Tunaotambikia Mizimu hasa mwisho wa mwaka tukutane hapa

Tunaotambikia Mizimu hasa mwisho wa mwaka tukutane hapa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Tawireeeeeeee.........

Hebu jamani kabla hatujaenda kutambika tujiulize Mizimu ni nani haswa?

Mizimu Ni watenda dhambi wa zamani.

Walikuwa wafiraji, wachawi, wauaji, waongo, wagomvi, wazinzi, wasengenyaji etc.

Sasa hawa mizimu tunaposumbuliwa na kushindwa tabia na wanetu, tunaenda kutambika kwao, eti watoto wanyooke. Watanyooka kweli?

Mizimu inataka pombe haitaki Pepsi, mizimi hii jamani. Mweeee.

Hebu tuendelee tu na kutambika
 
Wahaya hayo mambo ya mizimu tuliyaacha zamani sana
 
Wahaya hayo mambo ya mizimu tuliyaacha zamani sana
Acha kutusingizia wewe, wahaya hatujaacha asili yetu. Bado wenzio tunatambika na nyaruju zetu zipo na rubaya bado zipo nyingi. Mimi mwenyewe kwetu tunatambika kama kawaida na kuomba (kutela omushango). Ukipeleka kitu chochote nyumbani kama zawadi huwa kinatolewa kidogo kinawekwa huko madhabahuni (omurubaya/nyaruju) na mhusika anakuombea kwa mizimu ikubariki wewe uliyeleta rizki zako zizidi kufunguka na uzidi kufanikiwa na wakulinde na mabaya yote. Na kweli ukirudi mjini mambo yako yananyooka na mtu hawezi kuchezea au kukuroga.

Sema mtoa mada ameandika kama mtumwa wa dini za kuja (mental slave). Maana haiingii akilini kusema mababu zetu sisi waafrika walikuwa wafiraji, wezi, wachawi, wabakaji, n.k kwa hiyo mizimu (mababu zetu/ancestors) ni ya shetani, alafu mababu wa wazungu ni watakatifu[emoji57][emoji57]. Huu ni utumwa wa kiwango cha SGR. Na waafrika tusipojitambua tutatawaliwa sana na wazungu. Wazungu wenyewe wanatudharau kwa kuona tunadharau vya kwetu tunapapatikia vya kwao. Yaani hao mababu wa kizungu mnaoita watakatifu akina Joseph, Constantine, King James, n.k. Huyo mt. Constantine alikuwa muuaji mkubwa sana, aliua na kufunga watu wengi sana kwa kuwalazimisha kuukubali ukristo, huyo King James alikuwa shoga, n.k na ushahidi upo lakini wao mnawaita watakatifu. Ila mababu zetu ambao kwanza walikuwa watakatifu kimaadili na hamna ushaidi wa hayo mnayoyasema mnakuja kuwaita wafiraji. Very embarrassing[emoji17][emoji17]
 
Back
Top Bottom