Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Tunamkumbuka Edward Sokoine - Mtu wa Watu

Mwanakijiji na wengine,

Mnaonaje tukimuenzi Marehemu Sokoine mwaka huu kwa vitendo kama JF?
 
Mzee Mkandara na Mzee Machumo, heshima zenu kwa mpigo

Mzee Machumo, sidhani kama naweza kunyamazishwa kwa mtindo huu usio na kichwa wala miguu. Ingawa sio jambo la busara kuwapuuza hawa watu, lakini ni vema kuwadhalau. Mzee Mkandara, acha utani! Sijuhi nisisitize vipi mpaka unielewe kuwa kutofautiana kihoja ndiko kunaniweka Jambo Forums. Usipoona mchango wangu, basi ujue kuna jambo la msingi. Hata hivyo, nitamalizia viporo vyangu vyote kama nilivyoahidi.

Labda kwa leo nikatishe mchango wangu katika hii mada ya Sokoine, ili nitoe masikitiko yangu kuhusu tathmini ya hali ya uchumi iliyotolewa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Daudi Balali, na kuwasilishwa kwenye kamati ya fedha na uchumi ya Bunge (Habari leo Mei 29, 2007). Tathmini ya Gavana imegusia jambo ambalo tumelijadili kwa ufasaha ndani ya mjadala huu wa Sokoine. Huu utakuwa ushahidi tosha kwa Mzee JokaKuu aliyechokonoa mjadala wa IMF na WB. Binafsi, nadhani Gavana Daudi amewapotosha wabunge kwa kutokuongea kiini cha sababu za kushuka kwa thamani ya shilingi na chanzo cha mfumuko wa bei.

Pia, siamini kuwa Gavana wetu ni mjinga kiasi cha kutokujua njia za kurekebisha tatizo la kushuka kwa thamani ya shilingi au kupunguza mfumuko wa bei. Naamini kuwa mapendekezo yake yanalenga katika upotoshaji na wala sio utatuzi wa tatizo lenyewe. Eti ili kuondoa mfumuko wa bei, anawashauri watanzania wathamini bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi. Eti ili shilingi isishuke thamani, watanzania waache kusomesha watoto wao nje ya nchi, hivyo kupunguza matumizi ya fedha za kigeni.

Gavana anawatoa kafara wananchi kwamba ndio wanasababisha mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilingi. Mbona hajawakumbusha watawala wetu kuthamini hospitali na madaktari wetu wanaozalishwa Muhimbili? Mbona hajawaambia viongozi waheshimiwa waache au wapunguze safari za nje zisizo na manufaa kwa nchi yetu? Au hizo hazipunguzi matumizi ya fedha za kigeni?

Lakini ni watanzania wangapi wanasomesha watoto wao nje ya nchi kwa kutumia fedha za kigeni? Ni kweli, kuna watoto wa kitanzania wanaosoma Kenya na Uganda. Hata hivyo, idadi yao ni ndogo sana kiasi kwamba haiwezi kulitikisa taifa kwa kushusha thamani ya shilingi. Pengine, wengi wao wanatumia fedha za madafu zinazobadilishwa mpakani kwa fedha ya Kenya na Uganda. Fedha ya Kenya na Uganda, haiwezi kutikisa fedha yetu kama zifanyazo Dola, Paundi au Euro. Hivi ni visingizio vyenye lengo la kulikimbia tatizo la kweli.

Gavana lazima atambue na amshukuru Mungu kuwa kuna watanzania wanaoishi katika nchi zinazotumia fedha yenye thamani kubwa duniani. Wengi kama sio karibu wote, hawasomeshwi na wazazi wao, bali wanajisomesha wenyewe kwa kuchakalika. Niliwahi kuandika mahala kuwa naheshimu sana watanzania walioshindwa darasa la saba na kidato cha nne, alafu wakaamua kutimua na kuchakarika katika nchi zinazoitwa tajiri duniani. Hawa kwangu mimi ni majemedari wa taifa letu. Wangekuwa pale nyumbani, ungekuwa ni msalaba mkubwa kwa wananchi. Wengi wao wangekuwa ni vibaka au mashine za kusambaza ukimwi.

Gavana lazima atambue kuwa idadi ya hawa majemedari ni kubwa na hawapati msaada wa fedha kutoka nyumbani bali wanachakarika kuzisaidia familia zao zilizoko nyumbani. Wanatuma dola au paundi ishirini, mia moja, miatano, mpaka elfu moja. Hizi fedha kutoka kwa kila mmoja wao, zikijumlishwa kwa ujumla wake kwa kipindi cha miaka michache, zinakuwa maelfu kama sio mamilioni ya dola au paundi.

Wakati viongozi wetu wanahujumu uchumi wa nchi yetu kwa kusaidia utoroshaji wa fedha za kigeni kwenda nje ya nchi, hawa majemedari wanasaidia uchumi wetu kwa kuingiza nchini fedha za kigeni. Vilevile, fedha wanazotuma zinawasaidia ndugu zao katika mapambano dhidi ya umasikini uliokithiri, zinasaidia kuanzisha miradi midogomidogo, kuwasomesha ndugu zao, kuajiri mafundi kwa ujenzi wa vibanda vyao vya kufikia, kununua bidhaa kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya familia zao n.k. Fedha inayotoka nje kwa mtindo huu, inazunguka ndani ya jamii ya watanzania. Mzunguko wa fedha ndani ya nchi, ni neema kwa taifa letu.

Mchango wa mtu mmoja katika uchumi wa namna hii hautoi taswira halisi ya umuhimu wa hawa majemedari katika kukuza uchumi wa nchi yetu. Hata hivyo, ujumla wa watanzania wote walioko nje wanaotoa mchango wa namna hii, unaweza kutoa picha nzuri kwa wale waliodhamilia kufanya tathmini ya kweli. Waswahili wanatukumbusha kuwa haba na haba ujaza kibaba.

Hoja za kiini cha kushuka kwa thamani ya shilingi na kinachosababisha mfumuko wa bei kwa nchi yetu tumezijadili kwa undani katika hii mada ya Sokoine. Kama Gavana wa Benki na wengi wa wabunge wetu wangekuwa washiriki wa mijadara ndani ya Jambo Forums, wasingethubutu kudanganyana kwa tathmini zisizokuwa na mbele wala nyuma. Wasiwasi wangu ni kuwa, hata Raisi wetu anapewa tathmini hizi za ubabaishaji.

Nimetoa kiambatanisho (pdf format) cha habari inayohusu tathmini ya Gavana wetu kama ilivyoandikwa na gazeti la habari leo. Nachukuwa fursa hii kutoa onyo kwa wote wanaotubeza kuwa Jambo Forums ni mahala pa gumzo au porojo. Kama wadau wanavyosema, hapa “tunakata issues”. Tunatabiri mambo kabla hayajatokea. Utabiri wetu sio wa kutumia majini kama ule wa Profesa maji marefu au Yahaya. Utabiri wetu umelalia katika kuzichambua issues kama unavyochamabua karanga. Tuna-argue kwa logics, tuna evidenced evidence, na mifano tele.

Gavana wetu analipwa fedha kwa kazi yake. Amefanya tathmini ya hali ya uchumi ambayo ameipeleka kwenye kamati husika ya Bunge. Wabunge nao wanalipwa fedha (posho) kukaa vikao ili kuisoma hiyo tathmini. Lakini tathmini yenyewe ni ya upotoshaji, ubabaishaji, na uongo. Hailisaidii taifa letu.

Nimenukuu baadhi ya paragrafu kutoka katika mabandiko yangu ndani ya hii mada ya Sokoine zinazohusu vipengere vya tathmini ya Gavana kwa wabunge wetu. Hii inamaana kuwa Jambo Forums tulikwisha fanya tathmini yetu kwa njia ya mijadara na kujua kuwa fedha yetu itaendelea kushuka thamani. Pia, tulikwisha jua kuwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi yetu zitaendelea kukumbwa na dhoruba ya mfumuko wa bei. Tulitoa sababu na mifano hai ya kwa nini mambo hayo yatatokea. Habari nzuri kwa wadau wote ni kuwa mambo yanatokea, na yataendelea kutokea kama tulivyotabiri. Habari mbaya ni kuwa, taifa letu linaendelea kuegemea katika ukingo wa shimo la giza.

Yafuatayo ni baadhi ya maelezo yangu niliyoyatoa wakati namjibu JokaKuu kuhusu majangiri wa IMF na WB. Ukimaliza kuyasoma, yachungulie maelezo mafupi yaliyotolewa na Gavana wa Benki Kuu katika kiambatanisho (pdf format). Nikipata ripoti nzima ya Gavana nitaituma pia.

Binafsi, naona kuna tofauti kubwa kati ya Masharti na Sera. Masharti si Sera, na wala Sera si Masharti. IMF na WB hawana Sera, bali wana Masharti ya mikopo. Nchi yoyote ikikubali na kuyatekeleza hayo masharti, inakuwa kama vile umeonja Ganja, au Cocaine. Itaendelee kuwa tegemezi wa ile mikopo. Nchi ikiwa “addicted” na kitanzi cha Cocaine ya mikopo, ni vigumu kujinasua kutoka katika hicho kitanzi. Ndio maana IMF na WB wanakuja na Cocaine, kwa maana ya masharti yatakayotudumaza na kuendelea kutufanya mafukara wa mawazo, au tegemezi wa fedha. Tutaendelea kukopa kwa kuamini kuwa bila Ganja, yaani fedha za mikopo, hatuwezi kutatua matatizo yetu. IMF na WB wataendelea kutukopesha fedha mpaka siku ya kiama chetu. (labda tuazime busara za Venezuela)

Kumbuka kinachotutia umasikini sio riba ya hiyo mikopo bali ni masharti yanayoambatana na hiyo mikopo. Mfano, masharti tunayopewa ni kwamba, tukitaka kuongeza kiwango cha bidhaa zinazouzwa nje (export), na kupunguza kiwango cha bidhaa tunazonunua kutoka nje (import), yatupasa kuifanya fedha ya nje iwe na thamani kuzidi fedha ya ndani ya nchi yetu. Tunaaminishwa kuwa hii nadharia itakatisha tamaa manunuzi ya bidhaa kutoka nje. Hivyo, tunatakiwa kushusha thamani ya fedha ya nchi yetu, mfano kama tulivyofanya kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania, na thamani ya dola, paundi au euro inapanda.

Hata hivyo, kwasababu tunakwenda kichwakichwa, hatukumbuki kuwa viwango vya uzalishaji katika jamii zetu ni vya chini sana. Tunategemea malighafi kutoka nje ili tuweze kuzalisha. Mfano wa bidhaa za lazima zitokazo nje ni Mafuta, Vitabu, Madawa, na Mbolea. Bidhaa zote hizi zinanunuliwa kwa fedha za kigeni. Thamani ya fedha ya nchi yetu inaposhuka na ile ya fedha za kigeni kupanda, gharama za uzalishaji zinakuwa juu na kusababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi. (Tathmini ya Gavana imekwepa sababu hii ambayo ni ya msingi. Mfumuko wa bei haupo kwasababu watanzania hawathamini bidhaa zinazozalishwa ndani, bali kwasababu hizo bidhaa ni za ghari. Sababu za bidhaa kuwa ghari nimezitaja)

Mfano mwingine wa hayo masharti ni kwamba, fedha wanazotukopesha, kamwe, haziwezi kutumika kuwasaidia wakulima au wafugaji wetu ili kupunguza makali ya uzalishaji (subsidize). Hata hivyo, Serikali zao, zinawasaidia wakulima wao ili kupunguza makali ya uzalishaji. Wanataka tufungue milango kwa maana kuwa bidhaa za wakulima wao ambazo ziko subsidized, zishindane na bidhaa za wakulima wetu ambazo haziko subsidized katika mfumo wa kitu kinachoitwa soko huria. Mwalimu aliwahi kusema Kirimanjaro hotel 1995, kuwa bingwa wa ngumi wa uzito wa juu hawezi kuingizwa ulingo mmoja na yule wa uzito wa kati. Alisema Burkina Faso and German haziwezi kuwekwa kwenye ulingo mmoja. (Tahmini ya Gavana inasema mfumuko wa bei wa Tanzania umefikia asilimia 7 wakati mfumuko wa bei wa nchi ambazo Tanzania inafanyanazo biashara ni kati ya asilimia 2.5 na 3. Hakuzitaja hizo nchi. Wakati viongozi wetu wanasalimu amri kwa hayo masharti, walitubeza kuwa uchumi wa kisasa unaendeshwa kwa nguvu ya soko. Sasa hizi ghiliba zinatoka wapi? Leo Gavana anatuletea takwimu za kushindwa kwetu zinazoonyesha kuwa German na Burkina Faso haziwezi kuwa katika ulingo mmoja)


Ingawa hizo nchi hazikutajwa, lakini baadhi ya nchi anazozisema Gavana kuwa tunafanyanazo biashara, mojawapo ni Marekani. Serikali yetu iliwekewa masharti na IMF na WB kuwa isiwape fedha (subsidize) wakulima wa Pamba. Hata hivyo, nchi ya Marekani inasaidia kupunguza makali ya uzalishaji ya wakulima wake wa Pamba kwa kuwapa fedha (subsidize). Wakulima wetu wanatumia majembe ya mkono na wale wa Kimarekani wanatumia Mashine za kisasa. Hata hivyo, Pamba inayotoka Marekani na ile ya Tanzania inauzwa kwa mashindano katika soko la pamoja bila kuangalia upendeleo katika njia za uzalishaji. Haya ndio masharti ya IMF na WB, yaliyojumlishwa katika mfumo wa uchumi wa Soko huria au utandawazi, ambapo njia zote zinazoweza kuinua viwango vya maisha ya wakulima na wazalishaji wa watu wa nchi yetu zinapigwa mweleka na haya majinamizi. (Tathmini ya Gavana inaeleza kuwa mauzo ya bidhaa zetu kwa nje ni kidogo ukilinganisha na mahitaji yetu, lakini haelezi kwa nini. Hii ndio sababu kubwa).

Matokeo ya hizi ghiliba za IMF na WB, bidhaa zinazoingia nchini kwetu kutoka nje zinauzwa kwa bei ndogo kwa sababu mbili, mosi, njia za uzalishaji katika nchi zenye nguvu za kiuchumi ni za kisasa, kwa maana ya kutumia mashine, wakati sisi tunatumia majembe ya mpini. Pili, Uzalishaji wa bidhaa zao unapata msaada wa fedha kutoka katika serikali zao kwa lengo la kupunguza makali ya uzalishaji. Kitu wanachotukataza sisi tusifanye kwa wakulima na wazalishaji wetu. (Tathmini ya gavana inawatoa kafara wananchi kwamba hawapendi bidhaa zinazozalishwa ndani. Huo ni uongo wa mchana. Tatizo haliko kwenye mapenzi, bali ni liko katika umasikini wa mawazo wa viongozi wetu kukubali masharti ya soko huria na utandawazi. Kamwe tatizo la mfumuko wa bei haliwezi kutatuliwa kimapenzi, bali ama kubadili sera au kuwang’oa wote wanaotubebesha huu msalaba. Ikibidi, yatupasa kuanza upya na mawazo mapya).

Nasisitiza kuwa sikubaliani na nia ya mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani, ingawa kwa nje wanaonekana kuazima sera za utu za kutufutia madeni. Haya mataifa hayawezi kumpinga shetani upande mmoja kwa kutufutia madeni, alafu wakahalalisha shetani upande wa mwingine kwa kukataa kuondoa mifumo ya uchumi duniani isiyo ya haki. Tumefutiwa madeni, lakini mifumo iliyo ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu ambayo ilituingiza kwenye madeni, bado iko palepale. Tunachokifanya ni kuzunguka duara, na mwishowe tunarudi palepale.

Ndio maana baada ya kifo cha Sokoine na Nyerere, uchumi wa nchi yetu unaendeshwa na mataifa ya nje kwa kutumia mitambo ya ukopeshaji inayoendeshwa na mashirika ya fedha ya kimataifa IMF na WB, hivyo kuondoa dhana nzima ya matumaini na ndoto za kujitegemea.

Bahati mbaya wabunge wetu nao ndivyo hivyo kama tunavyojua. Hawawezi kumwambia Gavana wetu kuwa takwimu ulizozitoa ni za kweli, lakini sababu na suluhisho ni vya uongo. (fungua attachement)

Bajeti ya 2007 inaonyesha itilafu ambazo tumezijadili hapa Jambo Forums kwa undani zaidi, na hata tukapendekeza njia za kuondoa hiyo itilafu. Bado nasisitiza kuwa, nia ya WB na IMF ni kutuwekea masharti ya kututia umasikini ili tuendelee kukopa mpaka siku ya kiama chetu. Hivyo basi, kinachotutia umasikini, sio riba itokanayo na hiyo mikopo, bali ni masharti yanayoambatana na mikopo tunayopewa.

Ile “prescription” ya WB na IMF ya kutulazimisha kushusha thamani ya Shilingi kwa kisingizio kuwa, hilo zoezi litakatisha tamaa manunuzi ya bidhaa kutoka nje ya nchi (import), na badala yake, litaongeza mauzo ya bidhaa zinazouzwa nje (export), ni ya hatari na inabidi tuihepuke.

Sababu za msingi za kuikataa hiyo “dose” tulizitoa humu ndani ya JF tena katika mjadala huu. Tulisema kuwa: “viwango vya uzalishaji katika jamii zetu ni vya chini sana. Tunategemea malighafi kutoka nje ili tuweze kuzalisha. Mfano wa bidhaa za lazima zitokazo nje ni Mafuta, Vitabu, Madawa, na Mbolea. Bidhaa zote hizi zinanunuliwa kwa fedha za kigeni. Thamani ya fedha ya nchi yetu inaposhuka na fedha za kigeni kupanda, gharama za uzalishaji zinakuwa juu na kusababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi”.

Lakini takwimu kutoka katika bajeti ya Serikali, kama zilivyofanyiwa uchambuzi na taasisi ya Price Water House Coopers (pdf file attached) zinaonyesha kuwa: (page 10 of the pdf file) "Exports increased by 6.4% from US $ 2,945.5 million in 2005 to US $ 3,135.6 million in 2006”. ‘The value of imports increased by 28.9% from US $ 2,997.6 million in 2005, to US $ 3,864.4 million in 2006. This wa mainly due to an increase in fuel prices and raw materials needed for manufacturing”.

Hizi takwimu kutoka katika bajeti ya Serikali ya 2007 zina maana gani kwetu? Kadili tunavyokubali masharti ya WB na IMF, ndivyo shilingi yetu inavyozidi kushuka thamani. Kwasababu tunahitaji mafuta na "raw materials” kutoka nje, bidhaa zinazozalishwa ndani zinapanda bei na hazinunuliki. Hii ina maana kuwa, kwa makusudi ya WB na IMF, tunakatisha tamaa uzalishaji ndani ya nchi yetu.

Uzalishaji wa ndani ukianza kuchechemea, Serikali inakosa fedha. Inalazimika kwenda kukopa kwa mataifa makubwa au WB na IMF. Serikali inawekewa masharti kuwa ile fedha ya mkopo au ‘msaada” wanayopewa, haiwezi kutumika kurekebisha itilafu ya ndani kwa kusaidia kupunguza makali ya uzalishaji. Lakini wanaambiwa kuwa, wanaweza kutumia hizo fedha kununua ‘raw materials’ au mahitaji mengine ya lazima kutoka nje.

Kumbuka Gavana amewaambia wabunge kuwa Serikali inatumia fedha za "wafadhili” kununua mahitaji nje ya nchi. Lakini hakuwaambia wabunge kwa nini Serikali inafanya hivyo. Jibu ni kuwa wanalazimishwa na WB na IMF. Hapa kuna mantiki gani? Uzalishaji ndani ya nchi yetu unapokufa kifo kitulivu, Serikali inakosa fedha za kigeni, kwasababu hatuuzi bidhaa za kutosha nje ya nchi.

Je, bidhaa zinazozalishwa ndani zikiwa ghali, wananchi watakidhi vipi mahitaji yao ya kawaida bila kupanga foleni na kula unga wa njano? Tulishawekewa masharti ya kufungua milango kwa makampuni ya nje kuingiza nchini kwetu bidhaa zinazouzwa kwa bei rahisi. Je, Serikali itapata wapi fedha za kigeni kama hatuuzi bidhaa za kutosha nje ya nchi? Inabidi ikaemehe (ombaomba) nje ya nchi kama anavyosema Lowasa. Ikakope kutoka mataifa yenye fedha au Majangiri wa WB na IMF.

Je hii ina madhara gani kwa taifa letu? Katika kitanzi hiki, hakuna njia yoyote ya maana kwa Serikali kupata fedha kutosha za kigeni kwa ajili ya kununulia mahitaji muhimu kama mafuta. Njia moja tu ni kuomba nje na kukopa. Kitanzi cha pili ni kuwa, kwasababu uzalishaji nchini kwetu unapigwa kabari na kushindwa kupumua, tunategemea bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.

Kwa maana hiyo basi, nchi yetu inaandaliwa kuwa soko la bidhaa zinazozalishwa nje. Haiandaliwi kuzalisha bidhaa kwa ajili ya masoko ya nje. Serikali ikihitaji fedha za kigeni, inabidi ikakope nje. Hii hali inachukuwa sura ya mviringo kwa maana ya kujirudia rudia mpaka tutakapo anguka chini kama Zaire. Hili ndilo lengo la WB na IMF.

Ndio maana tuliandika huko nyuma katika huu mjadala kuwa "uchumi wa nchi yetu unaendeshwa na mataifa ya nje kwa kutumia mitambo ya ukopeshaji ya mashirika ya fedha ya kimataifa WB na IMF. Kuendelea kukubaliana na haya mashirika ni kuondoa dhana nzima ya matumaini na ndoto za kujitegemea”.

Kilimo

Viongozi wetu wanatulaghai, tena kwa kejeli kuwa hizi ni zama za Soko Huria, Utandawazi, Ujasirimali, na ujinga mwingine. Wamepiga teke ukweli wa kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa letu. Lazima viongozi wetu watambue kuwa, bila wakulima, wasingeendesha hayo mashangingi. Bila wakulima, wasingevaa tai. Bila wakulima wa vijijini, barabara za rami za mjini zisingejengwa. Kwa kifupi, mpaka sasa hivi, wakulima wa vijijini ndio wanatuweka mjini.

Takwimu kutoka katika bajeti ya Serikali 2007 (page 10 of the pdf file) zinaonyesha kuwa, mwaka 2006, sekta ya kilimo imekwisha changia pato la taifa (GDP) kwa asilimia 44.7. Hii ina maana kuwa, kilimo bado ni uti wa mgongo wa taifa letu. Sera za WB na IMF zenye lengo la kuwaumiza wakulima wetu, inabidi zipigwe vita kwa nguvu zetu zote. Tukiumiza sekta ya kilimo, tunakuwa tumeumiza nchi. Sekta nyingine zote ni za ubabaishaji.

Mfano, pamoja na kwamba Tanzania ni nchi ya tatu kwa kutoa dhahabu katika Afrika, lakini mpaka sasa hivi, sekta ya madini imechangia pato la taifa kwa asilimia 3.8. Sekta ya Nishati imechangia asilimia 1.4, sekta ya Viwanda asilimia 9.2, sekta ya Mawasiliano na uchukuzi asilimia 5.4, na sekta ya Ujenzi asilimia 5.4. Takwimu hizi zinatufundisha kuwa, tunaweza kusimamisha uchimbaji wa madini kwa kufukuza makampuni yote ya nje, na uchumi wetu ukabaki ulivyo. Lakini hatuwezi kufunga sekta ya kilimo, alafu tukabaki salama.

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa, hakuna sekta nyingine yoyote yenye ubavu wa kulipa madeni ambayo Serikali inakopa. Ni sekta ya kilimo peke yake. Wakulima wa vijijini ndio wanalipia gharama za mafuta ya kuendesha umeme tunaotumia mjini. Gharama za mafuta ya kuweka kwenye Mashangingi ya Viongozi na Wabunge. Gharama za kulipia viyoyozi maofisini kwa waheshimiwa na ndani ya magari yao.

Tumeuza benki ya wananchi NBC ambayo ilikuwa inafungua matawi vijijini, tukaleta benki za kibeberu zinazoishia mijini. Wakulima hawawezi kupata tena mikopo yenye ahueni ili kupunguza makali ya uzalishaji. WB na IMF wanaiwekea Serikali yetu masharti ili isiwasaidie fedha (subsdize) wakulima wetu. Mfano, bajeti ya Serikali 2007 (page 9 of the pdf file) imetenga asilimia 6.2 kwa ajili ya sekta ya kilimo. Inakuwa je sekta ya kilimo inachangia pato la taifa kwa asilimia 44.7, lakini inatengewa asilimia 6.2?

Karibia nusu ya fedha ya bajeti ya Serikali 2007, yaani Shilingi bilioni 2,549 zitapatikana kwa mikopo na zawadi. Lakini zaidi ya nusu ya fedha ya bajeti ya Serikali 2007, yaani Shilingi bilioni 3,866 ni kwa ajili ya matumizi tu na sio mipango ya maendeleo. Mchanganuo huu kutoka katika bajeti ya Serikali unatukumbusha kuwa, kwa kila Shilingi 100 anayotumia Rais wetu kwenda nje kukopa fedha, shilingi 63.7 ni za mkopo. Hivyo, tunakopa nauli ya Rais wetu ili aende kukopa. (tunakopa ili tukope-circle)

Kati ya mashirika ambayo yamekwisha tukopesha fedha kwa ajili ya hii bajeti ya Serikali, mojawapo ni WB. Lakini haohao WB wanatushauri tutenge asilimia chache kwenye sekta ya kilimo (6.2). Hata hivyo, tumeona kuwa sekta ya kilimo kinachangia pato la taifa kwa asilimia 44.7. Hata kwa mtu mjinga kabisa, baada ya kuangalia michango kutoka katika sekta nyingine, atawekeza asilimia kubwa ya bajeti yake kwenye kilimo ili mchango wa hiyo sekta uongezeke. Je fedha ya kuwalipa hao WB itatoka wapi?

Let me be clear: corrective actions are needed to eliminate our country’s indebtedness, restore national ownership, control of productive assets, and balance exports and imports. A key step would be to close the World Bank, IMF, and restore the right of economic self-determination to our people and in deed, to our government. Responsibilities for economic management should be transferred to the people of Tanzania.

........Mkuu Kyoma uko wapi ndugu?....heri ya mwaka Mpya.....

Salute
 
Mwanakijiji na wengine,

Mnaonaje tukimuenzi Marehemu Sokoine mwaka huu kwa vitendo kama JF?
Yeah, hata sisi tulio machimboni tutarudi mjini. Huyu bwana ingawa nilikuwa kijana mdogo sana wakati akifariki, namkumbuka kama shujaa wa kweli na mtu aliyekuwa anaijua dawa ya matatizo ya uongozi Tanzania.

Kama tungeliendelea kupambana na shida zile, tungezalisha wafanyakazi makini na wagunduzi wa kweli kwa maelfu. Alipokufa waliomfuatia ndo hao ruksa mpaka na ufisadi hadi ukatinga Ikulu.
 
Kwa kumkosa huyu mpambanaji wa rushwa , magendo na wizi wa fedha za uma tumeona mengi. Machache tuliyoshuhudia ni epa, kagoda, tics, kiwira na buzwagi. Shujaa huyu asingekubali ushenzi huu.

Amekosekana aliye vaaa viatu vyake. Hongezeni mapungufu mengine.mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.
 
Huyu mzee alijkitahidi kweli but mdogo wake dah. Namaanisha yule morani mwingine!
 
Lakini morani mwingine pamoja na mapungufu yake alikua mchapa kazi, alitolewa kafara on behalf of vigogoz, cause kama kwey tuhuma za ufisadi zingekua kwa kiwango hicho wakisemacho why hajafikishwa kisutu au wanaogopa maumbuo maana Deep Green, Kagoda na Maremeta sio morani wahusika tunawajua lkn mhhh walijisemea ndugu zangu kina Soda Nitakutapika " Kumkoma nyani Giladi" tumebaki kumuhukumu morani na Richmond.

Mhhh I think its diversion of attention tu tusahau Kagoda, Deep Green, Maremete, Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu Vingunguti aka Mwananchi Gold Ref...... na mengi tu ya mashenzini. anyways ...............
 
Tunamuenzi vipi marehemu Edward Sokoine?

ANAYESTAHILI pongezi hana budi kupongezwa. Wengi wetu tunapenda sana kufanya kumbukumbu ya mambo yanayofurahisha, lakini mambo ambayo yanasuta dhamiri zetu huwa si ya kukumbukwa sana, maana mambo hayo hutukosesha raha.

Mojawapo ya mambo ambayo yanakosesha raha, viongozi wa Tanzania wa leo kuyakumbuka, ni kuhusu kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania wakati wa utawala wa awamu ya kwanza, Edward Moringe Sokoine, na ndio maana hata kumbukumbu yake haipewi mkazo na viongozi wa chama tawala na serikali yetu.

Je ni kweli kwamba Edward Moringe Sokoine si wa thamani sana kiasi cha kubezwa kukumbukwa kwa heshima na chama au na serikali ya chama chake enzi za uhai wake?

Edward Moringe Sokoine alizaliwa mwaka 1938 na kuaga dunia Aprili 12, 1984. Alikuwa Waziri Mkuu mara mbili, Februari 13, 1977 hadi Novemba 7, 1980, na tena Februari 24, 1983 hadi kifo chake kilichosababishwa na ajali ya gari eneo la Dakawa mkoani Morogoro akitokea bungeni Dodoma. [/SIZE]
Uongozi wa Sokoine ulionekana kuwa wa mfano kwa uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma. Huenda hii ikawa ni mojawapo ya sababu kubwa ya uongozi wa nchi yetu kususia kumfanyia kumbukumbu ya heshima, kwani uadilifu aliokuwa nao Sokoine haupo hata chembe katika CCM na serikali yetu ya sasa.

Sokoine alikuwa ni mpenzi wa wananchi wote; alikuwa mzalendo mwaminifu, mwenye vitendo vingi, lakini pia maneno machache.

Je, hali halisi katika uongozi wa serikali yetu ikoje? Maneno mengi, lakini vitendo kidogo au hakuna kabisa.

Watanzania wa sasa wamekuwa wakiahidiwa vitu vingi na serikali yao; vitu ambavyo haviwezekani hata kwa wenye imani ya kuhamisha milima, je, uadilifu uko wapi?

Sokoine aliendesha yeye mwenyewe Operesheni Wahujumu Uchumi, mafisadi walitupa barabarani pesa walizokuwa wamezikwapua kwa njia haramu ili kujisalimisha.

Vipi vigogo wetu wa sasa walivyo na uswahiba na wahujumu uchumi. Viongozi wetu wa sasa, akiwemo rais, mawaziri na makatibu wakuu na wakuu wa mikoa na wilaya; wanahusudu zaidi urafiki na wahujumu uchumi, wanaowahujumu Watanzania huku walalahoi wakiendelea kusota katika njaa na lindi la umaskini.

Unategemea wahusudu mafisadi hawa wanaweza kukumbuka kuandaa kwa heshima kumbukumbu ya mzalendo huyu ambaye matendo yake yanachefua hawa waliopo sasa?

Viongozi wetu wa sasa ndio marafiki wakubwa wa mafisadi, Sokoine alitafsiri kauli zake kwa vitendo na bila woga.

Enzi za Sokoine, kama kulikuwa na viongozi wala rushwa na mafisadi, basi Sokoine alikuwa chanzo cha hofu kubwa ya wala rushwa na mafisadi hao; alikuwa akifanya ziara za ghafla sehemu za kazi na kisha akapata maelezo na ushahidi wa ufisadi wa viongozi husika. Hicho ni sawa na kiyama.

Viongozi wetu wa sasa wanakaa na Mafisadi, wanakula nao, na kufanya mikutano pamoja kupanga namna ya kuwahujumu Watanzania, hata wale wanaotuhumiwa waziwazi, wanateteana. Turejee kauli ya Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, aliposema mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi ahukumiwe kwa kazi alizofanya na si majungu ya bungeni.

Enzi za Sokoine yeye mwenyewe alisimama kidete kupambana na wahujumu uchumi ambao baadhi walilazimika kukimbia nchi na wengine kutelekeza biashara zao.

Je, viongozi mafisadi waliopo sasa wanaweza kweli kumkumbuka mtu ambaye alikuwa tishio kwa maisha yao?

Sokoine alionekana kama tishio la majambazi, lakini wakati huu wa utawala hasa wa awamu ya nne, majambazi na vibaka wanapapasa hadi Ikulu. Kibaka aliingia Ikulu akaiba maua, majambazi yakavunja hata ofisi ya Rais mstaafu Benjamini William Mkapa wakaiba kompyuta; kama majambazi yanapapasa hadi sehemu nyeti kama hizo, sijui huku mitaani walalahoi tunalindwa na nani? Huenda ndio maana wananchi wanazidi kujichukulia sheria mikononi.

Sokoine alikuwa mfano wa kuigwa. Alishi kama alivyohubiri. Siyo tu hakujilimbikizia mali, bali alipunguza hata mali zake ili apate nafasi zaidi ya kututumikia Watanzania.

Jamii ya viongozi tulionao sasa, ambao hata kutaja mali zao wanaogopa, watu wasiotumia muda mwingi kukaa ofisini, watu wanaotumia muda mwingi kukaa katika biashara na starehe zao, wanaweza kuwa na lipi la kuigwa?

Wanaweza kukumbuka kweli kumuiga Sokoine? Na watamuiga kwa lipi? Watafanya hivyo hadharani au sirini ili wasisutwe na Watanzania maskini ambao hawategemei hata chembe ya huruma kutoka viongozi hao?

Pamoja na kiwango cha maendeleo kilichokuwepo wakati huo, Sokoine na Nyerere hawakuwachangisha Watanzania katika suala la elimu; madawati yalitosha na waalimu walienda shuleni kufundisha. Kwa sasa ni tofauti, madawati hayatoshi, madarasa hayatoshi, na walimu wanatangaza waziwazi kuwa wamechoshwa na ufisadi wa serikali isiyowajali, hivyo wataendelea kufundisha wanavyojisikia.

Bahati mbaya walimu wamezira kuwafundisha watoto wa maskini, na watoto wa vigogo hawapo nchini katika shule za kata, ndio maana hata tishio la walimu haliwagusi vigogo.

Sokoine aliutambua ukweli, kuwa katika nchi yetu, mahitaji ya wachache wenye nacho ni makubwa mno na kamwe hawaridhiki na walichonacho na wapatacho, lakini la msingi wanalohitaji wanyonge wa nchi hii ni moja tu: kutokandamizwa.

Lakini ukandamizaji uliopo katika nchi yetu kwa sasa ni mkubwa, watu wamefukuzwa katika nyumba zao kwa sababu ya kulazimishwa kuchangia michango ya sekondari hata kama hawana, kina mama wamejifungulia katika ofisi za watendaji kwa kukosa michango, wanaotaka kuandamana wanatishwa na wasipotishika huambulia kipigo, je ndani ya jamii hii iliyochafuka vile tungeweza kumkumbuka mtu msafi?

Enzi za Sokoine, wananchi waliwapenda viongozi wao, walijipanga barabarani kuwaimbia viongozi wao, kwa kuwasifu walipowafukuza wahujumu uchumi, walivyokosa uswahiba na wafanyabiashara, tofauti na sasa, hata msafara wa rais unapigwa mawe, mabango kibao kila anapokuwa na ziara katika nchi!

Wananchi wanalalamika kila siku, ufisadi, ujambazi, wizi, maadili ya kazi hakuna, lakini rais aliyepo na chama chake wameendelea kuwaingiza wananchi mjini, kwa kuwaahidia maisha bora kwa kila Mtanzania, ambayo labda yanapatikana katika Tanzania ambayo sio hii tunayoiona.

Je, tunamuenzi Sokoine, au tuache kabisa kuliko kuchafua jina safi kwa sifa za kijinga!? Tutafakari. [Kifo cha Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtegemea Sokoine kuwatetea wanyonge na kuinua kiwango chao cha maisha.

Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha. Pamoja na maadili mazuri aliyoonyesha, viongozi waliomfuata katika uongozi hata jimbo alilotoka wamekuwa wakituhumiwa sana kwa Ufisadi.

Kuna kila sababu ya Watanzania kutofanyiwa kumbukumbu ya heshima ya aliyekuwa waziri wao mkuu, waziri msafi, aliyechukia ufisadi, kuliko kufanyiwa kumbukumbu ya mtu msafi na mafisadi.
 
presdaa anataka kujifanya baba wa taifa kila anaetofautiana nae anajidai kumfungia mwaka huu inakula kwake ngoja uchaguzi ufike utjua alikuwa kimya au alikuwa kazini, na babu seya lazima atoke korokoroni.
 
Duh! kwa hakika umenikumbusha hii figure, sijui iko wapi! Jamaa kaamua kuwa kimya kwelikweli!
 
ni moja ya wanaCCM wanaofahamu vema siasa za nchi..ndio maana hawezi kuongea kwa sasa..
 
mwacheni, JK na Makamba wanajifanya majinias sana.
 
''mimi mangula,nipo lupembe hapa BARAZANI!nasimamia mashamba yangu ya chai...''
karibuni lupembe vijana
 
Mangula kashindwa siasa za fitna na rushwa za CCM kaamua kulima.

Kama kumbukumbu zangu ni nzuri Mangula aligombea uenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa akashindwa,bila shaka mtandao ulihakikisha hapenyi.

Lakini nakumbuka baada ya kushindwa alilalamika uchaguzi kugubikwa na rushwa kitu ambacho yeye alidai hawezi kukifanya. Alisema siku hizi wapiga kura hawataki vipeperushi, wanataka vipeperushwa.
 
Inasemekana Mangula katka uchaguzi wa 2005, alikuwa kambi ya Sumaye, hakuwa ana mfagilia Kikwete aingie madarakani. hivyo kikwete alivyo win akaamua kumpoteza kisiasa.
 
Nimejifunza mambo mengi juu mzee jumbe ningependa kujua tena kuhusu sokoine.mara uliuliwa lakin inasemekana ni mwanamapinduzi wa ukweli kwa nin aliuliwa? Alikuwa anapinga ufisadi wa enzi hizo
 
Back
Top Bottom