Habari za muda huu.
Tunaomba Serikali na mamlaka husika, hususan Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika kozi ya Bachelor of Science in Nurse Anaesthesia.
Kozi hii imekuwa na mahitaji makubwa, hasa kwa wahitimu wa Diploma ya Nursing wanaotaka kujiendeleza kielimu. Wapo waombaji wengi ambao wanakidhi vigezo vya udahili lakini wanakosa nafasi kutokana na idadi ndogo ya wanafunzi wanaopokelewa.
Kwa sasa, nafasi zinazotolewa zinaonekana kuwa chache sana ukilinganisha na idadi ya waombaji. Tunaomba uwezo wa udahili uongezwe, kwa mfano kutoka wanafunzi 60 hadi angalau 200, ili kuwapa fursa zaidi wale wanaokidhi vigezo.
Kwa baadhi yetu, tayari tumefanya kazi na kuomba ruhusa kutoka kwa waajiri wetu ili tuweze kujiendeleza kielimu. Baada ya kupata ruhusa, tunapoomba chuo na kukosa nafasi kutokana na ushindani mkubwa wa nafasi chache, hali hii inakatisha tamaa na kuwaumiza wengi ambao walikuwa na matumaini ya kuendelea na masomo.
Aidha, tunaomba MUHAS ifungue tena awamu ya tatu ya maombi ya udahili, kama ilivyotangazwa na TCU, na kutoa nafasi kwa waombaji ambao wamekidhi vigezo vya kozi hiyo.
Pia, tunaomba Serikali na mamlaka husika zizingatie uwezekano wa kuruhusu vyuo vingine kutoa kozi ya Bachelor of Science in Nurse Anaesthesia. Mahitaji ya kozi hii ni makubwa, lakini waombaji wengi wanakosa nafasi kwa sababu ushindani umejikita katika chuo kimoja chenye uwezo mdogo wa kudahili wanafunzi.
Kuongeza nafasi za udahili au kuruhusu vyuo vingine kutoa kozi hii kutasaidia kuongeza fursa za elimu ya juu kwa wahitimu wa Nursing, huku pia kukidhi mahitaji ya wataalamu wa Nurse Anaesthesia nchini.
Tunaomba ombi hili lisikilizwe na kufanyiwa kazi kwa kuzingatia maslahi ya wanafunzi, wataalamu wa afya na mahitaji ya taifa kwa ujumla.