Tunaomiliki magari ya mzungu tukutane hapa

sakasaka,
1 series haina tofauti na BMW 3 series E90(2005- ). Zina-share kila kitu kasoro body tu. BMW ni BMW barabarani imetulia hata iwe 1 Series. Service ya kawaida tzs 100,000-150,000. Vitu vinavyosumbua ni vile vile vya gari yoyote used, ila BMW lazima uwe na hela sio kama Toyota.
 
kaka kwema, naomba unijuze kuhusu landrover discovery 2 2.5 td5 juu ya
1. Ulagi wa mafuta
2. Upatikanaji wa mafundi
4. Upatikanaji wa spea
5. Na gharama mpaka mkononi kutokea uingereza

Natanguliza shukran kaka
1. Mafuta inatumia vizuri sana
2. Mafundi wapo wengi
3. Spares zipo nyingi tu
4. Gharama inategemea unanunua yenye hali gani, kodi tumia kikokoteo cha TRA.
 
Asante Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeep Grand Cherokee gari nzuri sana cha kushangaza bei yake ikiwa mpya ni ya chini kuliko magari mengi tuliyoyazoea.
Unanishawishi sasa vp spea zake na mafundi wapo wapo
 
Mimi nimetokea kuipenda sana VW Jetta 2006 option nilizonazo ni kati ya 2005-2006 BMW 320i ila jamaa zangu wananiambia Jetta itanipa shida sana kwenye spare, ninachoipendea Jetta ni urahisi wa kuipimp ina pimpika vizuri sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…