Kuna babu yangu yuko SA ana rafiki yake alifiwa na mke wake zamani. Miaka ya karibuni akaoa mke mdogo mdogo kamtoa Bongo kampeleka SA. Wakiwa na miaka michache na mtoto mmoja pekee mzee akafa kwa corona, kipindi kile usafiri tabu kuna lockdown sikuwahi amini mwili wa marehemu unasafirishwa kwa milioni zaidi ya 20 aisee.
Babu aliwasaidia sana ile familia, wanae wakubwa wa mke wa kwanza wako nchi mbalimbali ila zote zilikuwa hazina usafiri wa anga muda huo. Wachache walifika msibani. Rafiki wa marehemu alijua mambo yake mengi kuliko watoto wake wa tutafute mali zetu wenyewe