msouth hata kama wangemkaanga isingesaidia chochote, Sokoine was already dead. Kwamba alipelekwa uingereza, mmmh, hamna ushahidi. Ni mtu tu unaamua kusema, kwa kuwa wengine hawajui, wanakubali au kukataa.

Lakini kuikubali hiyo theory kwamba hakufungwa alipelekwa Uingereza bila kuwa na ushahidi, unahitaji kuwa umeshajenga consipiracy kichwani mwako!
 
FMES,
Nadhani wakati Sokoine anafariki Mzee Mzena alishastaafu. No?

- Sawa sawa je Kolimba alishastaafu naye? Halafu inawezekana vipi kwamba baada tu ya kumuua Sokoine hawa kuuua wengine maana huwezi kuuua mmoja tu ukaridhika au?

FMES!
 
Kama ni kweli Sokoine aliuliwa, mbona hatuna intelligence report yoyote kuhusu hilo? Mimi naamini kuwa hapa JF wapo watu ambao kwa njia moja au nyingine wanapata access to investigation reports za hapa nchini.

Hili la Sokoine limebaki mystery hadi wtu wnaanza kumsingizia mpendwa wetu Mwalimu Nyerere (may his soul rest in peace). kwakuwa hakuna taarifa za zinazoonyesha kuwa kifo cha sokoine si ajali, sioni ni kwanini sisi tuanze kumtafuta mchawi.

Ni kweli kuwa intelligence wakati wa Nyerere ilikuwa nzuri sana, lakini si kweli kuwa Mwalimu angepaswa kujua kila kitu. Kwamba dereva aliyegonga gari la sokoine alikiri kosa, si ajabu kwani it is true aligonga. Mimi nadhani hoja hapa ni kama kifo chake kilitokana na uzembe au vinginevyo.

Siamini kuwa Waziri Mkuu angeweza kusafiri bila msafara unaoongozwa na polisi, na kama msafara ulikuwepo, ho could that vehicle be allowed to proceed na kumgonga EMS?
 
Je waweza kuwa na uhakika alikuwa na magari mangapi katika msafara? Je ni kwa nini alikataaa ndege siku hiyo na akaamua kuja wa gari? Who convinced him? Ukitegua maswali hayo muhimu then I will concide with you.

Maarifa,

Hapa hata mie nimeuliza na bado sijapata jibu. Mwenyewe kwa macho yangu niliiona ndege ya RAIS (nyeupe na makelele saana) ikipita na baadaye tukasikia ikitua uwanja wa ndege AREA C/Makole. Baada ya muda fulani tukasikia ikiondoka na kila mtu akajua kuwa SOKOINE kashaondoka.

Hivi ndege ya JKN ya wakati ule, kuna mtu anafahamu ilikuwa inaweza kubeba watu wangapi? Isingewezekana yeye Sokoine na hao akina CHiledi, Kolimba nk kupanda ndege hiyo na kurudi wote Dar? Hivi kusema "alikataa kupanda ndege na akaamua kurudi kwa gari na wenzake" ni sababu inayoingia akilini? Kwenye ule msafara, si kila mtu alikuwa kwenye gari lake, jambo ambalo kama ingelikuwa kwenye ndege, angeliweza hata kukaa karibu na wenzake na kuendelea na majadiliano. Kukija tokea mtu anipe SABABU YA KWELI YA SOKOINE KUKATAA KUPANDA NDEGE, sintaweza kuwa na uhakika wa asilimia 100 kuw ilikuwa ajali ya kawaida.
Vinginevyo dawa ni moja tu nayo ni kuwa siku moja kulifukua kaburi la Sokoine na UKWELI UANIKWE. Hii itamaliza mzizi wa fitina kama Shaba alisema ukweli au alikuwa KALEWA CHAKARI.
 
FairPlayer,

Ni kweli miaka ya 90 katikati nilianza kusoma habari za Chiledi akiwa Zimbabwe na baadaye kama kumbukumbu zangu ziko sawa, nilisoma sehemu kuwa AMEFARIKI. Ila huyu bwana mwaka 90/91 nilikuwa naonana naye hapo Dar akifanya kazi SHIHATA na si Zimbabwe.

Huko alikuja kuenda baadaye na ni tofauti kidogo na maelezo ya Semi kuwa BAADA YA KIFOCHA SOKOINE, alikuwa mtu wa kukimbiakimbia.
 
Hivi tunaamini kuwa hii misafara kweli huwa inakuwa planned perfectly? Tunapoona hayo mashangingi yakichanja mbuga kwa 150KPH, do we think everything is perfectly planned. No way, kikwete asingepigwa mawe!

Kuna makosa mengi ya kibinadamu yanafanyika katika kupanga hii misafara na if disaster strikes, unadhani wapanga misafara watakubali? Kwamba walifanya kosa wakam-expose kiongozi? Hakuna mtu anayespeculate makosa ya wapanga misafara na ya kwenye misafara yenyewe.

Ukweli ni kuwa makosa mengi huwa yanafanyika na viongozi wanakuwa exposed mara nyingi tuu. Angalia Mwinyi alipopigwa kibao, security was very lax. Kama angechomwa kisu tungesema nani kapanga? Hawa watu wanapofanya makosa kama hayo lazima wafanye cover-ups. Ni hizi cover-ups ndo hufanya ajali nyingi zionekane mysterious kuwaacha watu waki-guess what happened.

Muulize Dreva yeyote baada ya kupata ajali. Atakuwa very protective na hakuna anayekiri kuwa hapa nilikosea hiki na kile. Watu hulaumu hata majini, halucinations, etc. 'niliona mtu kati ya barabara nikajaribu kumkwepa gari likaingia mtaroni' - kumbe alilala. Hizi mysteries zinazo-sorround mazingira ya kifo cha EMS ina hallmarks za cover-ups za wahusika wa huo msafara. Kuna kitu walichemsha wakam-expose kiongozi na disaster ikatokea kweli. Nani atakubali kuwa tulikosea??? Hizi mysterious na conspiracy theories zinawasaidia sana hawa wanausalama ku-cover their asses.

The most plausible explanation ni kuwa, kulikuwa na makosa ya kiutendaji katika kupanga msafara na ndani ya msafara wenyewe. Haya makosa hakuna atakayeyakiri for ever and we will keep guessing!!
 
acheni speculations za ajabu ajabu sokoine alikufa kwa ajali ya gari tu hakuna zaidi.hata mwakyembe angekufa msingeacha kusema kuna mkono wa mtu huku dereva wake akijua dhahiri makosa yake ya kiuendeshaji.sasa kila anayekufa kwa ajali ana sababu ya kusingiziwa kuuwawa tuu.kwani siye watz tukipingana au kuzidiana nguvu za hoja basi tunauana kwa ajali ooh kuserereka oooh safari za usiku n.k je madereva hawa wanaouwa watu kibao kila kukicha basi zima watu kumi ,saba,hamuwasemi ila wa viongozi ndo tu wanasababishiwa vifo???tatizo lipo katika elimu ya barabarani kwa madereva wetu,wawe wa viongozi wawe wa magari ya abiria,malori n.k hakuna hata mmoja mwenye elimu ipasayo ya kuendesha magari.achilia mbali wale wanajifunza katika chuo cha taifa cha usafirishaji (nit) ambapo ni ubabaishaji mtupu,si lolote si chochote kwani hata hao wakufunzi wenyewe hawakuwahi kuendeshagari zaidi ya nadharia tuu.leo hii katika barabara za jiji la dar es salaam mtembea kwa miguu hana uhakika wa kufika salama aendako kisa hofu ya kugongwa na wendawazimu hawa tunaowaita madereva!!!hakuna dereva wa kweli hapa bongo wote ni walenga madaraja na wauwaji wa watu tuu!!!elimu mathubuti inahitajika ili waendeshao vyombo vya moto,waendao kwa miguu na watumiaji wengine barabara wapate kupona.saokoine ,salome mbatia na wengine waliokufa barabarani ni kwa uzembe wa madereva tu na wala si vinginevyo.


mkubwa usijumuishe ajali zote kuwa zinasababishwa na uzembe wa madereva, kuna circumstances ambazo unaweza kuona tu it was a set up, mazingira ya kifo yanatatanisha, watu wanaona mbali hawakurupuki kusingizia kifo cha mtu tu. Acha uzalendo usiokuwa na mpango, na balali je?
 
Nafsi yangu nafikiri Kipimapembe is right, kuna umuhimu wa kupunguza speculations! Siyo kwamba fouls haziwezi kufanyika lakini too much speculations pia huondoa uwezo wa mtu kuangalia realties.

Wanasemage 'You are what you feed your mind'. Kwamba nani alifanya nini, ultimately there is a divine justice. Hapo kila kitu hadharani, hakuna cover ups! Na ukweli ndio utaanikwa. Mchana mwema.
 
Hamna kitu kinachoniumiza kichwa kama kumbukumbu ya kifo cha kipenzi chetu sokoine.

Ila ukweli utadhihiri tu, hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe.
 
kazi ipo ila always truth will prevail hata miaka 100 tutakuja jua tu.....ipo siku tena si nyingi...keep hii thread live
 
RIP Mr Sokoine ,he was a greatman and leader that Tanzanian where blessed with. I don't bother with all doubts arised here, because if there is a foul play someone will answer it to Almighty God.
 
Hii ni burudani. Hivi Tanzania hatuna waandishi kama Dan Brown. Yaani hii ni Da Vinci Code.

Kama watu mnaweza kupata mikataba ya Buzwagi, hivi autopsy ya Sokoine si inakuwa kitu kidogo tu? Au walichoma moto?

Anyway, katika ajari watu wanakuwa-traumatized. Maelezo yote kuhusu huo mwandishi wa habari zinaweza kuwa posttraumatic stress disorder.

Mnataka mtu aliyeshuhudia ajari kama hile na kumwagiwa damu atoke akiwa na akili timamu wakati mnamshuku kuwa yeye kahusika? Err no.
 
Nakumbuka miaka ya mwishoni mwa 80 kuelekea 90 nilisoma kitabu kimoja cha KGB kikielezea namna ajali ya Samora Machel (RIP) ilivyopangwa na kutekelezwa. Ilichukua mda mrefu jamaa wa CIA na wenzao wa Kusini kujua ratiba na kupanga namna ya kuenenda na hiyo ratiba ya rais ya mwaka mzima. Na matokeo yake walifanikiwa kwa asilimia mia moja. Mpango ulikuwa wa muda mrefu suala lilikuwa wasikosee ktk utekelezaji wake.

Vivyo hivyo nikiangalia suala la Moringe naona kuna pazia ambalo limefunika zile indoor plumbing za ajali yake. Na kwa ushahidi wa kimazingira unaleta mashaka kwenye jamii basi ninatilia shaka sana UZALENDO wa wengi wa watawala wetu.
 
kipimapembe said:
Back to kifo cha Sokoine. JKN hakuwa na motive ya kumuua sokoine. Na hao wengine wote wanaotajwa (Kawawa, Msuya, Jumbe, ... sijui nani) naona ni watu wenye damu za kunguni tuuu! Hawaishi kusingiziwa mambo. Lakini I tell you kama mwalimu angejua mmoja wapo aliyeshiriki au kama ni wote alikuwa na uwezo wa kuwasambaratisha wote na kuinua wengine kipindi kile kile. Ndo maana watu baada ya kuona mwalimu hakumwangushia rungu mmoja wao wanahamishia lawama zao kwake. Mwalimu aliujua ukweli na asingemsingizia mtu. Time will always prove mwalimu was innocent.

Kuendelea kupeta kwa watu hao baada ya kifo cha EMS ni ushahidi tosha kuwa mwalimu hakuwasuspect. Sidhani kama kuna mtu alikuwa more informed than JKN wakati huo. Na sidhani kama kuna mtu alikuwa na mikono ndani ya UWT kama JKN. Sidhani kama mchezo mchafu kama huo ungechezwa na JKN asijue au akajua akaamua kukaa kimya tu na kuendelea kula sahani moja na watu ambao wamemuua mtu aliyemuamini vile.

Hizi theory zote zinagonga mwamba. Inabaki moja tuu, mwalimu mwenyewe!! Which is absurd given the timing. Jambo moja linalobaki plausible na ambalo hatulitaki ni hili tuu, AJALI WAS REAL.

kipimapembe,

..i agree with you 100%.

..Nyerere asingeweza kumhifadhi mhaini yeyote yule aliyeshiriki kupanga mauaji ya Sokoine.

NB:

..baada ya kifo cha Sokoine, Kawawa alikuja kuwa Katibu Mkuu CCM, na baadaye Makamu Mwenyekiti. kwa nafasi zote hizo he had the full support of Mwalimu Nyerere.

..Cleopa Msuya alipelekwa wizara ya Fedha, baadaye viwanda na biashara, na alistaafu kama Waziri Mkuu. pia aligombea nafasi kuwa mgombea Uraisi CCM.
 
He was a Prime Minister of the United Republic of Tanzania, URT. He was knocked by a car (involved in a car accident):m

Yes: Who where there?
1. Mr. Mustafa Nyang'anyi - Leader wa msfara

2. Mr. Chuma - The driver who had a passenger in his passenger sit; Mr. Edward Sokoine. Had suffered a broken leg, where he is? He never testified!

3. Acadogo Chiledi - was sitting beside Mr. Sokoine during the accident!

4. The circumstance that Mr. Dube crashed the PM car, was not valid, another car was crashed; and even pictures are showing that the car which Mr. Sokoine was in was knocked from the back. His own Usalama wa Taifa knocked him from behind. But Mr. Dube was coming in an opposite direction, and then this car didn't show that it was knocked on the side (ubavuni).

5. A Prime Minister with such a popurality dies; at least there should be an investigation carried. A Task Force, Tume, or anything to investigate on the cirumstances of the death.

Let us be serious!!
 
Hapa kuna hoja kubwa mbili:

a. Sokoine aliuawa - hii ni hoja ambayo imekuwa ikisemwa tangu 4/12/1984 (alhamisi ile). Na kuna watu ambao hawakuamini amekufa na walisema amechukuliwa "msukule" na kuna baadhi waliapa "kumuona Dodoma". Magazeti ambayo leo tungeyaita ya Udaku yaliandika alleged apparitions za Sokoine hadi Nyerere kuja kusisitiza kuwa ni kweli amekufa.

Kama kuna mtu yeyote anajua kuhusu kuuawa kwa Sokoine mtu huyo yupo hai leo hii. Na kwa hakika haiwezekani awe ni mtu mmoja tu. Aliuawa wapi, vipi, na kwa malengo gani? Sasa kusema "nilisikia"... "nilisoma".. "naamini".. ni majaribio tu ya kujaribu kujenga hoja pasipo msingi mzuri. Tatizo ni kuwa hakuna Mtanzania anayekufa kwa kawaida! NONE whatsoever awe kiongozi au mtu wa porini.. we always have to find some irrational explanation.

Sasa, wakati mwingine ni mazingira ya kifo yanachangia mawazo hayo na wakati mwingine kunakuwepo na sababu ya kushuku mchezo mchafu kwani maelezo ya kifo au ajali yanagongana. Firikia, Mkuu wa Polisi amesimama (ambaye alifika mapema zaidi kwenye tukio) na kusema ni "shimo"; halafu bosi kutoka dar anasema "shimo halikusababisha kwa namna yoyote ile ajali" halafu huyo huyo anatoa pendekezo serikali itengeneze barabara na magari yasitumie matairi ya x,y!.. eh?

b. Kwamba Nyerere ndiye anahusika na kifo hicho.
Madai haya nayo yanatolewa kwa nguvu yakidai ukweli. Kwamba wanajua Nyerere alipanga, kuagiza, kusimamia na hatimaye kuficha ukweli juu ya "mauaji" ya Sokoine. Wanajaribu kutafuta motives n.k Lakini basi angalau basi chembe ya ushahidi wa aina yoyote ile basi angalau tujue pa kuanzia... mtu anasema alisikia maneno ya mlevi na akayaamini!

mwingine anasema Nyerere aliua watu wengi kweli, weka orodha basi na chembe za ushahidi wa mauaji hayo ya nyerere. Wataleta stori zile zile ambazo zimekuwa zikirudiwa rudiwa from time immemorial. Ni sawa na wale wanaosema "maelfu ya watu waliuawa katika operesheni vijijini".. tukiuliza basi tutajieni majina ya watu 50 tu waliokufa katika operesheni vijijini watu wanasema "nimesoma kwenye kitabu fulani"..


Well, madai yanayotolewa ni mazito na baadhi ya viongozi waliokuwepo 1984 bado wapo hai leo hii. Waulizwe au itakiwe kuundwa tume huru ya uchunguzi; si kina Dube bado wapo hai, kawawa si yupo, Malecela yupo, Salim yupo, Pinda yupo.. wote hawa wapo!... Msiniambie wanaogopa kuzungumzia kwa sababu wanamuogopa Nyerere!
 
Kama ni kuwa aliuliwa vile vile kuna possibility ya kuwa aliuliwa na watu wa nje ya nchi si lazima wawe wa ndani wenye chuki naye tu.
 
Back
Top Bottom