Tunamuomba Serikali yetu isiyumbishwe na kelele za watumishi

Tunamuomba Serikali yetu isiyumbishwe na kelele za watumishi

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Tunamuomba Mhe. Rais asiyumbishwe na kelele za baadhi ya wanao jiita watumishi wa umma juu ya nyongeza ya mshahara wanayo sema ni ndogo.

1. Uchunguzi unabaini kuwa baadhi ya watumishi wanatumiwa na baadhi ya wanasiasa kudhihaki na kukejeli nyongeza iliyo tolewa.

2. Wanasiasa wenye uchu wamelishikia bango hoja hili kama kete/fimbo ya kisiasa........hao ni wanasiasa uchwara.

3. Kundi la wenye chuki binafsi limo humo.

4.

Naishauri Serikali yangu kamwe isiyumbishwe na makelele haya, anayetaka nyongeza afanye kazi asiyetaka aache aende akalime.

Chonchonde serikali isiwadekeze hawa watu ni hatari naomba style ya Magufuli itumike ktk jambo hili, hakuna kubembelezana, kama kuna mtumishi ambaye haja ridhika aache kazi, vinginevyo.

Uchumi wa nchi bado haujaimarika ni jambo la kushangaza kudai nyongeza kubwa!!! huu ni upuuzi na unafaa kupuuza, narudia tena anaye taka afanye kazi la acha nenda kalime.

Kama kuna mtumishi anaye ona hiyo nyongeza haimtoshi ana uhuru wa kuacha kazi na kutafuta kazi kwengine maana Utumishi wa umma ni Wito.

Kimsingi katika kipindi hiki chenye changamoto lukuki za kiuchumi haikutakiwa kabisa kuwaongeza hiyo nyongeza ambayo baadhi ya wanao jiita watumishi wanadai ni "kidogo".

Lakini huruma ya Mama akaona bora hiyo hiyo kidogo kuliko kukosa kabisa, angeweza kukomaa hadi miaka 5 iishe lkn kwa huruma yake akaona hapana, bora hata hicho kidogo kuliko kukosa kabisa, sasa shukurani zenu ni lawama na kejeli? Kama kweli asiye shukuru kidogo hata kikubwa hawezi!!!

Watumishi mnaharibu sana! mtqmlazimisha mama akose huruma kabisaaa!!

Awamu hii ya 6 ndani ya muda wa mwaka mmoja tu kawafanyia watumishi mambo mengi kabla ya nyongeza hiyo;

1. Bima ya afya sasa watoto wenu wataweza kutumia hadi miaka 22.

2. Watumishi wengi kwa mkupuo wamepandishwa madaraja sambamba na ongezeko la mishara yao, jambo hilo halijawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru.

3. Ajira lukuki zimemwagwa kila idara za Serikali, haijawahi kutokea tuache tabia ya kuziriba mambo mazuri yanayo fanywa na viongozi wetu.

Tuache tabia ya KUZIRIBA mambo mazuri yanayo fanywa na Rais wetu Mama Samia,
 
Tumia akili kutoa maoni Yako, usiwaze tumbo lako tu
shida iko wapi, kama unaona nyongeza haitoshi acha kazi nenda katafute kazi itakayo kutosheleza.

Nchi yetu bado uchumi wake mdogo, changamoto kibao leo unataka ujaziwe halafu!

huo ndio uwezo wa Serikali haiwezekani kuzidisha hutaki nenda kalime.
 
Kumbe shida ni kutaka watumishi waache kazi ili machawa muajiriwe? CCM mnafeli Sana katika hili la kucheza na stahiki za watumishi ili wakasirike waache kazi kupisha nafasi mkazijaze Kwa kuwaajiri watoto wenu ili wakaendeleze ufisadi wa wazazi wao!

Nimekudharau mno! Kazi haiachwi na mshahara mtaongeza TU mtake msitake!
 
Ukifuatilia kwenye historia hata za ulaya mabadiliko mengi kuanzia ya kisiasa yalisababishwa wafanyakazi either kutokana na maslahi duni au mambo mengine.kuwa Makini na wafanyakazi.
 
9e51e1cd812a52d0d840ee20145f7e93.jpg
 
Kama ni teuzi unakaribia kuukwaa !!! Hongera !!
 
Kaka wewe ndiyo baba wa familia na huu ndiyo uwezo wako wa kufikiri, Hii familia neema ya bwana iwafunike na mke ajaaliwe maarifa kulea watoto, maana baba yao.............
 
Kimsingi kuna chuki kubwa sana dhidi ya waajiriwa wa serikali hasa kutoka kwa wale ambao familia Yao haikubahatika kutoa hata mtumishi mmoja serikalini.
 
Back
Top Bottom