Tunapaswa kuwafundisha watoto wetu kuwajua maadui zetu

Tunapaswa kuwafundisha watoto wetu kuwajua maadui zetu

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,593
Habari wadau..!

Nimewaza sana kwa nn baadhi ya wazazi hawawafundishi watoto wao kuwajua maadui zao.

Binafsi naona kuna umuhimu sana wa kumfundisha mtoto awajue maadui na marafiki zako ,ili kesho asije kupata matatizo kwa kutokujua adui za baba yake.

Kama utamfahamisha mtoto kuwajua marafiki wako wa kweli hii itasaidia pindi anapopata tatizo au familia inapopata tatizo pindi wewe haupo duniani atajua yupi wa kumuamini na kumkimbilia kuomba msaada.
 
Kuna babu yangu yuko SA ana rafiki yake alifiwa na mke wake zamani. Miaka ya karibuni akaoa mke mdogo mdogo kamtoa Bongo kampeleka SA. Wakiwa na miaka michache na mtoto mmoja pekee mzee akafa kwa corona, kipindi kile usafiri tabu kuna lockdown sikuwahi amini mwili wa marehemu unasafirishwa kwa milioni zaidi ya 20 aisee.

Babu aliwasaidia sana ile familia, wanae wakubwa wa mke wa kwanza wako nchi mbalimbali ila zote zilikuwa hazina usafiri wa anga muda huo. Wachache walifika msibani. Rafiki wa marehemu alijua mambo yake mengi kuliko watoto wake wa tutafute mali zetu wenyewe
 
Kwasababu uadui ni sifa ya maana na unadumu...

Dah, waafrika aisee sijui shida yetu ni nini..
Hate harm who Carrie's it...

Sasa maadui zako wanahusiana vipi na kizazi chako? dunian maisha yanapita upes kuliko unavyoweza kufikiri.
Spread love mzee not hate
 
Maadui zake, hawawezi kua maadui za watoto zako pia...
 
Back
Top Bottom