Tunaomiliki magari ya mzungu tukutane hapa

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
55,727
Reaction score
123,094
Wale wamiliki na wanaopenda kumiliki magari ya Mzungu tukutane hapa kwa ushauri na kubadilishana mawazo. Najua ni changamoto sana kumiliki haya magari hapa Tanzania kuanzia mafundi, spare na uchumi vilevile. Nina uzoefu mkubwa sana kwenye haya magari.

Niulize chochote kuhusu magari haya nitakujibu kwa uzoefu wangu. Karibuni tujadiliane. Jitahidi kununua gari isiozidi miaka 10 kwasababu vitu vingi kwenye gari vinachoka baada ya miaka kumi.

Maoni ya wadau:
 
Baba Taibali anakusalimia.

Hivi LandRover, Range Rover 504 na 505 na Vogue, haya asili yake ni wapi, Japan au German?

Kuna mtu kaniambia nichague zawadi ya birthday mwaka huu.

I'm thinking...🤔🤔🤔
 
X3 2.5i au 2.5si sio mbaya kama huna hela ya mawazo kwenye wese,spare kama kawaida gari za Mzungu zipo juu. X3 roho ya paka na zipo mjini kitambo so sio issue sana kwenye ufundi.
Kwenye wese unamaanisha kwamba mtu ajipange au? Kwamba consumption si ya kitoto?
 
Bavaria, Kijana amemaliza chuo, amekomaa na forex akapata 20'000$. $20,000 on the road? That's nearly Tshs 50m. Anaweza kupata 2008-10 VW Touareg Tdi au V6 Petrol, Mercedes M class W164 2007-10 diesel or petrol au BMW X5 E70 2008-10 3.0si
 
Naona unatutisha tukae mbali. Hio hata ukipewa bure inabidi uwe na hela otherwise mtoaji aendelee kuihudumia.
Napenda sana magari ila sipendi hadi bovu, bora nipaki nipande bajaji au Uber au daladala.

Mtoa zawadi ana fahamu kuwa zawadi ikishatolewa inatakiwa itunzwe....

Kwani Euro 900 ni sawa na Tsh ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…