Tunaomiliki magari ya mzungu tukutane hapa

Tunaomiliki magari ya mzungu tukutane hapa

M sijawahi kumiliki gari ila Mungu akisaidia mwisho wa mwaka ntavuta chuma,na sio mpenz wa toyota katika pitapita zangu nimeona Audi A4 ya 2005 mpaka2006 ndo naweza afford je unaushari gani mkuu?kwa gari ya kwanza?nimeielewa sna

Sent using Jamii Forums mobile app
A4 nzuri. Spares zipo nyingi na si ghali sana.
 
Mungu amenijalia nimetumia VOLKSWAGEN KHARMANN GHIA (ya kizamani sana hii)
Peugeot 504 pick up, Land Rover 110 TDi, Mercedes Benz E190, ML500, E200 (W210),Volkswagen Golf MKIV, AUDI A4, na VOLKSWAGEN TOUAREG 2.5.

Hizi ni gari za ukweli,changamoto tu ni gharama za maintanance.

Mafuta pia inategemea na ukubwa wa engine, nyingi za 4 cylinders,ulaji wake ni kawaida sana.

Mfano hiyo Mercedes Benz E200 ni CC1990 bila kompressor ya mwaka 1998, full tank petrol ni 60 ltrs, natoka nayo Dar mpaka Arusha inasalia chini kidogo ya robo tank.

Hiyo ML500 ni almost 5000cc V8 petrol , full tank 95ltrs Dar - Arusha,taa ya mafuta itawaka na salio la lita kama 10.

Hapo zote mshale unacheka kati ya Kph 120 mpaka 160,kisha kidogo 180 na mara chacheee nafika mpaka 200 kwenye maeneo huria na barabara tulivu kama lami ya Korogwe mpaka Same.

Volkswagen ulaji wake wa mafuta naona ni chini zaidi kulinganisha na Benz,pia hata maintanance ya VW iko nafuu.

Kwa ujumla gari za mzungu wa ulaya Nzuri sana,kupata uhalisia,,, endesha au Basi hata safiri nayo ukiwa abiria,,, Safari ya masafa marefu utafurahia zaidi kuliko towntrip...

Na sasa nazimia sana Range Rover Autobiography toleo la kuanzia 2013 kuja mbele,na Bentley Arnage T2 (2007-2009) na Bentley Mulsanne.

One day Yes kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu Muumbaji wa mbingu na nchi,bahari na chemchemi za maji na vyote vilivyomo.
 
Wale wamiliki na wanapoenda kumiliki magari ya Mzungu tukutane hapa Kwa ushauri na kubadilishana mawazo. Najua ni changamoto Sana kumiliki haya magari hapa Tz kuanzia mafundi,spare na uchumi vile vile. Nina uzoefu mkubwa sana kwenye haya magari. Nimetumia BMW,Mercedes,Audi, Volvo na sasa hivi natumia VW Golf Mk5 2.0FSi. Niulize chochote kuhusu magari haya nitakujibu kwa uzoefu wangu. Karibuni tujadiliane. Jitahidi kununua gari isiozidi miaka 10 kwasababu vitu vingi kwenye gari vinachoka baada ya miaka kumi.
Mkuu kuna hizi VW Touran Golf za cc 1600,1400 na 2000. Kwanza kati ya hizo,ipi ni nzuri. Wadau wengu wanasema hayo magari yanasumbua sana. Lakini kipekee nayapenda mwenokano wake pamoja na speed. Je gari hizo spea zipo!? Je hazina changamoto ya kusumbua mifumo ya umeme,engine,gia box? Mafundi wapo na ni wabobezi au ikoje? Zipo kuanzia 2005 na kibongobongo angalau 2010 inakua poa. Naomba info,nitashukuru.

Engine nzuri cc2000. Gari ikishazidi miaka 10 ni wazi kuna vitu vinaanza kuchoka inabidi ubadilishe. Shida kubwa gari hizi vitu ni bei kubwa kidogo ila spare zipo na mafundi wapo
 
Wale wamiliki na wanapoenda kumiliki magari ya Mzungu tukutane hapa Kwa ushauri na kubadilishana mawazo. Najua ni changamoto Sana kumiliki haya magari hapa Tz kuanzia mafundi,spare na uchumi vile vile. Nina uzoefu mkubwa sana kwenye haya magari. Nimetumia BMW,Mercedes,Audi, Volvo na sasa hivi natumia VW Golf Mk5 2.0FSi. Niulize chochote kuhusu magari haya nitakujibu kwa uzoefu wangu. Karibuni tujadiliane. Jitahidi kununua gari isiozidi miaka 10 kwasababu vitu vingi kwenye gari vinachoka baada ya miaka kumi.
Hapo kwenye Golf Mk5 nakukubali sana.
Hiyo kitu ni simple machoni ila mziki wake barabarani ni hatari.
Nishatembea na Golf Mk 5 2.0 GT (sio GTI)
Kiatu chake na burdani si mchezo
 
Jeep Grand Cherokee gari nzuri sana cha kushangaza bei yake ikiwa mpya ni ya chini kuliko magari mengi tuliyoyazoea.
hilo unalosema linawezekana maana hata huyo jamaa aliyenunua hiyo gari hafanani na perception za watu wengi na mimi nikiwemo za bei ya JEEP.
 
Hapo kwenye Golf Mk5 nakukubali sana.
Hiyo kitu ni simple machoni ila mziki wake barabarani ni hatari.
Nishatembea na Golf Mk 5 2.0 GT (sio GTI)
Kiatu chake na burdani si mchezo
Yeah ni gari ya kawaida, haina makuu ila iko vizuri barabarani na kiuchumi.
 
Back
Top Bottom