Tunamshauri arudiane na mkewe: Waliachana baada ya mume kuzaa nje ya ndoa

Tunamshauri arudiane na mkewe: Waliachana baada ya mume kuzaa nje ya ndoa

Kiuhalisia hawezi kumdharau mke wake kiasi kile.
Watu wengi sana(wanaume na hata wanawake) wana watoto nje ya ndoa.
Lakini wanatunza siri isijulikane hadi wamekuwa watu wazima.
Hii kumuonyesha mke wako kuwa wewe ni kijgoo na umezaa nje, na huna la kujutia, hilo linamweka kaka yako katika mtego alioingia mwenyewe.
Mwanamke kurudi kwake atafanyiwa hivyo hivyo tena.
Kaka yako ana makamasi ndani ya fuvu badala ya ubongo.
 
Ubabe kama ubabe matokeo yake kakosa Mke na Mtoto, endeleeni kumshauri kama wanafamilia halafu itapendeza kama utaleta mrejesho hapa.
 
Heshima ni kitu muhimu saaaana huyu Brother Hana adabu na kakipata kapoteza vitu vya maana ktk maisha yake.

Alikuwa gizani katupa Almasi akaokota mawe shauri ya kiburi
 
aisee mimi mtu akishanisaliti kila atakachokua anaongea naona ananichora tu,,yani sijui aniambie nini nimwelewe 🤨🤨
Mimi nikihisi mwanamke ana kinyongo na mimi siwezi kulala naye chumbani, kula chakula chake n.k kwa kifupi huyo hanioni tena. Sijui labda niko na misamiati michache ya faragha.
 
Itungwe sheria kali ya kuthibiti wanawake matapeli wanaobambika wanaume watoto, mtu anajibu atarudisha gharama za kulea, je hasara ya kumvunjia ndoa!! Hii ni PATERNITY FRAUD, ndiyo maana mauaji ya kinachodaiwa WIVU WA MAPENZI hayatopungua hadi Yesu arudi, makahaba wamezidi ushenzi.
 
Huyo mke labda awe mtu wa njaa njaa asiye na courage ya kuamini kujitafutia riziki mwenyewe kwa jasho lake ndipo atakubali kurejea lakini kama si mtu wa njaa na anaweza kujitafutia riziki halali kwa jasho lake kamwe hawezi kurejea nyuma [emoji108]
 
Kuna wengine nawajua wameuziwa watoto si wao,

Mmoja amekuwa akipata changamoto ya uzazi mkewe mara Kwa mara mimba kuharibiwa N.k.

Sasa mwanakwaya mwenzio na mume aka-take advantage akamtega mume wa mtu wanaeimba naye kwaya na huku akijua anahitaji mtoto,

Akategesha mimba haishiki , akapata Mwalimu malaya mstaafu akamwambia zaa Mwanaume mwingine lofa yeyote halafu mtoto muuzie jamaa Fanya kumbambikia kuwa ni wake ili ule hela zake maana huyo mume ako anafanya kwenye taasisi inayochukuliwa kuwa na hela kwenye jamii.

Basi mke akajua akaondoka huu Mwaka sijui wa ngapi,

Jamaa mtoto si wake anaibiwa hela ya malezi ya Mtoto tangu mimba hadi leo,

Mwanamke mwenyewe mchawi inasemekana yaani ilimradi ni shida.

Nasikia mke huko aliko ana mimba.
 
Huyo mke labda awe mtu wa njaa njaa asiye na courage ya kuamini kujitafutia riziki mwenyewe kwa jasho lake ndipo atakubali kurejea lakini kama si mtu wa njaa na anaweza kujitafutia riziki halali kwa jasho lake kamwe hawezi kurejea nyuma [emoji108]
Anaendesha V8 sasahivi. Amejenga mbweni na anaduka kubwa la vinywaji, na anakwenda China kuchukua bidhaa sometimes anaenda na watoto wake yupo fresh kinoma.
 
Alishachezea shilingi chooni. Ishaisha hiyo.
 
Back
Top Bottom