Tunaowaita waheshimiwa nchini, tunawaita hivyo kwa kulazimishwa au kwa sababu wanafanya mambo yanayostahili waitwe hivyo?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Heshima ni neno la kawaida tu la kiswahili, lililotakona na neno la Kiarabu kuonyesha hadhi anayopewa mtu kama alama ya kuthaminiwa kwake. NI namna ya kumwonyeha mtu huyo kwamba utu wake una thamani, hasa kwa jinsi anavyoshughulika kuhusu watu wengine, kutia ndani matendo na kauli zake.

Kwa jinsi hiyo basi, heshima kuelekea mtu fulani sio jambo la kulazimishwa, ni jambo ambalo mtu hupata toka kwa watu wanaomthamini.

Sasa nikiangalia watu tunaowaita waheshimiwa hapa nchini, matendo yao, utu wao, kauli zao, jinsi wanavyoshughulikia watu wengine, kwa maoni yangu, naona labda ni 5% wanaostahili kuitwa waheshimiwa. Wengine wote wanaoitwa hiyo ni mapoyoyo watupu - wabinafsi, wenye kiburi, wenye dharau, waonevu, mafisadi, waongo, wauaji, wasiojali watu wengine, wenye kujiona miungu wadogo nk. Mengi ya haya wanayafanya mtu mmoja mmoja binafsi au kama kikundi. Wanapaswa kuona aibu kuitwa waheshimiwa, lakini nahisi hawana tena hisia ya aibu katika utu wao.

Sasa niambieni, kwa nini hawa watu tuwaite waheshimiwa? Mimi binafsi, neno mheshimiwa huwa silitamki kabisa kwa mtu yeyote Tanzania. Sitaki huo unafiki pale ninapoona mtu hastahili kuitwa mheshimiwa halafu mie nimuite mheshimiwa. Naepuka kwa kila namna mazingira yatakayonifanya nimwite mtu mheshimiwa.
 
Hakuna mzungu anaitwa Mheshimiwa lakini wanafanya mambo makubwa sn duniani, kutukuzwa huku ndiyo kumepumbaza sn watanzania sijui Mheshimiwa/Pro/Dr/CPA/Wakili msomi ni title za kijinga sn zinasababisha watu wanakuwa wavivu haswa.
 
Wakuu wa itifaki wakianza na hizo "mheshimiwa, Dr, Prof, CPA, Wakili msomi, Eng nk" ni kichefuchefu tu!
 
Heshima ni neno la kawaida tu la kiswahili, lililotakona na neno la Kiarabu kuonyesha hadhi anayopewa mtu kama alama ya kuthaminiwa kwake. NI namna ya kumwonyeha mtu huyo kwamba utu wake una thamani, hasa kwa jinsi anavyoshughulika kuhusu watu wengine, kutia ndani matendo na kauli zake.
Mfano nani?
 
Hakuna mzungu anaitwa Mheshimiwa lakini wanafanya mambo makubwa sn duniani, kutukuzwa huku ndiyo kumepumbaza sn watanzania sijui Mheshimiwa/Pro/Dr/CPA/Wakili msomi ni title za kijinga sn zinasababisha watu wanakuwa wavivu haswa.
Vice versa is true
 
Huwa sikubaliani na hoja zisizo na mifano. Na kama unaogopa kuwataja, kiherehere cha kuandika kitu unachokiogopa cha nini?
Utakuta na wewe unaitwa mheshimiwa? Basi mfano mzuri ni wewe. Maneno machafu lakini unataka watu wakuite mheshimiwa!
 
Ahahahahaha! Nawachukia sana wachangiaji wajinga wanaojiona wanajua. Siku nyingine ukileta hoja TOA MIFANO!!
 
Nawachukia sana wanaojiita waheshimiwa wakati hawana lolote la kufanya wastahilia kuitwa waheshimiwa.

Pia nawahurumia sana watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri ambao hata ukiwaambia ni asilimia 5% ya viongozi ndio wanastahili kuitwa waheshimiwa wengine wote ni mapoyoyo, bado wanataka uwatolee mfano wa watu wasiostahili kuitwa waheshimiwa. Ni kwamba watu wa hivyo ni wenye IQ ndogo sana kuwafanya waelewe jambo ni kupoteza muda wako. Siku hizi katika nchi nyingi madaktari wana uwezo wa kuona watu wa namna hii kabla hawajazaliwa, huwa wanawaambia wazazi, mtoto huyu atakuwa na tatizo la akili, mngependa tuiharibu hii mimba?

Shukuru mimba yako ilitungiwa Tanzania!
 
Heshima ni neno la kawaida tu la kiswahili, lililotakona na neno la Kiarabu kuonyesha hadhi anayopewa mtu kama alama ya kuthaminiwa kwake. NI namna ya kumwonyeha mtu huyo kwamba utu wake una thamani, hasa kwa jinsi anavyoshughulika kuhusu watu wengine, kutia ndani matendo na kauli zake.

Kwa jinsi hiyo basi, heshima kuelekea mtu fulani sio jambo la kulazimishwa, ni jambo ambalo mtu hupata toka kwa watu wanaomthamini.

Sasa nikiangalia watu tunaowaita waheshimiwa hapa nchini, matendo yao, utu wao, kauli zao, jinsi wanavyoshughulikia watu wengine, kwa maoni yangu, naona labda ni 5% wanaostahili kuitwa waheshimiwa. Wengine wote wanaoitwa hiyo ni mapoyoyo watupu - wabinafsi, wenye kiburi, wenye dharau, waonevu, mafisadi, waongo, wauaji, wasiojali watu wengine, wenye kujiona miungu wadogo nk. Mengi ya haya wanayafanya mtu mmoja mmoja binafsi au kama kikundi. Wanapaswa kuona aibu kuitwa waheshimiwa, lakini nahisi hawana tena hisia ya aibu katika utu wao.

Sasa niambieni, kwa nini hawa watu tuwaite waheshimiwa? Mimi binafsi, neno mheshimiwa huwa silitamki kabisa kwa mtu yeyote Tanzania. Sitaki huo unafiki pale ninapoona mtu hastahili kuitwa mheshimiwa halafu mie nimuite mheshimiwa. Naepuka kwa kila namna mazingira yatakayonifanya nimwite mtu mheshimiwa.
Nakuambia aliyewaloga Watanzania alaaniwe. Hii haina tofauti na ile mtu anaenda dukani au sokoni kununua kitu au bidhaa anatoa hela yake mwenyewe halafu anamwambia muuzaji naomba sukari kilo moja. Sasa unaomba ya nini wakati unatoa hela yako mwenyewe umeitafuta kwa jasho na damu
 
Back
Top Bottom