Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
TUNAPOENDA KUANZA MWEZI JUNE; AYA HII IKUSAIDIE, IWE MUONGOZO KWAKO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Isaya 48:17
Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
Nisikie!
Mungu aliyekuumba, ndiye unayetakiwa umuamini. Kumwamini Mungu ni kutomtilia Shaka yoyote.
Mungu aliyekuumba ndiye Mkombozi wako.
Kwa sisi watibeli, hatuhitaji msaada Wala ukombozi Kwa yeyote isipokuwa Mungu. Msaada wowote usiotoka Kwa aliyekuumba hauna baraka. Hivyo hautakuwa na furaha.
TAIKON Master ninafalsafa isemayo; kama Mungu hatanisaidia hakuna mwingine wakufanya hivyo.
Falsafa hii ukiichukua itakusaidia sana.
Mungu ndiye akupaye watu sahihi wakukupa msaada Kwa wakati sahihi.
Elewa katika kanuni ya vita, Your enemy waits until your next step become your last. Kumaanisha Nini?
Wakati mwingine msaada unaweza kuuona ni ukombozi wako. Ukapanga na mipango ya hatua zinazofuata kumbe hatua inayofuata ndio mwisho wako adui anakumaliza.
Mungu aliyekuumba awe ndiye Mwalimu wako anayekufundisha..
Wanasema Baba ndiye Mwalimu wako.
Usikubali kufundishwa na Walimu wengine. Jitahidi yule aliyekuumba awe Mwalimu wako Ili upate Faida.
Faida ya kufundishwa na Mungu utaipata mwishoni, kwenye hatma Yako. Wengi wanaomba wawe na Mwisho Mwema.
Mwisho, kwenye Maisha kuna Njia nyingi. Lakini sio njia zote za wewe kuzifuata. Ipo njia Yako.
Kama Sayari na nyota zilivyo na njia zake Kila kimoja kikipita katika njia yake bila kukosea. Ndivyo na wewe unanjia Yako.
Mungu pekee aliyekuumba ndiye anayejua njia sahihi unayotakiwa kuipita.
Ndio maana unatakiwa kumfanya awe Kiongozi wako. Ili upite katika njia ikupasayo kuifuata.
Njia ambayo itakukutanisha na baraka zako na kukuepusha na mikosi.
Njia ambayo itakukutanisha na Mke Mwema wa kukupa raha na kuwa Mama Bora Kwa wanao.
Njia ambayo itakukutanisha na mume Bora na sio wanaume watakaokuzalisha na kukugeuza single mother na kufanya heshima Yako na jina lako kushushwa thamani.
Njia ambayo utaipata kazi itakayokupa furaha.
Kama Mungu hatakusaidia no one Will.
Taikon Master katika Ukuhani wa Kifalme.
Mungu akupe hekima ya kuyaelewa Maisha na kusudi lake.
Mungu akupe roho ya kuushinda uovu Ili uwe na moyo safi.
Nawatakia MWEZI JUNE Mwema.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam