Tunaosumbuliwa na vibarango Tukutane hapa

Pole ila dawa ya vibarango/mapunye ni rahisi sana ni hii

Chukua msusa(majani ya maboga) yasigine mpaka upate majimaji, weke kwenye hayo mapunye, hata mara 2 tu. Unafuta mpaka kovu.

Ulete mrejesho

Nashukuru ndugu nitajaribu
 
Kongole kwa kuchukua uamuzi wa kutibu, kiuhalisia vitu kama hivi wengi huchelewa kuvitibu for no reason, unaweza kuta mtu ana utango utango mwili mzima mpaka uso unabadilika anakuwa na mabaka kama chui ila anachukulia poa tu

Akijitahidi ni kujipaka mifuta ya breki kama juha ilhali kuna dawa bei nafuu tu inayoweza kutibu sharti ujitoe na ujipende

The same applies kwa fangasi, ugonjwa wa ngozi, mapunye etc. Haya magonjwa yakikupata tu yaitbu fasta usirembe
 
Paka maji ya matunda yanaitwa tula (Usukumani) au ndulele (Uchagani) mara 2 kwa siku baada ya kuoga. Unatafuta matula yaliyoiva unakata unakamulia maji yake kwenye hayo mapunye. Majimaji yakishakaukia pangusa mbegumbegu. Hii yenyewe ni kiboko ya mpaka yale mapunye yaliyoshindikana kwa dawa za kumeza.

Come and thank me later.
 

Mi vinanikera sana mwanzo nilikua navichukulia poa kalianza kamoja heee mara vikatapakaa nikakasirika
 

Haya madude nayapata wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…