Tunangojea mbio za mwenge kubaini Sh. 63bil zimeibwa?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Waliogundua kuwa 63 bil zimeibwa kwenye miradi angeweza kugundua hivyo mapema hata bila mbio za mwenge.

Kuna ushahidi uliothibitika kuwa mbio za mwenge ni uchochoro Mpana unaopitisha:
1. Ulaji wa fedha za umma
2. Maambukizi ya HIV na magonjwa ya ngono
3. Kipimdupindu na typhoid kutokana na watu kukusanyika wengi mahali kwenye uhaba wa vyoo na maji ya kutosha.
4. Covid-19 na TB kutokana na msongamano
5. Mimba za utotoni na mimba zisizotarajiwa.
6. Kuvunjika kwa ndoa na mahusiano kutokana na fumanizi na kukesha nje ya familia.
7. Ajali za barabarani, kujeruhiana na hata kuuana.

Hivi inakuwaje hakuna watu waliozuia au kugundua upotevu wa hela hizi kabla hasara haijafikia hizo 60s bil?

Binafsi napata shida sana kuona mwanasiasa anahimiza wananchi kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza kama covid-19 wakati amewakusanya watu weeeengi sehemu moja ambao wameshinda na wamekesha mahali hapo. Ndio maana wananchi wanachanganya na akili zao kuhusu chanjo ya covid-19.

Hii ya mwenge kipindi hiki Cha covid-19 ni ushahidi kuwa viongozi wetu wanataka uongozi sio watu.
 
Mwenge ni masharti ya mganga hamna lolote la maana , upo Kwa ajili ya kuhamasisha uzinzi na uasherati , Askari wengi wametolewa kafara kwenye hzo mbio hewa za mwenge ...
 
Mwenge ni kitu kilichoanzisha kitambi hiko kuonesha kwamba serikali ipo hasa maeneo ya vijijini huko. Dunia ya sasa imebadirika teknolojia imekua mwenge tubadirishe namna ya kuikimbiza
 
Mwenge ni kipimo cha juu kabisa kinachowatambulisha mbogamboga ,kiwango cha ujinga ,uchawi, umbumbu walionao
 
Waliogundua kuwa 63 bil zimeibwa kwenye miradi angeweza kugundua hivyo mapema hata bila mbio za mwenge.

Kuna ushahidi uliothibitika kuwa mbio za mwenge ni uchochoro Mpana unaopitisha:
1. Ulaji wa fedha za umma
2. Maambukizi ya HIV na magonjwa ya ngono
3. Kipimdupindu na typhoid kutokana na watu kukusanyika wengi mahali kwenye uhaba wa vyoo na maji ya kutosha.
4. Covid-19 na TB kutokana na msongamano
5. Mimba za utotoni na mimba zisizotarajiwa.
6. Kuvunjika kwa ndoa na mahusiano kutokana na fumanizi na kukesha nje ya familia.

Hivi inakuwaje hakuna watu waliozuia au kugundua upotevu wa hela hizi kabla hasara haijafikia hizo 60s bil?

Binafsi napata shida sana kuona mwanasiasa anahimiza wananchi kuhusu kujikinga na magonjwa ya kuambukiza kama covid-19 wakati amewakusanya watu weeeengi sehemu moja ambao wameshinda na wamekesha mahali hapo. Ndio maana wananchi wanachanganya na akili zao kuhusu chanjo ya covid-19.

Hii ya mwenge kipindi hiki Cha covid-19 ni ushahidi kuwa viongozi wetu wanataka uongozi sio watu.

Kwani zile 19bn/- za ofisi ya yule kigogo zimo humo?
 
Mwenge ulikua ni wa kuwekwa makumbusho tu watakaohitaji waende kuuona sio kuvuruga ratiba na shughuli za kiuchumi na kelele na mikusanyiko isiyo na maana
 
Unasikia kiongozi wa mwenge amekataa kufungua mradi kwasababu hajaridhirika kuhusu viwango au matumizi ya fedha.

Swali ina maana bila mwenge viwango na hata matumizi ya fedha visinge julikana? Na hakuna mfumo wa ukaguzi na udhibiti?

Au unasikia kiongozi fulani kakataa kufungua barabara na kuagiza mkandarasi kurudia kazi au kusitishwa kazi. Je, hakuna mfumo wa udhibiti hadi mkubwa sana atembelee miradi?

Naona kama maigizo vile!
 
Wanzania zindukeni kuhangaikia usanii wa aina hii kwa wananchi. Huku ni kutafuta sifa za majukwaani ili muone kuwa watu wako serious. Lakina kwenye kila mradi kuna BOQ, mdhibiti ubora na watu wa monitoring and Evaluation. Itawezekana vipi hadi mradi uishe bila kujulikana ubora na thamani yake halisi? mbona wasimamizi wote hawa hawafukuzwi kazi na kurudisha pesa walizoiba?
 
Unasikia kiongozi wa mwenge amekataa kufungua mradi kwasababu hajaridhirika kuhusu viwango au matumizi ya fedha.

Swali ina maana bila mwenge viwango na hata matumizi ya fedha visinge julikana? Na hakuna mfumo wa ukaguzi na udhibiti?

Au unasikia kiongozi fulani kakataa kufungua barabara na kuagiza mkandarasi kurudia kazi au kusitishwa kazi. Je, hakuna mfumo wa udhibiti hadi mkubwa sana atembelee miradi?

Naona kama maigizo vile!
Haiwezekani mtu mmoja uwe sehemu ya tatizo na sehemu ya suluhisho kwa wakati mmoja, ni usanii. Aliyepaswa kuzuia wizi hakuuzuia kisha ndiye huyohuyo analalamika baada ya wizi kutokea tena analalamika hadharani kwenye mbio za mwenge badala ya kwenda mahakamani kisha ndipo waje kwetu wananchi watujulishe hatua zilizochukuliwa kurudisha pesa na kuwawajibisha wezi wote.

kazi ya kuwapeleka TAKUKURU kuchunguzwa ilitakiwa ichukuliwe administratively sio mbele ya wancnhi waliosongamana walioko kwenye hatari ya kuambukizwa covid, ukimwa nna TB
 
Gharama za kukimbiza Mwenge jumlisha na zilizochotwa ni janga.
Ndiyo maana Mwendazake aliupotezea Mwenge.
 
Kwani mwenge uligharimu sh. ngapi maandalizi yake yote jumla?

Tunafahamu kuwa mwenge kwenda Kanda Ile ni sehemu ya siasa za 2025.
 
Back
Top Bottom