Tunaomba turudishiwe fedha zetu za maombi kutokana na ugawaji wa viwanja kwa upendeleo jijini Mwanza

Tunaomba turudishiwe fedha zetu za maombi kutokana na ugawaji wa viwanja kwa upendeleo jijini Mwanza

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Ni masikitiko makubwa kuona upendeleo wa dhahiri wa ugawaji wa viwanja katika Jiji la Mwanza. Wote tulitangaziwa kuomba viwanja hivyo kwa ada ya Tshs.20,000 kwa kila kiwanja lakini cha kusikitisha waliopata viwanja ni vigogo ambao hata hawakufika kuchukua fomu na kuzijaza.

Hivi ni kweli mtu alitoka Bungeni, Dar(TRA) kuja kuchukua fomu na kuzijaza na kuzirudisha. Nashauri turudishiwe fedha zetu za maombi kutokana na ugwaji kuwa wa upendeleo sana.

Kweli Mhe. Magufuli tutakukumbuka. Upendeleo kama huu usingetokea kama ungekuwa Rais. Tunamwomba Mhe. Rais asitishe ugawaji huu na uanze upya ili taratibu na kanuni zifuatwe.
 
Kamba yako fupi mkuu...kaa kwa kutulia.
 
Magufuli huyo huyo alichota pesa za wastaafu.Wastaafu wanamlaani tu.
 
Ni masikitiko makubwa kuona upendeleo wa dhahiri wa ugawaji wa viwanja katika Jiji la Mwanza. Wote tulitangaziwa kuomba viwanja hivyo kwa ada...
Hizo ni dili za wakurugenzi kuwapiga buku 20 zenu, tena lazima itakuwa uliandikiwa non refundable, kwahiyo usitupigie kelele hapa.

Huyo Magufuli kumtaja hapo ndio umekosea, yeye ndio alikuwa mbaguzi namba moja.
 
Back
Top Bottom