Tunaoishi single (Ghetto Geez) Tukutane hapa

Mkuu maji ya kumezea dawa huwa unachota kwenye ndoo ya chooni?
Maana sijaona hapo umetaja budget ya maji
 
Most of the time inadepend na maokoto ya siku iliyopita na iliyopo sisi wengine kipato chetu cha unga mwana leo unaweza kuotea laki afu ukakaa wiki nzima bila mchongo wowote.

Sasa hii ni budget wakati shimo limetema

Asubuhi
  • Supu na chapati mbili 3000
  • Sambusa na yai la kuchemsha 1000
  • Pepsi na Maji Lita moja 1300

Mchana
  • Zege na mishikaki miwili 4000
  • Maji Lita moja na nusu 700

Usiku
Hapa chief cooker nakuwa mwenyewe
- kinapitiwa kidali cha broiler chicken 4000 unga unakuwepo geto linatolewa dongo
-maji lita moja 500

Total 14000 Tz Shillings

Sasa kuna hii budget wakati harakati hazieleweki

Asubuhi inatoka kwenye ratiba nakuja kula mihogo miwili na soda 1100 majira ya saa sita nikitoka hapo natulia mpaka usiku napitia mayai mawili 600 na nyanya moja 200 litapikwa ugali mkubwa wakati wa kula ni kuhakikisha mayai na ugali vinaisha sambamba hapa maji ya kunywa ni ya bomba hichi ndio kipindi mikakati ya fedha kichwaani inakuwa mingi ila pesa ikipatikana nasahau shida zote

Total 1900 Tz Shillings
 
Chai hakuna, lunch hakuna. Nakula jioni ugali wa buku Kwa mama ntilie. Vocha ya bando ni 2100/=. Jumla ni 3100/=. Imeisha hiyo!
 
Vipi kuhusu usafiri?
 
Kuna kipindi nilipigika ndani ulibaki unga na gesi tu kazi ikawa ni kutafuta mboga tu, nikawa nanunua maharage yaliyochemshwa ya tsh 500 natia chumvi nakula na ugali. Kipindi hicho ndio nilijua kujibajeti na kuacha matumizi yasiyo yalazima na ndio kipindi nilifanikiwa kuachana na makamari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…