Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Tumekumbwa gonjwa hatari lenye kuuwa hadi 90% ya wahanga.

Sisi kwa tunachoita kuondoa taharuki tumependelea kuliita Marburg badala ya jina lake linalofahamika uswahilini, yaani Ebola.

View attachment 2562190

"Kwamba tumependa kutoliita koleo kwa jina lake."

Maajabu ya Mussa.

Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?

Katika kinachoitwa kuepuka taharuki gonjwa halipewi umuhimu wala coverage yoyote ya maana kwenye media zetu. Kwetu Simba au Yanga kwenda robo fainali ni habari kubwa, Lakini si gonjwa hili.

Maisha yanaendelea kama vile kila kitu ni sawa.

Ya nini kutoambiana ukweli wote tukajipanga kukabiliana nalo ana kwa ana kama nchi?

Kwenye tahadhali zilizotolewa na wizara katika namna za kujikinga, kutogusana nayo imo. Inawezekana namna gani kwenye maisha yetu ya kawaida watu kutokugusana masokoni, magulioni, mashuleni, makanisani, misikitini, kwenye mabasi au kwenye madala dala?

Ebola si ya maji tiririka, barakoa, michaichai, matango pori wala upigaji nyungu.

Walioyasikia ya kwetu wameshtuka kuliko sisi wakati sisi tukichukulia poa. Dhidi ya gonjwa hili dunia tayari inatunyanyapaa.

Angalia Rwanda, The New Times - Rwanda on Marburg alert after Tanzania outbreak

Angalia mabeberu, BBC News - Ebola-like Marburg virus kills five people in Tanzania

Coverage zao ni makini na kamilifu (extensive and focussed). Kwetu wenge la awamu ile na njama za mabeberu bado lingalipo.

Kwanini watu wasiambiwe ukweli wote kukiwa kungali mapema? Ya nini kujidanganya?

Magonjwa haya si vita (vya kiuchumi). Ebola si corona ambayo kuuwa kwake kulikuwa hadi 2%. Hiyo hata ikihusianisha uzee na uwepo wa magonjwa mengine pia.

Kwa hakika kwenye ugonjwa huu tusipoamka mapema, usanii wetu uliozoeleka utatuumbua.

Naomba kuuliza; somo la Biology na Chemistry ulipata pass gani Form Four?
Nimeona nianzie hapo nisijekuwa nabishana na mtu asiyekuwa hata na msingi wa Elimu husika.
Labda nikupe mfano rahisi; Typhoid ina dalili zinazofanana na ugonjwa wa malaria kama 85%
Kwa hiyo Mgonjwa akiwa na Typhoid, tuseme tu ana Malaria kwa sababu ndio watu wanaihitaji kusikia?
 
Ebola na Marburg vyote hupimwa kwa ELISA na antibody titer test
Ngoja niweke tu comment ya Isanga family wa pale Mwanjelwa Mbeya [emoji1787]
Screenshot_20230322-233720.jpg
 
Kazi yangu ni kushughulika na makanjanja ya mitandaoni kama brazaj

Nimejiajiri kwenye hii kazi, na ninaifurahia sana.

Rest assured, nitakufuata kila utakapokwenda.

Na usiponijibu ndio vizuri sana, lakini mimi nitaendelea kujibu kila upotofu unaouandika humu. Nitakujibu usiku na mchana kwa faida ya wengine.
Duh[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Soma mada usirukie treni kwa mbele. Uswahilini hakuna google. Maisha yako uswahilini siyo kwenye google wala mitandaoni.

Rwanda on Marburg alert after Tanzania outbreak

Ebola-like Marburg virus kills five people in Tanzania
Nimesoma taarifa zote ulizoweka link sijaona mahali hao jamaa wamesema huu mlipuko uliotokea Bukoba ni Ebola siyo Marbug. Nimeona wote wamenukuu WHO wamesifia hatua zilizo chukuliwa na serikali ya Tanzania kudhibiti mlipuko.
Wamesema kumekuwa na uwazi katika hatua zote za kutambua aina ya ugonjwa na namna ya kudhibiti mlipuko.

Nashauri tusitoe hisia zetu bila ushahidi wa kisayansi au kitakwimu rasmi juu ya mambo nyeti kama haya.
 
Anachanganya ebola wana present Sawa na Marburg ingawa ebola ni more virulence

Cha muhimu mpe Elimu aelewe ndicho nlichofanya

Serikali haina sababu ya kuficha aisee kwamba Ile ni ebola no haina hio sababu kabisa

Especially Serikali hii ya sasa
Hapa sasa nimekuelewa.


Huyu Braza J analazimisha itangazwe kuwa ni Ebola ili kuwaconfuse watu..
Lengo lake ni kwenda tu kinyume na serikali bila kujali serikali ipo sawa au haipo sawa.
Serikali ikikaa upande huu,yeye anakaa huu.

Nadhani Braza angejikita tu kwenye mada nyingine ambazo ana utaalam nazo.
 
Naona upo na ndugu yako bichwa komwe[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nimeanza kusoma
Mpuuzi tu...

I love someone who challenges my brain kama mtoa Mada

Lakini sio mtu ameshiba maharage yake huko tandika anaanza kudharau watu Humu hio Hapana kwakweli [emoji23]
 
Hapa sasa nimekuelewa.


Huyu Braza J analazimisha itangazwe kuwa ni Ebola ili kuwaconfuse watu..
Lengo lake ni kwenda tu kinyume na serikali bila kujali serikali ipo sawa au haipo sawa.
Serikali ilikaa upande huu,yeye anakaa huu.

Nadhani Braza angejikita tu kwenye mada nyingine ambazo ana utaalam nazo.
Yeye itakua kaona Serikali labda imeamua ifiche kitu( labda kutokana na historia ya Serikali iliyopita kuficha mambo ya corona) asichofahamu ni kwamba hauwezi kuficha sababu ukificha unaiweka Dunia nzima hatarini hata nchi za jirani unaziweka hatarini

Kwenye tafiti kama hizi za magonjwa kama haya WHO huwa makini Sana na wao pia hutuma wataalamu wao

Kuthibitisha hili ingawa bado sijaangalia ila nenda website ya WHO lazima washatoa tangazo kwamba Tanzania eneo flani Kuna Marburg watalii, wasafiri kuweni makini
 
Yeye itakua kaona Serikali labda imeamua ifiche kitu( labda kutokana na historia ya Serikali iliyopita kuficha mambo ya corona) asichofahamu ni kwamba hauwezi kuficha sababu ukificha unaiweka Dunia nzima hatarini hata nchi za jirani unaziweka hatarini

Kwenye tafiti kama hizi za magonjwa kama haya WHO huwa makini Sana na wao pia hutuma wataalamu wao

Kuthibitisha hili ingawa bado sijaangalia ila nenda website ya WHO lazima washatoa tangazo kwamba Tanzania eneo flani Kuna Marburg watalii, wasafiri kuweni makini
Mimi nipo upande wa serikali ilichosema
Huyu brazaJ asitutoe kwenye reli🤣
Kama vipi atupe kwanza vipimo vyake
Na si kuguess tu anachotaka kwa kutumia mambo yaliyopita.
 
Kumbe magufulism bado inalitafuna taifa
Bado tupo tupo sana:

.. Neno taharuki lipo kazini tena
.. bila shaka vita vya kiuchumi ni vile vile
.. ID za msaada zimeanza kuchomoza
.. huu tunaambiwa jina jipya siyo Ebola kule tuliambiwa kalikuwa ka upepo
.. mabingwa wetu wa matango pori na nyungu hawajachomoza labda mitishamba ingali inatokota
.. taarifa kuhusiana na ugonjwa, ni nyara za serikali
.. nk nk.

Hali ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom