Most of the time inadepend na maokoto ya siku iliyopita na iliyopo sisi wengine kipato chetu cha unga mwana leo unaweza kuotea laki afu ukakaa wiki nzima bila mchongo wowote.
Sasa hii ni budget wakati shimo limetema
Asubuhi
- Supu na chapati mbili 3000
- Sambusa na yai la kuchemsha 1000
- Pepsi na Maji Lita moja 1300
Mchana
- Zege na mishikaki miwili 4000
- Maji Lita moja na nusu 700
Usiku
Hapa chief cooker nakuwa mwenyewe
- kinapitiwa kidali cha broiler chicken 4000 unga unakuwepo geto linatolewa dongo
-maji lita moja 500
Total 14000 Tz Shillings
Sasa kuna hii budget wakati harakati hazieleweki
Asubuhi inatoka kwenye ratiba nakuja kula mihogo miwili na soda 1100 majira ya saa sita nikitoka hapo natulia mpaka usiku napitia mayai mawili 600 na nyanya moja 200 litapikwa ugali mkubwa wakati wa kula ni kuhakikisha mayai na ugali vinaisha sambamba hapa maji ya kunywa ni ya bomba hichi ndio kipindi mikakati ya fedha kichwaani inakuwa mingi ila pesa ikipatikana nasahau shida zote
Total 1900 Tz Shillings