ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Checkers au waweza kuliita draught kwa lugha ya kigeni Ni mchezo ambao unazidi kuwa maarufu Sana katika vijiwe vingi.yaani zamani nilikuwa naona wazee tu wakilicheza katikati ya miji Ila siku hizi vijana mashabiki na wachezaji tumekuwa wengi sana mida ya jioni utatukuta tukiumiza ndonga.mimi nimejifunza zamani kidogo na Nina record kubwa Sana mtaani wote nawafunga na ninatamba Sana wapo watu walikuja kunijaribu tena walikuja na uchwawi kabisa wakidhani sitaziona kete lakini niliwapeleka mbio wakaishia kuambulia draw..sasa nataka Wana jf wanaojifanya wanalijua hili dude niwatembelee popote walipo niwaonyeshe uwezo wangu.nipo tayari kukufuata nikufunge wewe na kocha wako.