Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Kiuhalisia nishati safi ni nafuu kuliko kuni na mkaa. Gharama tunayonunulia mkaa na kuni siyo halisi. Hiyo siyo bei yake halisi. Gharama za kuukuza mti ni kubwa kuliko hiyo bei tunayonunulia.
Lakini pia bei ya mkaa na kuni hailingani na athari za ukame tutakazolipia huko mbele na tunazolipia sasa. Gharama ya kuni na mkaa hailingani na athari za ongezeko la joto tutakazolipia huko mbele.
Miti itaisha, tutakosa hewa safi. Tutasababisha ukame. Umeme utakatika kwa mabwawa yetu kupungua maji. Mifugo na wanyama pori watakufa kwa kukosa malisho na maji.
Hizo zote ni gharama tutakazolipia kwa kukata miti na misitu yetu kwaajili ya mkaa. Hiyo miti itaisha kama tusipo amua kuchukua hatua leo.
Kwa kumalizia tu: Miti ndiyo inatengeneza hewa ya oxygen. Miti ndiyo inayofyonza hewa ya ukaa. Tunapohamia kwenye nishati safi tunalinda miti yetu na misitu yetu.
Tunapaswa kuhamia kwenye nishati safi, haya mambo yote yanawezekana wewe ukikubali.