Tunaopitia hii changamoto tupeane ushauri

Pisi kali

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2019
Posts
1,234
Reaction score
2,535
Habari za weekend wakuu


Changamoto yangu haswa kubwa ni hii
Mimi ni binti wa kwanza kwa mama yangu tumezaliwa wawili, tumelelewa single parent Ila kwenye extended family.
Tatizo linakuja mma yangu mzazi kabisa kanilea kanisomesha hadi nimemaliza form 4, (primary kayumba secondary za momy am going).

Kuingia chuo hapo kati nikaanza vibiashara vidogo dogo pia nilikua na boyfriend (x bf) alikua akinisaidia sana kwenye mambo mengi haswa elimu, miaka yote mitatu ya chuo kuhusu kula, mavazi na malazi ilikua juu yangu sio mama wala familia yangu sikua tegemezi na hadi sasa.


Bado sijabahitika kupata kazi ila najimudu maana kuna vibiashara vinanikeep busy kidogo na kunisaidia vitu vya hapa na pale.

Hiyo ni habari yangu kwa ufupi, changamoto inakuja mama yangu hajawahi kunipa baraka yoyote ile hata kusema Mungu akusaidie mwanangu, cha zaidi yeye ni kuniomba hela tu na nikisema sina ni kosa nitasemwa hapo hadi kutolewa radhi!!! Muda mwingine namwambia mm bado sijapata ajira na sijakaa sawa kimtaji hiki kidogo wacha nikizungushe wee ni balaa nitasemwa hapo wiki nzima hadi nitampa.

Muda kidogo, alinambia kuna viwanja vinauzwa nitume hela anunue nikatuma, Leo hii nikiuliza naambiwa nenda Ili hali sijui hata ni wapi ila alisema ni bagamoyo, bado vicoba nishatuma hela sana na bado za miradi hewa hapo kati remind you muda huo bado niko chuo.

Nikitaka kufanya kitu nikimshirikisha ataomba hela nampa nikimdai naambiwa sitafanikiwa na nitadhulumiwa[emoji17]

Kuna siku nilimwambia kiutani tu kua nashukuru Mungu nimemaliza kadiploma salama sasa nitafute hela ya kwenda degree nilichojibiwa ni kua ungeendaje hiyo dip bila cheti cha form4 na ambayo nimekusomesha mm, jamani hata kunisapoti ya kinafki tu hapo chuo nimejisomesha mwenyewe sijui stationary kuumwa mitihani ada, kodi, nauli maana nimesoma mkoani

Nimefupisha mambo ni mengi sana, Mimi hadi sipendi kuishi nyumbani nakaaga mkoa mwingine kabisa kuepusha makelele ila bado nikiwa na huko nitaombwa hela ya marejesho na hazirudi!!!

Hapa juzi kati nilimtumia mzigo nikamwambia uza hela utakayoipata ni ya kwako huo mzigo faida yake ni laki5 Alhamdulillah aliuza, kuna kitambaa cha kushona nilimuomba mita moja na robo tu akanijibu sitaki we si mchoyo (kisa aliniomba hela ya marejesho nikamwambia sina watu bado hawajanilipa ngoja sikukuu ipite) nikamwambia mm mchoyo kisa nimekuambia sina? Sinimekutumia vitu na nimekupa hela ubaki nayo, akanijibu sikukuomba[emoji17]


Hivi ni mm tu au kuna wezangu tunapitia changamoto hii tupeane ushauri maana nikimfikiria sipati jibu neno asante kwake sijawahi kulisikia wala Mungu akubariki Mwanangu sijawahi

Kuna siku nipo chuo kipindi cha final akaniomba laki6 nikamwambia sina ila nitakupa laki3, kesho naanza final nikitoka jioni nitakutumia, nilikua na mitihani miwili wa saa2 na saa6, nilipigiwa simu balaa na bahati mbaya sikuweka silence ikabidi niitwe kuzima simu nikaizima remind you hata kuambiwa mtihani mwema sikuambiwa!!! Nilivyotoka nawasha simu tu nakutana na msg zake za lawama nimemzimia simu sitaki kumpa hiyo hela ningemwambia mapema wakati nilimwambia nitakutumia jioni maana aliniomba usiku na kwa wakala ni mbali nikasema nikimaliza paper najua itakua kwenye mida ya saa10 nitamtumia tu, ikawa kesi


Hivi Leo tu kuna kesi, kwangu kupewa radhi imekua kitu cha kawaida maana nishaambiwa maneno mengi mabaya,

Nimetype kwa uchungu sana ee Mungu anione jamani kwann napitia mitihani hii

Samahanini kwa mwandiko mbovu na essay ndefu (hapo sijaweka vitu vingi sana)

Maoni yako ni muhimu, nifanyaje au ww uliyepitia kama yangu haya ulifanyaje?

Kuna muda nilifikiria kuolewa ila sitaki kukurupuka
 
Kabila ?
Dini gani?
Chuo umesomea kitu gani?

Ukiotoa hizo detail itakuwa vizuri kwa kupata ushauri zaidi.
 
Kama Laana zingekua za kweli na zinamfikia mtu basi leo hii mimi ningekua naokota makopo njiani,nazurura nadondosha mate naongea mwenyewe njia nzima.

Mama yangu alishanitamkia maneno magumu na mfano wa 1 ambalo nalikumbuka mpaka na kesho aliniambiaga "wewe najuta hata kukuzaa ,natamani ile siku nakuzaa ningebana miguuu ufe kabisa"

asee mimi hamna laana sijatamkiwa na mama,ila nikwambie kitu mamilooo "kaza buti songa mbele" huyo si mama ako sasa huyo ni shetani anaemtumia mama.

Nakwambia hivyo kwa sababu yule mama angu aliyenilaani mimi,na mimi nilimwambiaga MUNGU kuanzia leo MUNGU nakwambia kwa mdomo wangu kuwa SINA MAMA nitajihesabu nina baba tu.

basi nili m cancel mama nikawa staki story zake wala kumsikia,Nilipambana nikasema siku 1 ataniona kwenye tv ama kunisikia kwenye radio ama kunisoma kwenye gazeti,kisha nika kaza zangu Mama yangu akawa MUNGU nikitaka kitu namwambia MUNGU nikitaka kudeka namdekea MUNGU yes ndio alikua mama yangu.

Baada ya miaka mi 5 siku 1 nipo ofisini natoka nafata gari nisepe zangu nilimuona mama yangu akinifata kwa Magoti akitokea getini akiingia huku analia unajua nilihisi ni movie ya kihindi au macho hayaoni,nilifikicha macho kuangalia vizuri yes ni Mama controla.

anakuja kwa magoti analia kwa uchungu "nisamehe mwanangu" hakua anatamka neno jingine zaidi ya "nisamehe mwanangu" asee unajua ile kum miss mama muda hujamuona then mnakuja onana mama anakulilia umsamehe.

Mimi ni nani nisimsamehe mama asee ile siku tulijaza Raia pale nnje maanaa nililia kama mtoto mama alilia kama mtoto,ni mzee mmoja alikua kutubeba na kutupeleka ndani na kuanza kazi ya kutunyamazisha.

Mama yakaisha na hadi leo nilipofika asee zile laana zilikua kama KICK ya kunipitisha,pamoja na changamoto zote ila nakwambia Sina siku nililala njaa,sina siku nilikosa nguo,sina siku nilikosa sadaka kanisani,Mungu alikua MAMA kwangu.

Huyo mama yako si yeye nakwambia tena si yeye mtambue shetani na hila zake kisha mwambie hakuwezi nakuhakikishia usiponasuka kwenye huo mtego wa MAMA umepotea. Kunja sura kaza mwendo songa mbele mwambie live mama "siwezi" mwambie "sina" mwambie "nipo vibaya" Akikulaani tu, KATA Mawasiliano nae.

Saa zingine kuwalinda watu tunaowapenda zaidi ni kukaa mbali nao.

Mama yupo tu hafi leo wala kesho so usimuendekeze hata kidogo,kaza buti asikuyumbishe hata kidogo atabaki kuwa mama na milele utamuheshimu ila ktk swala la yeye kukurudisha nyuma "USIKUBALI" kataa kwa maneno na vitendo.
 
Nimeshalia sana na kuomba Mungu kama kuna kitu chochote basi akipitishe mbali kati yetu lakini naona kadri ya siku zinavyoenda na mambo ndio yanazidi
Kuna wakati my x bf alisafiri nje kikazi na next wk inabidi nirudi chuo nikawa sina hela nikamuomba ela ya nauli tu NAULI TU ili nifikishe chuo na ningeirudisha ila akanijibu sina
Ikabidi niazime kwa mkaka wa jirani baadae x bf alivyorudi akanipa hela nikamrudishia huyo jirani
Hicho kitu kinaniumaga sana ina maana nisingepewa na jirani nisingerudi chuoni
 
Polee sana Binafsi kama nitahitaji Baraka za mzazi ntaziomba, ila huwa nashindwa sababu naamini yawezekana hataki kuniaminisha kwamba baraka zake ndo kila kitu. Namimi najiaminisha yawezekana ananiombea akiwa kajificha peke ake bila mimi kujua..nawe chukulia ivo mkuu
 
Sijawai kuwa ,kuona ,au kusikia mama mkandamizaji na asiye na huruma kwa mwanae/ wanae ,Kama maelezo yako jinsi yalivyo
Fanya uchunguzi wa kina sana kubaini kwa undani kama kwl huyo n mama yakao
Fanya juhudi pia ya kushirikisha baadhi ya ndgu zako wa karibu Sana juu ya suala hlo pia.
Jielekeze kwa muumba wako( swali Sana na swali kikweli kweli )
Tekeleza Yale unayoyaweza kwa mzazi wako kwa kiwango chako tu usipopaweza mweleze tu ,hakutakuwa na laana yoyote Kama itakuwa hvyo ,,,
Nataka kuandika vingi but nashindwa hebu tuanzie hapo ,mm tu npo hapa mama yangu sijamtumia hata Senti tano toka november lakn hachoki kunitafta na kuniombea katika mihangaiko yangu ,
Zingatia Sana sababu ya kwanza juu hapo[emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516][emoji3516]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama yako anamaumivu moyoni, ambayo yamesababisha akuone tofauti na wewe unavyotamani akuone. Lamuhimu ni kuchunguza, je anaishije na huyo mdogo wako? Je anafanya kwake, kama anavyofanya kwako? Then, jaribu kuongea na mdogo wako kuhusu unavyoishi na mama yako!..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante kwa maneno yako ya faraja
Hata mm nahisi sio yeye japo hizi tabia zake ni za muda mrefu na naona ni muendelezo

Mm kwasasa naishi mbali nae kabisa kuepusha vitu vingi baina yetu

Naona afadhali nilale njaa hata kwenye mateso ila sio kukaa nae pamoja maana hana maneno mazuri juu yangu kila kitu mm ni mbaya

Maneno makali tena makali haswa nishaambiwa ila nashukuru Mungu hadi leo hamna kibaya kilichonipata

September aliniomba laki4 nikampa mwezi huo huo akaniomba nauli aende mkoa x nikamwambia sina hela mimi mwenyewe nataka kusafiri kupeleka hii mizigo yangu

Akanambia kama mm nilikutoa kwenye uchi wangu huu hautafanikiwa nakuomba nauli unaninyima?? Wakati hapo nilimpa laki4 cash
Hapo napoenda kuna kula, bili za umeme bado nauli za kuzungushia vitu, kodi nimechanga na mwenzangu tukalipa ya mwaka mmoja

Maajabu nimefika vitu havikuchukua hata mwezi vikaisha na bado order ikawa kubwa ikabidi nirudi dar kufunga mzigo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…