Mama Sinono
Member
- Jun 4, 2013
- 7
- 2
Dear Serikali, kuna tetesi kuwa wananchi wako wa Kunduchi Mbuyuni wanatakiwa kuondoka kupisha mradi wa Serikali wa mwendokasi.
Tatizo wananchi hatujawekwa wazi kuhusu huo mradi. Taarifa zinakuja kienyeji. Mfano mimi jana ndo mjumbe ananipigia simu kunieleza kwamba watu wa kuthaminisha maeneo wamekuja (property valuation). Nawauliza wanasema watu wote walishapewa taarifa wiki tatu kabla. Kitu ambacho si kweli.
Hakuna uwazi kabisa na taarifa zinatolewa kimafungu. Waliwaita baadhi ya watu sio wananchi wote na wanaconclude kwamba wananchi wote tumeridhia kitu ambacho si kweli. Tunaomba Serikali itoe taarifa rasmi na wote tushirikishwe kwa pamoja sio divide na rules approach walitumia.
Ombi letu kama huo mradi upo tunaomba uwazi ,tupewe barua rasmi ya wito wa kikao, taratibu zifuatwe na kuwepo na uwazi. Pia tunaomba viongozi wa Serikali (Waziri husika, Mbunge, Mkuu wa Mkoa, DART, Mkuu wa Wilaya wajitokeze ili tuone uhalisia wa huo mradi.
Please tuaomba utusaidie wananchi wako. Tunaona hakuna haki kwenye hili. Yaani ni tetesi kila mtu anasema lake.
Tunaomba sana Serikali iweke wazi. Na ni eneo lipi haswa. Maana inaenekana wameongeza na eneo tofauti na proposed eneo husika(tetesi.). Eneo wanalohitaji ni kubwa.
Tunaomba ufike uongee na wananchi wote tujue mradi unaukubwa wa eneo gani. Ni wapi unaanzia na kuishia. Maana taarifa zinachanganya sana. Pia tunaomba Ikiwezekana zoezi la kuthaminisha maeneo wasitishe kwanza.
Wananchi tuitwe wote kwa pamoja kwa utaratibu rasmi. Samahani kwa kutumia hii platform tumekosa msaada.