Tunaomba mrudisheni Polepole, huyu alikuwa Balozi hawezi kupotea kama kuku

Kosa langu nini? kusema arudishwe ndo tatizo nimesema mtu kama balozi anapotea kama kuku Je sisi wengine?
Unauliza mtu kama balozi anapotea kama kuku, unashangaa balozi kupotea kama kuku.

Je, Ben Saanane, au raia mwingine ambaye hakuwa balozi lakini kapotea , yeye kupotea kama kuku ni sawa?
 
Unataka arudishwe arudishwe na nani?
Wenye mamlaka ya kulinda raia na mali zake ndo wanatakiwa watimize uwajibu wao ndo wanatakiwa kumtafuta alipo na kumrejesha ndo kazi yao. Police wakisema hawajui alipo huyu ambae alikua mtumishi wa Umma uoni kwamba IGP inatakiwa afukuzwe kazi kwa kutotimiza uwajibu wake?
 
Unauliza mtu kama balozi anapotea kama kuku, unashangaa balozi kupotea kama kuku.

Je, Ben Saanane, au raia mwingine ambaye hakuwa balozi lakini kapotea , yeye kupotea kama kuku ni sawa?
Mbona hoja yangu iko wazi mtu amewahi kua Katibu Mwenezi Taifa Balozi na Mjumbe wa Bunge maalumu la Katiba, alikua Mbunge ndo anawezaje kupotea kama kuku sijasema wote waliopotea hawana Umuhimu hapana tunaangalia Nyazifa za huyu jamaa ambazo kashika huyu huwezi mfananisha na Ben Saanane huo ndo ukweli mchungu mtabaka yapo kwenye maisha ni sawa sawa leo Usikie Waziri mkuu Mstaafu kama pinda kapotea au JK
 
Ukishaanza kutaja nyadhifa maana inayojionesha ni kwamba watu walio na nyadhifa ndio hawafai kupotezwa kama kuku.

Wasio na nyadhifa wapotezwe tu hakuna anayejali, kwa sababu hawana nyadhifa.

La sivyo, kama nyadhifa si muhimu kwenye suala la kupotezwa, kila mtu anatakiwa asipotezwe kama kuku, kwa sababu ni mtu, nyadhifa hazina umuhimu katika hoja hii.

Kwa sababu aliye na nyadhifa hatakiwi kupotezwa kama kuku, asiye na nyadhifa hatakiwi kupotezwa kama kuku.

Sasa hapo nyadhifa zina umuhimu gani ikiwa hata asiye na nyadhifa hatakiwi kupotezwa kama kuku?
 
Kiranga punguza ubishi
 
Kiranga punguza ubishi
Wewe ndiye upunguze ubishi somo rahisi unakataa kuelewa.

Kama kupotezwa mtu, yeyote, balozi, mfagizi, si jambo zuri, halistahili kutokea, then suala la cheo cha mtu katika hoja ya kupotezwa ni superficial.

Hili ni suala la kupanga watu kwa madaraja katika jambo la haki za msingi za binadamu wote bila kuhitaji madaraja.

Umefanya kosa la kuwapanga watu kimadaraja katika suala la haki ya binadamu wote bila kujali daraja.

Huelewi wapi?
 
Miaka 60 wapo Madarakani hujajifunza tu? CCM sio wakuwaomba jambo badilisheni strategy mnawatoa siku sio nyingi.
 
Wenye mamlaka ya kulinda raia na mali zake ndo wanatakiwa watimize uwajibu wao ndo wanatakiwa kumtafuta alipo na kumrejesha ndo kazi yao. Police wakisema hawajui alipo huyu ambae alikua mtumishi wa Umma uoni kwamba IGP inatakiwa afukuzwe kazi kwa kutotimiza uwajibu wake?
Wamtafute vipi wakati hata wao walimuita akatoe maelezo akasema yeye serekali haijamrudisha nchini baada ya kumuachisha kazi kwahiyo bado yuko Cuba, au unamaanisha police wa Cuba ndo wamtafute?
 
Polepole mara nyingi kamasema yuko nchini
 
Bado hajarudi?
abracadabrra bwashasha,
Wiki ijayo tutegemee akiwepo mtaani.
Nipo hapa.
 
Bado hajarudi?
abracadabrra bwashasha,
Wiki ijayo tutegemee akiwepo mtaani.
Nipo hapa.
Suala la Polepole linaongeza chuki kubwa kwa serikali Samia unawezaje kugombea yule aliyekua anapiga uteuzi wako kwenye chama anatekwa Wewe unaendelea kuomba kura hii hapana
 
Ni ukakasi kabisa,wangeongea nae tu waelewane.
Kumnyima haki zake za ustaafu akiwa balozi si haki.
Mambo yao baadae siingilii🙏
 
Tunaomba mrudisheni Polepole kama kuna kosa alifanya mahakama zipo. Huyu alikua katibu Mwenezi wa chama taifa, balozi Mjumbe wa Bunge la katiba pia Mbunge huyu mtu anawezaje kupotea kama kuku?

Tafadhali wakuu naomba mtoe tamko Polepole yuko wapi? serikali ina kila kitu vyombo vyote vya ulinzi twambie polepole yuko wapi? Utu wetu uko wapi na Utanzania wetu tuliojivujia na Umoja wetu inakuaje mtu kama balozi anapotea kama kuku sisi Wengine huku itajuaje?

Pia soma > GE2025 - Gerson Msigwa: Serikali haijui alipo Humphrey Polepole, ndio maana Polisi inafanya uchunguzi
 
Back
Top Bottom