Tunaosubiri namba E tukutane hapa

Gari 2 zimetengenzwa mwaka mmoja 2005 ila moja imesajailiwa T# CAB na nyingjne T# EAB ipi ni gari ya zamani? Naombeni ushauri.

Wengi wakishaamini mpya ni number E usijaribu na kupoteza nguvu kubisha, just go with the flow,
Mbongo ashatekwa akili, anaamini ikitumiwa na mzungu ni bora kuriko apaapa
 
Kwa taarifa tu,

Hata mwezi haujaisha toka tuingie DZA leo tuko T 600 DZD+

Bado tuna week nzima kuhitimisha mwezi toka DZA ianze.
Hizi ni zile gari 3000 zilizoshushwa mwezi uliopita na ile meli kubwa. So ni kama moto wa kifuu tu zitaanza kukwamia kwenye DZF. Zikifika F tunarudi kwenye trend ya herufi kukaa mwezi mzima.

Kutoka F mpaka Z ni takribani herufi 18 zitakazobaki ambapo zitanipa magari 16,164 ambapo itachukua zaidi ya miezi 8 kuzimaliza.....
 
Wewe jamaa hiyo hoja ya magari 16,164 ni kama imeshakukaa sana kichwani!😁.

Siyo mengi kama unavyofikiria wewe.

Kuna meli 4 za magari zinatia nanga mwezi May pale Dar port.👇


Hivi ninavyoandika leo 10th May kuna meli mbili za magari zipo hapo Dar port.
 
Kuna chuma imetia nanga leo na magari 4000+ imevunja tena rekodi ya kuingiza gari nyingi zaidi
 
Ni kawaida meli kuleta magari miaka nenda rudi but kutoboa magari 10k si kwa mwezi wala miezi mitatu ni zaidi ya 6
 
Ni kawaida meli kuleta magari miaka nenda rudi but kutoboa magari 10k si kwa mwezi wala miezi mitatu ni zaidi ya 6
Hata hoja yako haieleweki.
Kama ni kawaida meli kushusha magari, inakuwaje tena unatutisha kwamba yakiisha yale 3000 tutakwama kwenye DZF?

Meli si zitaendelea kushusha kama hiyo iliyoshusha 3000?
 
Kuna meli nyingine imeingia jana ina magari 4600 hivi
 
Kutoka F mpaka Z ni takribani herufi 18 zitakazobaki ambapo zitanipa magari 16,164 ambapo itachukua zaidi ya miezi 8 kuzimaliza.....
Ngoja nikupe mfano hai labda utaelewa uhalisia ulivyo.

Mimi nilisajili gari yangu 1_th September 2021 namba DXE.

Leo hii tupo 10th May 2022 na namba ni DZE.

TOKA September 2021 hadi leo May 2022 ni miezi tisa (9).

Kwa hiyo miezi 9 pekee tumesajili DXE-DXZ,DYA-DYZ na sasa DZA-DZE.

Hiyo miezi 8 ya DZF-DZZ wewe sijui unaitoa kwenye rejea ipi?
 
Sasa mkuu hapo herufi 6 zimechukua miezi 6. Je hizo 18 zilizobaki inakuaje?

Hii kasi ya April na May ni accumulation ya magari yaliyoagiziwa miezi mitatu iliyopita yamekuja in bulk isikuchanganye sana. Subiri mwaka uanze kusimamia katikati yani mwezi wa 6 uone hiyo kasi kama itakuwepo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…