Tunaomjua Mwamba wa Lusaka (Chama) na makubwa aliyoyafanya katika ligi hii lazima tutafakari tuhuma alizopewa kuwa ni mtovu wa nidhamu

Tunaomjua Mwamba wa Lusaka (Chama) na makubwa aliyoyafanya katika ligi hii lazima tutafakari tuhuma alizopewa kuwa ni mtovu wa nidhamu

Chama amefanya mengi Simba,hata hatua tuliyofikia kwenye Champions league ana mchango mkubwa,ila kwa sasa hana cha ku-offer tena Simba, namba haziongopi. Aidha kiwango kimeshuka au hajisikii amani tena kuwepo Simba na si dhambi kwake. Itoshe tu kumwambia Thank you Chama.
Wampe thank you Kama wanaona anastahili lakini siyo kuzusha utovu wa Nidhamu.
 
-Taarifa zinasema mwalimu wa viungo wa Simba aliwaita wachezaji kupasha miili joto katika mchezo dhidi ya Wydad AC, Chama alikua bado anataka kuuchezea mpira so alichelewa kidogo kwenda, ukatokea ubishani na mwalimu kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
..
Ndugu Phiri hakuvaa bips ya mazoezi yenye nembo ya CAF ilhali wapo katika mchezo wa CAF, ikatafsiriwa kama hakuwa siriaz na mchezo hivyo akawekwa pembeni kabisa katika mchezo huo dhidi ya Wydad.
..
Shehe Kapama hakufika mazoezini hii ni kabla ya mchezo dhidi ya Wydad AC, alimpa sababu mwalimu wa viungo kuwa alikua anaumwa na alikuwa hospitali, mwalimu wa viungo akasema anatakiwa kupewa taarifa hiyo na mwalimu mkuu Benchikah sio Mchezaji.m
 
Utovu wa nidhamu ni nini?

Lazima ujue kwanza maneno hayo yanamaana pana sana. So usikimbilie ku judge.

Cha msingi ni hao wanaosema kuwa ana utovu wa nidhamu wabainishe ni kipi alichofanya kila mtu afahamu.

Simba ni taasisi, kwanini wanaficha taarifa muhimu? Kulikuwa na haja gani yakurelease hiyo statement kisha kuficha huo utovu wenyewe?
Imagine wakisema chama ni kibaka mwizi ktk jamii inaleta picha ipi kwa upande wangu naona ni statement sahihi kama ulivosema utovu wa nidhamu ni neno Pana lenye ukakasi ndani.
Wacha tusubiri nani yu sahihi kati ya bwana chama na waajiri wake
 
Unajua kafanya nini kwanini tusielezwe alichofanya tukipime
Muhusika si kajulishwa kuwa amekiuka utaratibu wa taasisi yake [emoji16]
Ni vema mngelimtafta chama mmuulize kwa mapana zaidi[emoji16]
Kwani manyara anasemaje si mshikaji wake[emoji2][emoji2][emoji2]
Kama vipi aje yanga achukue nafasi mnata
 
Nionavyo mimi ni kiwango kidogo anachoonesha uwanjani kimesababisha yote hayo.

Kuhusu longolongo za malipo hizo zipo tuu hakuna klabu inayolipa wachezaji kwa asilimia zote.

Licha ya kuonekana angalau tumejipata lakini ligi yetu bado sana kuhusu maslahi ya wachezaji.
 
Imagine wakisema chama ni kibaka mwizi ktk jamii inaleta picha ipi kwa upande wangu naona ni statement sahihi kama ulivosema utovu wa nidhamu ni neno Pana lenye ukakasi ndani.
Wacha tusubiri nani yu sahihi kati ya bwana chama na waajiri wake
Kama ni kibaka asemwe. Kuficha ndio kutaleta picha nzuri?

Kama taasisi kuwa responsible na trasparent ni jambo zuri. Kufichaticha mambo ndio huarisbu taswira ya taasisi.
 
Timu za kariakoo (Simba sc na Yanga Sc) Hawa mapacha huwa wanakasumba sana haswa Hawa viongozi wanapoulizwa kuhusu suala la masilahi.

Nimemshuhudia Chama (kipenzi Cha mashabiki) akicheza mpira katika ligi yetu hii kwa nidhamu kubwa kwa misimu kadhaa bila kusikia kakwaruzana na mchezaji mwenzie au kiongozi mwenzake je leo hii Kuna Nini kwa Chama?

Tulizoea kusikia Mkude kafanya hivi au Benard Morson kafanya kile hapo nzungumzia wakiwa Simba sc acha Yanga Sc kwa Bernard morsoni watu Kama Hawa mwisho wa siku mashabiki tulizoea kutokana na utundu wao.

Aliachwa Saidoo ntibazonkiza pale Yanga Sc juu juu tu hakuna sababu ya maana iliyoelezwa, hii ni kasumba kwa timu yetu/timu zetu za Kariakoo na hii hutokana na viongozi kutoa ahadi zisizo na vitendo na wachezaji wakihoji wanaonekana ni watovu wa Nidhamu.

Maoni Yangu: ifike hatua timu za kariakoo ziache janja janja haswa kwenye masilahi/posho za wachezaji.

Hakuna shabiki wa Simba sc na Yanga Sc asiyejua kuwa Chama kwenye Suala la nidhamu yupo vizuri Ila janja janja za viongozi wa kariakoo huwa zinatengeneza hadithi za kumtoa mtu kwenye Reli.

Nawasilisha hoja.
Lazima umjue Mwamba wa Lusaka maana huwa anakushikisha ukuta
 
Hoja yako umeielezea upande mmoja tu wa Chama.

Chama kila kipindi cha usajili huwa anakuja na drama zake.

Nitajie mwaka gani ambao msimu wa usajili umefika hujasikia longolongo za Chama

Akifakisha achukuliwe hatua na hiyo ndio inapaswa kuwa nidhamu endelevu, wachezaji wajue kuheshimu mamlaka.

Sisi mashabiki na sisi tutambue kuwa wachezaji wetu tunaowapenda tuna fursa ya muda mdogo sana ya kumuona mchezaji.

Katika huo muda ni awapo kiwanjani tu, na akiwa hapo hutamuona akiongea.

Maana yake kuna mengi yanayofanyika akiwa eneo ambalo sisi mashabiki hatupo.

Eneo hilo ndio sehemu anayopata fursa ya kuongea na kufanya mambo mengi ambayo mengine pengine hata sisi mashabiki tungepata fursa ya kuyaona kama si kupunguza mahaba yetu basi tungeweza kumchukia mazima.

Sasa kama huko ndio anafanya mambo yanayokiuka sheria, sisi mashabiki hatuwezi kuwa na guts za kuwalaumu viongozi kwa adhabu watayotoa kisa tu ni mchezaji kipenzi.
Asante Sana Scars Kwa ufafanuzi mzuri. Lakini haya yote yasingeongelewa kama upande wa mashitaka ungekuwa umeweka Wazi kosa/makosa ya mtuhumiwa hadharani. Hapa wanachofanya watu ni kuwa upande wa Mnyonge. Hebu elezeni Chama kafanya nini ili Mahakama ya Jamii ipitishe hukumu ya Wazi.
 
Ukikipima baadae utamuondolea adhabu iliyotolewa? Au unahisi club inaonea wachezaji? Suala limepelekwa kamati ya nidhamu likajadiliwe, we ni nani haswaa na why midomo kwa chama mbona hamuongelei Kapama? Mapenzi yenu kwa mchezaji isiwe kigezo cha kuona fulani kaonewa, acha kamati husika ilitazame.
Sisi ni Wadau wa mchezo huu, tuna haki ya kujua chanzo cha tatizo. Kama walitaka iwe Siri wangeacha kimya tangu mwanzo.
 
Back
Top Bottom