A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na ongezeko la nauli za mabasi ya mikoani katika miaka ya hivi karibuni, lakini hadi sasa LATRA haijaweka hadharani waraka au PDF mpya ya viwango vya nauli. Hati inayopatikana kwa urahisi ni ile ya mwaka 2023.
Kutokana na hali hiyo, waajiri wengi wanaendelea kutumia viwango vya nauli vya mwaka 2023 katika malipo ya likizo ya mwaka (annual leave), jambo linalosababisha watumishi kupata malipo yasiyoendana na gharama halisi za usafiri zilizopo sasa.
Pindi watumishi wanapohoji tofauti hiyo, hupewa majibu kwamba LATRA haijatoa waraka rasmi unaoonyesha viwango vipya vya nauli za mabasi ya mikoani, hivyo hakuna nyaraka zinazoweza kutumika kuthibitisha mabadiliko hayo.
Tunaiomba LATRA kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili na kuweka wazi viwango vya sasa vya nauli kwa njia rasmi na inayopatikana kwa urahisi. Je, kuna changamoto gani inayozuia kutolewa kwa waraka mpya wa nauli wakati mabadiliko ya bei yamekuwepo kwa muda mrefu?
Hatua hiyo itasaidia kuondoa mkanganyiko uliopo na kuhakikisha watumishi na wananchi kwa ujumla wanapata stahiki zao kwa kuzingatia viwango halisi vya nauli vinavyotumika sasa.