DOKEZO Tunaomba Serikali iingilie kati Hospitali ya Dar Group (T.O.H.S), Mmiliki hajulikani

DOKEZO Tunaomba Serikali iingilie kati Hospitali ya Dar Group (T.O.H.S), Mmiliki hajulikani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Watoto wamezaliwa Kwenye hii hospital hawa jamaa walikuwa vizuri Sana Kwenye huduma zao...
Serikali iingilie Kati haya malalamiko ya wafanyakazi
 
Acha majungu dogo. Husipofuata standard Treatment Guideline NHIF hawawezi kukulipa.

Halafu siyo kweli kwamba STG ina matibabu yote hiyo ni guideline ambayo baadhi ya maeneo ipo very shallow. Wewe utakuwa ni miongoni wa madaktari wazembe, mpenda majungu kwenye hiyo hospital.
Mheshimiwa kwanza uwe na adabu unapotoa hoja zako, katika maelezo yangu sijasema kwamba STG ina matibabu yote ila ni mwongozo i.e summary inayomsaidia daktari ku assemble shule yake ya miaka mitano na mwaka mmoja wa utayari.

Kitu nilichoelezea ni mashinikizo ya kutubu nje ya muongozo na nje ya miiko ya kidaktari...kujaza vipimo vingi amabavyo haviko relevant na presenting condition ya mgonjwa au ku-exacerbate symptoms ili vipimo viandikwe vingi na dawa ziandikwe nyingi.

Kama ni daktari au mtaalamu wa afya utakuwa umenielewa.
 
Kumbe hospital zisizo na wamiliki ni nzuri aisee.mimi naifahamu hiyo hospitali .ina huduma nzuri kuliko Amana na Temeke.Nadhani maboresho ni waiwekee bodi yenye nguvu ila wasiichukue serikali maana itaharibika.imeweza kujiendesha kwa 100% big up mkurugenzi.ijapo mpigaji ila umehakikisha huduma zinapatikana pia.hilo ndiyo la msingi.Kulingana na maelezo yao inaoneka pia huyu DG ameweka usimamizi madhubuti ikiwa ni pamoja na kuajdili mtu wa surprise monitoring/visit kwa vyumba vya madaktari ili kuzuia uzembe na upigaji (wa watumishi (wenyewe manaitaga CCD)manes na madaktari).

Nadhani Huyo DG angukuwa siyo strick,ingeshakufa zamani hiyo hospitali
Hii hospitali ina miaka zaidi ya 40 lakini inazidiwa na hospitali za juzi kama Rabininsia na bochi....!! Ni bora iwe chini ya uangalizi maalumu ili iendelezwe kuliko kuwa kisima cha wachache.

Shughuli za kitabibu hazisimamiwi kama unavyosimamia shamba lako au mtumishi wako wa ndani...kuna namna ya ku deal na haya mambo huku uki maintain privacy ya mteja. assume ww uko na daktari halafu mlango unafunguliwa ghafla na mtu aliyeshika nyundo mkononi.....huo ni ubakaji wa taalauma.
 
Mmmh Kuna mengi ya ukweli, nikiwa mteja mzuri hapo hospital kiukweli morali ya wahudumu hasa manesi umeisha sababu wanapunguzwa kazini, nilipiga story na baadhi yao ni kuwa wale wazoefu mkataba ukiisha na chako ndo kimeisha na hakuna ku-renew na hata mafao yao kuandikiwa umekuwa mtihani, kwa sasa Kuna upungufu wa wahudumu na wachache walioajiliwa bado hawajawa na uzoefu. So waliobakiza muda mfupi wanaenda kutimiza tu wajibu Ila hawana morali ndicho nilichoona.
Broo kuna mdada ni mjamzito... mkataba wake nadhani umeisha na kanyimwa mkataba mpya japo ni mjamzito... mtu aliye nje hawezi jua kero zilizopo katika ile hospitali na hakuna mfanyakazi mwenye ujasiri wa kureport sehemu yoyote.
 
Kama kuna Hospitali ambayo Serikali ilitakiwa iimarishe zaidi ni hii, lakini nasitika imekuwa ni kama Mtoto Yatima huku pia ikidharaulika na Watu.
 
Hapa naona kama majungu kazini,Mimi na familia yangu ni Mdau mkubwa sana kwenye hiyo Hospital huduma zake ni nzuri sana na hospital inafanywa maboresho kuanzia majengo hadi huduma.
Unahudumiwa vizuri sababu madaktari na wahudumu wanajua nini wajibu wao... ila moyoni wana uchungu mwingi... usitete jambo usilolijua. Fanya uchunguzi, kwanini majungu yaanze leo yasianze zamani. Unajua kwamba hata benki ya CRDB ambayo ndio mishahara ya wafanyakazi wa pale inapitia hapo haiwakopeshi kwa sasa sababu ajira zao hazina uhakika. Ndugu usihukumu au kutoa hitimisho... usiwakaange wenzako sababu wewe upo kivulini.
 
Kama kuna Hospitali ambayo Serikali ilitakiwa iimarishe zaidi ni hii, lakini nasitika imekuwa ni kama Mtoto Yatima huku pia ikidharaulika na Watu.
hakika ndugu...hii hospitali ipo strategic area....highway inapita pale. iltakiwa iwe hospitali kubwa huenda kuliko hspital za rufaa na za kanda tunazozifahamu. wanachi wengi wanahangaika kwenda mbali lakini wangeweza pata huduma zote pale.
 
Watoto wamezaliwa Kwenye hii hospital hawa jamaa walikuwa vizuri Sana Kwenye huduma zao...
serikali iingilie Kati haya malalamiko ya wafanyakazi
Hospitali ya Dar group imejaaliwa wahudumu wa faya wenye weledi wa hali ya juu, wapo kwenye mazingira magumu lakini wanafanya kazi as if " ni salama na shwari" ila kwa sasa naona maji yanazidi unga... naona uvumilivu unawashinda. Ila ni the best doctors, ukiachana na wahudumu wa afya hata watumishi wa kada zingine wapo vizuri sana.
 
Hiyo kwenda tofauti na Mwongoz wa matibabu wa Serikali kwa ajili ya kujiongezea mapato ni uhujumu uchumi
Exactly...na hiyo ni dilema kubwa...kazi unaitaka na miiko ya kazi unataka kuifata. Nacho wapongeza madaktari ni kujitahidi kukaa kwenye miiko yao na kufanya walichofundishwa darasani japo mazingira si rafiki.
 
Kuna mambo huwa ni rahisi sana kuyatatua wala hayahitaji serikali, hapo ni kuhamasisha wananchi wasiende kupata huduma kwenye hiyo hospitali, baada ya hapo itakufa natural death, full stop.
 
hii hospital ina miaka zaidi ya 40 lakini inazidiwa na hospitali za juzi kama rabininsia na bochi....!! ni bora iwe chini ya ungalizi maalumu ili iendelezwe kuliko kuwa kisima cha wachache.

shughuli za kitabibu hazisimamiwi kama unavyosimamia shamba lako au mtumishi wako wa ndani...kuna namna ya ku deal na haya mambo huku uki maintain privacy ya mteja. assume ww uko na daktari halafu mlango unafunguliwa ghafla na mtu aliyeshika nyundo mkononi.....huo ni ubakaji wa taalauma.
Labda tabia zenu nyinyi madaktari wa hapo ndio imewafikisha hapo, yaani hamuaminiki. Mna side deals nyingi sana, yaani mwizi kapewa kazi ya kuchunga wezi wenzie
 
Labda tabia zenu nyinyi madaktari wa hapo ndio imewafikisha hapo ,yaani hamuaminiki .mna side deals nyingi sana.yaani muizi kapewa kazi ya kuchunga wezi wenzie
Sio lazima uchangie ndugu... hata kama umepewa maelekezo basi shirikisha na fahamu zako kidogo. Be humble sio kila kitu utakuwa na majibu yake... ukikaa kimya utakuwa mwenye hekima zaidi.
 
Ukiona mfanyakazi mswahili anasifia management ujue manager hasimamii vizuri...

Huu uzi unaashiria mkurugenzi hataki ujinga..
 
Kwa siku za hivi karibuni, hospital ya Dar Group (T.O.H.S) imekuwa na mgogoro na wafanyakazi wake, hali inayopelekea mzoroto wa huduma za afya katika hospitali hiyo iliyopo eneo la Tazara ikiwa imetazamana na Azam TV, mfugale fly over na kupakana na TBC.

Chanzo cha mgogoro katika hospitali hyo ni ubabe na unyanyasaji wa mkurugenzi mkuu (D.G) wa hospitali hiyo.

Wafanyakazi wamekuwa wakiachishwa kazi kiholela kwa taarifa ya masaa 24 au kupewa shinikizo la kuandika barua ya kujiuzulu ndani ya masaa 24 nakumfanya mfanyakazi kupoeza stahiki zake.

Mkurugenzi mkuu amekuwa na kawaida ya kuingilia taaluma adhimu ya udaktari na kuwashinikiza madaktari kutoa tiba nje ya muongozo wa tiba wa taifa (STG) ili kujitengenezea faida zaidi kutoka katika mashirika ya bima za afya.

Aidha inaripotiwa kwamba kumtukana na kumvunjia heshima mtumishi mbele za wateja(wagonjwa) ni kitu cha kawaida kwake, na endapo utahoji basi unaweza kufukuzwa au kuhamishwa kituo cha kazi. mifano ya wafanyakazi waliokumbana na kadhia hyo ni; daktari daraja la pili (M.D) ambaye amehamishiwa katika DISPENSARY ya shirika iliyopo mbeya. pian kuna daktari daraja la pili(M.D) ambaye amesimamishwa kazi kwa kipindi cha mwezi bila kosa lake kubainishwa huku madaktari na wafanyakazi wengine wengi wakiandikishwa barua.

Aidha mkurugenzi ameajiri mtu amabaye kazi yake nikukagua vyumba vya madaktari, na anaingia muda wowote bila taarifa hata kama upo na mteja, jambo linaoharibu usikivu na utoaji huduma bora kwa mteja kwani huduma za kitabibu ni siri baina ya daktari na mteja wake.

Mkurugenzi mkuu amemfukuza kazi mkurugenzi wa fedha(Director of finance) , na kwa kipindi hiki yeye ni mkurugenzi mkuu na msimamizi wa fedha kwa wakati mmoja(monopolisim).

Kwa ujumla hali za wafanyakazi katika hospital ya dar group zipo matatani, hakuna mwenye uhakika na ajira yake masaa 24 yajayo labda uwe kipenzi cha mkurugenzi mkuu. Wafanyakazi wanafukuzwa na kusimamishwa kazi kiholela kwa utashi wa mkurugenzi mkuu.
sintofahamu inayoendelea hospitalini hapo imepelekea kupoteza morali na hali za wafanya kazi nakupelekea huduma zisizokidhi viwango kwa wateja.

A. DAR GROUP (T.O.H.S) NI HOSPITALI YA NANI??

I. KUANZISHWA

Ilianza kama kituo cha kutoa mafunzo kwa afya za wafanyakazi wa viwandani mnamo mwaka 1967.

Baada ya muda kupita ilionekana hitaji la kufungua hospitali ili ihudumie wafanyakazi kwa wakati na kuwawezesha kurudi kwenye majukumu yao kwa wakati. Mashirika zaidi ya mia moja(100) yalifikia muafaka wa kufungua hospital na ikawa ikiendeshwa chini ya usimamizi wa mashirika hayo. Baadhi ya mashirika ni pamoja na ; ORYXY, TANITA, DABREW, KIOO, ARAF, CRDB, NATIONAL BATTERY na IFM ambayo yalitoa wajumbe wa bodi na mwenye kiti wa bodi kwa awamu.

mnamo mwaka 1971 tar 9 Agosti, hospitali ilifunguliwa rasmi na hayati baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, wakati huo ikijulikana ka Kliniki wa wafanyakazi.

II. MUUNDO WA T.O.H.S(DAR GROUP) YA AWALI

Hospital ilikuwa ikiendeshwa na bodi yenye wawakilishi kutoka mashirika anzilishi. mwanyekiti wa bodi alikuwa akidumu kwa awamu na kila awamu alkuwa akitoka moja ya shirika anzilishi. Hakuwa mwenyekiti wa milele. Mkurugenzi mkuu aliteuliwa na bodi na alikuwa anawajibika kwa bodi.

III. DAR GROUP (T.O.H.S) CHINI YA DR NELSON.

Huyu alikuwa daktari mwenye asili ya India ambaye wakati wake wa Uongozi kulikuwa na manyanyaso na uvunjaji wa haki za biandamu. pia wakati wake kulikuwa na kashfa ya kuwapa wagonjwa dawa zilizoisha muda wake (expire). Serikali ya awamu ya pili chini ya rais Ally Hassan Mwinyi iliingilia kati nakuagiza daktari huyo( mkurugenzi mkuu) kuacha kazi ndani ya saa 24.

IV. DAR GROUP (T.O.H.S) CHINI YA DR LOUIS MLINGI.

Alifuata baada ya Dr Nelson. Aliongoza kama mkurugenzi mkuu kwa kufuata misingi ya utawala bora hadi mwanzoni mwa mwaka 2018.

V. KUFA KWA MASHIRIKA.

Baadhi ya mashirika yalikufa jambo liliopelekea bodi ya wakurugenzi iliyoundwa na wawakilishi kutoka katika mashirika hayo kufa na kutoa mwanya kwa watu wachache kuichukua hospitali na kuifanya kuwa hospitali binafsi ( private hospital) ambayo mmiliki wake hajulikani.

B. DAR GROUP (TOHS) MPYA.

- Ni hospitali binafsi ambayo mmiliki wake hajulikani.

- Inaundwa na bodi yenye wajumbe amabao ni wafanyakazi (waajiriwa) wa hospital ambao kimsingi hawana uwezo wa kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu maana ni bosi wao. hivyo kwa lugha nyepesi ni " bodi hewa".

- Iwenyekiti wa bodi anatoka kampuni ya Tanzania Oxygen ambaye anaonekana hana sauti kwa mkurugenzi mkuu kwani umri wake umeenda.

- Haijulikani mkurugenzi mkuu anapatikanaje na anatakiwa kuwa na sifa zipi.

- Hakuna chama cha wafanyakazi.

- Gharama za matibabu kwa wateja ambao sio wanufaika wa bima za afya zipo juu sana hali inayowanyima fursa raia na walipa kodi wa kipato cha chini kupata huduma.

- Ina zaidi ya miaka 40 lakini bado imedumaa kimaendeleo licha ya kupokea wastani wa wagonjwa 400(mia nne) kwa siku.

- Ni hospitali kongwe lakini haina wodi za kutosha kulaza wagonjwa, hakuna jengo la kuhifadhia maiti, hakuna huduma ya CT-scan, hakuna kitengo cha watoto wachanga. kuna jengo la ICU lakini hakuna huduma mdhubuti za ICU. kuna jengo la huduma ya dharula lakini hakuna vifaa tiba wala dawa zakutosha kuhudumia wagonjwa wa dharula.

- Mapato ya hospitali ni makubwa lakini hospitali haiendelezi huduma zake wala majengo licha ya kuwa na eneo kubwa la takriban hekali nne. pesa zinatumiwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi nakuacha hospitali ikiwa kama mtoto yatima asiye na msaada.

C. OMBI KWA SERIKALI SIKIVU YA MH Dr JOHN JOSEPH POMBE MAGUFURI YA "HAPA KAZI TU"

I. Iteue tume ya kuichunguza hospitali ya Dar group(T.O.H.S) - Kujua chimbuko lake, uhalali wake wa kuwa hospitali binafsi, umiliki wake na mapato na matumizi ya hospitali hiyo.

II. Iwakusanye waanzilishi halisi wa hospitali hiyo(mashirika anzilishi) na watengeneze bodi ya wakurugenzi yenye meno itakayo simamia mapato na uendelezwaji wa hospitali na upatikanaji wa mkurugenzi mkuu mwenye kariba na weledi wa uongozi.

III. Kwasababu hospitali imeshindwa kujisimamia na dhumuni mama la kuanzishwa ...yaani kuhudumia wafanyakazi halifanyiki tena, basi serikali iiteue kuwa moja ya hospitali au taasisi chini ya wizara ya afya ili kutanua wigo wa huduma na kupunguza mzigo kwa hospitali za temeke na amana. Hospital ina eneo kubwa sana ambalo likiendelezwa inaweza kutoa huduma bora kwa wakazi wa wilaya ya temeke, ilala na viunga vyake.

NAWASILISHA, MIMI MWANANCHI MVUJA JASHO, MLIPA KODI MWENYE MAPENZI MEMA NA NCHI YANGU MAMA AFRIKA, TANZANIA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

View attachment 1652088
 
Ukiona mfanyakazi mswahili anasifia management ujue manager hasimamii vizuri...

Huu uzi unaashiria mkurugenzi hataki ujinga..
Kwahiyo kila mtawala anayelalamikiwa na walio chini yake ni sababu hapendi ujinga?? Kama watu wangekuwa wanapambanua mambo kwa staili hii basi kusingekuwa na vyombo vya kusikiliza watu au platform kama hizi..!! Kama jambo hulijui pata muda ulifatilie kwa kina. halafu punguza fikra za kigeni..." kuwa mswahili " sio fedheha....jivunie vya kwako.
 
Back
Top Bottom