Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
hakuna haja ya kubabaika my friends ladies and gentlemen,Heshima ni neno la kawaida tu la kiswahili, lililotakona na neno la Kiarabu kuonyesha hadhi anayopewa mtu kama alama ya kuthaminiwa kwake. NI namna ya kumwonyeha mtu huyo kwamba utu wake una thamani, hasa kwa jinsi anavyoshughulika kuhusu watu wengine, kutia ndani matendo na kauli zake.
Kwa jinsi hiyo basi, heshima kuelekea mtu fulani sio jambo la kulazimishwa, ni jambo ambalo mtu hupata toka kwa watu wanaomthamini.
Sasa nikiangalia watu tunaowaita waheshimiwa hapa nchini, matendo yao, utu wao, kauli zao, jinsi wanavyoshughulikia watu wengine, kwa maoni yangu, naona labda ni 5% wanaostahili kuitwa waheshimiwa. Wengine wote wanaoitwa hiyo ni mapoyoyo watupu - wabinafsi, wenye kiburi, wenye dharau, waonevu, mafisadi, waongo, wauaji, wasiojali watu wengine, wenye kujiona miungu wadogo nk. Mengi ya haya wanayafanya mtu mmoja mmoja binafsi au kama kikundi. Wanapaswa kuona aibu kuitwa waheshimiwa, lakini nahisi hawana tena hisia ya aibu katika utu wao.
Sasa niambieni, kwa nini hawa watu tuwaite waheshimiwa? Mimi binafsi, neno mheshimiwa huwa silitamki kabisa kwa mtu yeyote Tanzania. Sitaki huo unafiki pale ninapoona mtu hastahili kuitwa mheshimiwa halafu mie nimuite mheshimiwa. Naepuka kwa kila namna mazingira yatakayonifanya nimwite mtu mheshimiwa.
heshima ni kitu cha bure na salamu haigombwi..
ni muhimu wanaostahili wapewe maua yao bila chuki binafsi wala kinyongo,
ni hiyari tu ndrugu zangu, hakuna haja ya kujenga chuki au kujiskia vibaya kwasabb ati fulani anaitwa muheshimiwa.
By the way,
kazi na maisha Lazima yaendelee bila mbambamba ya mtu yeyote 🐒