Tunaotoka mkoa wa mkoa wa MARA njoo hapa

Tunaotoka mkoa wa mkoa wa MARA njoo hapa

Tunaotoka mkoa wa MARA

Kwa neema za Mwenyezi MUNGU wanajamii forum wote mu wazima wa afya

Jamii forum ina watu tofauti tofauti kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini

Leo naomba kwa wale wote tuliokaa ,tunaotoka au tunaoishi mkoa wa MARA tuambie ni changamoto gani unayokutana nayo kutoka kwa watu wa sehemu tofauti au uliyokutana nayo kwa sababu tu wewe ni kutoka mara (mkurya kama wengi wanavyodhani )

Au wewe ulipata changamoto gani kutoka kwa watu wa mara

......... Kuanza na mimi changamoto kubwa ni pale napojitambulisha kuwa ni mtu wa mara na mkurya watu kutamka hadharani kuwa Sisi wakurya ni KATILI na wanatuogopa huwa najisikia vibaya sana na sifa mbaya nyingne kama hizo

Karibu na wewe utwambie changamoto na ikiwezekana tuweze kubadirisha watu mitazamo yao kuhusu Sisi ::

Nb...si kila mtu kutoka mara ni mkurya
Ila mimi ni ndiyo

Sent using Jamii Forums mobile app

Na visu vyenu?
 
Wakurya achen wizi fanyen kazi

Vile vile achen kuzikimbia familia zenu na kukimbilia mikoa ya watu

Ukiangalia mkoa wa mara kwa sasa ndo mkoa masikin kuliko yote kanda ya ziwa, mkoa kwa sasa unazidiwa mbali sana na mikoa mipya ya usukuman kama geita na simiyu pia inazidiwa mbali sana na wilaya za kahama na maswa

Wakurya badiliken kuwen na akili achen ushamba

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kiac upo sahihi.,ila hapo kwenye neno *ushamba* cyo,...kwa kweli wakurya tunaweza kuchukuliwa km washamba ndiyo ila changamoto kubwa huku ni kuwa *mwamko wa elimu kwa jamii nyingi za kikurya ni haba sana*,kwa7bu wazee wetu wengi na ndugu wengine hawakusoma,hata waliofanikiwa kwenda shule hawakuhitimu,wali-quit,nan wa kuwa inspire vijana ss!!?[emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22]

Kuryan boy
From,Nyamwaqa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeishi Na wakurya mda mrefu sana!
Kwanza niwasifu kitu kimoja mna jali sana ndugu,
Ila MNA haya;
Ati mtoto akifeli shule au akiharibu chochote basi mwanaume anakuja kumgombeza mama nyumbani! Yaani utafikiri huyu mama alimtuma mtoto afeli......

*Kujifanya much know sana ! hapa Ndio mnameza rekodi!
*Wivu kwa wanawake wakati huo we mwanaume kutoka Na wanawake wengine basi Ndio unajiona wewe kidume!
*Kukeketa watoto wenu wa kike halafu mkifika mjini mnashoboka Na wanawake wa makabila mengine ambao hawajakeketwa Na kuona kama ulipotea vile kuoa aliyekeketwa!

[HASHTAG]#Nitaendelea[/HASHTAG]
Leta sifa za wanawake mkuu
 
Mie Mzanaki,kila nikijitambusha kuwa mi ni mzanaki bado huwa wananiita Mkurya ingawa Mama yangu ni Mkurya na mama yake mama ni Mjaluo!-kiufupi uzao wangu umetokana na makabila halisi ya mkoa wa mara.
Kwa kweli huku nilipo sifa moja kubwa ni kuwa Naogopeka hata mtu akija kuongea nami anongea kwa step
 
Mimi nilizuru mkoa flani na kujitambulisha kuwa ninatokea Serengeti. Watu wale niliojitambulisha kwao wakawa wanashangaa na kuniuliza, "serengeti si ni hifadhi ya WANYAMA???!"

Ilibidi nichukue muda wa kutosha kuwafahamisha kuhusu wilaya yetu pendwa ya Serengeti.

sent from servant of God
nimrcheka labda walijua na wewe ni mnyama!
 
Mimi nipo Mgango huku Musoma vijijini. Changamoto kubwa ninayoiona huku ni watu kuchukuliana wake. Unakuta mama mtu mzima ameacha familia kwake anatoka na kijana mdogo tu haooo hadi gesti. Sasa sijui huko wanafanya nini labda wanabadilishana mawazo ya kimaisha ila akili yangu inanituma kuhisi wanabambiana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni wapi hili halifanyiki chini ya jua mkuu. Hii ni asili ya binadamu woteeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe uzi huu ni wa Wakurya na si wa wana Mkoa wa Mara wote? Naomba msaada wenu wana Mara mliopo humu hivi kuna tofauti yoyote kati ya Wakurya na Wazanaki? Huku Kwetu nchini Rwanda Wazanaki wanakubalika na wanasifika sana hadi nashangaa wakati kiuhalisia Mkoa wa Mara umekuwa dominated hasa na Wakurya. Nitashukuru nikielimishwa juu ya hili ili nami niweze kuwaelimisha Wanyarwanda wenzangu hapa Mkoani Kwangu ninapoishi Gisenyi.
 
Mkuu watu wanaishi kwa mazoea na jambo likitokea mara linakuzwa sana tofauti na uharisia kabisa.

Na ukijaribu kuwambia ukweli watu wanaona unawadanganya

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu, tukio likitokea mara hata kama ni mtu kampiga mke wake hadi kupoteza fahamu litaripotiwa vyombo vyote vya habari ila likitokea tanga hauwezi kuskia.

sent from tekno ya shilingi elfu saba na mia tano.
 
Back
Top Bottom