Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Hawataki kusema ebola wanataka kusema Marburg Ili atakaye hoji waseme google. Eti kwamba hilo ni jina jingine wakiita "kisawe."

Cc: Ruble

Kaka una uhakika ni ebola? i mean ww ni mtaalam wa afya ambae uko eneo husika na una uzoefu wa magonjwa ya mlipuko?
 
Nimechelewa kuuona huu uzi.

Ila nilipofungua kabla sijasoma nikakuta mwandishi Ni brazaj nikatabasamu Kisha nikaanza kusoma na kupitia maoni ya watu.

Mkuu,

Hawa ndiyo watu wanaokimbilia ajali na kuwahi kureport kwenye social media "watu 20 wamekufa papo hapo kwenye ajali ya basi"

Siku serikali ikitangaza kwenye ile ajali walikufa watu 7 na majeruhi 25 utamsikia Tena anakuja na nyuzi kila platform na vichwa vya habari "serikali inapata faida gani kuficha vifo vya waliokufa kwenye ajali ya basi?" .Unaishia kumsamehe mtu Kama huyu kwani tatizo lake Ni moja tu; amekosa exposure ya mambo ya afya. Hakujua kuwa Kuna ambao walizimia wakazinduka baadae na Kuna ambao walifanyiwa cardio pulmonary resuscitation (CPR) na huduma zingine za 1st aid na kimatibabu kisha wakaamka nankuendela na maisha.Ila Hawa watu wakiona damu na mtu yupo kimya anahesabiwa Kama amekufa na kufunikwa khanga hadi kichwani.

Kwa matukio Kama haya Unaishia kujiuliza Sasa serikali inapata faida gani ikificha vifo vya ajali?

Serikali inapata faida gani ikificha ugonjwa eti wananchi wasijue huu ugonjwa ni Ebola?

Je, Serikali ikisema ukweli kuwa huu ugonjwa ni Ebola si ndiyo wananchi watachukua taadhari kwa umakini zaidi?

Mara ya mwisho nakumbuka ilikuwa mwezi February nilipoona video kwenye hospital ya serikali inayosisitiza tahadhari na njia za kujikinga dhidi ya Ebola na Nini Cha kufanya endapo utahisi kuna mgonjwa wa Ebola kwenye familia yako. Hii ilikuwa ni tangu ulipoibuka huu ugonjwa wa ebola kule Congo. Sasa kwa nini leo ionekane serikali inaficha wananchi wasijue ni Ebola. Kwa taaruki ipi? Kwa kuogopa nini?

Nimeshawahi kuingia kwenye majibizano na mleta mada juu ya mambo ya afya hasa suala la Corona na chanjo na Hakuna hoja ya maana aliyoongea zaidi ya siasa. brazaj ,mimi nadhani endelea kujikita na maswala ya siasa,huku kwenye afya upo shallow,achana na contents na links za kuokoteza Kisha unashusha threads. Yes utapa likes na replies nyingi za kukusuport lakini wewe ni mweupe hujui chochote kuhusu afya. Huku omba msada na siyo vinginevyo.

Mkuu nilitaka kukupuuza lakini nikadhani sitakuwa nimekutendea haki. Ikizingatiwa waungwana wanasema elimu haina mwisho.

Kwamba badala ya hoja umetokea kumshambulia mleta mada? Tena bila ya msingi wowote ila kwa perception zako tu?

"Kwani wewe ni malaika, Mungu, Jini au shetani?"

Kwamba:

________
"Nimechelewa kuuona huu uzi.

Ila nilipofungua kabla sijasoma nikakuta mwandishi Ni brazaj nikatabasamu Kisha nikaanza kusoma na kupitia maoni ya watu."

----------

Na hivyo ndiyo sasa unataka ueleweke kuwa wewe ni mwerevu sana?

"Huo si ndiyo wenda wazimu wenyewe sasa? Au?"

Kwamba unasema ulikuwa biased na preconceived kabla ya yote? Hadi hapo bado ungependa kuchukuliwa seriously ndugu? Labda na mamburula wenzio tu.

Kumbe huenda hata mada hukuisoma wala kuelewa ila ukaanza ku comment ukilenga kumshambulia mleta mada kwa vyovyote na kwa lolote? Yaani alimradi itakavyokupendeza wewe?

"Hiki si ni kituko cha kufungia mwaka kabisa?"

Huku sasa si ndiko kule kukimbilia kwenu kuripoti tukio la ajali kwenye social media unakokuongelea? Tena mkionyesha na mapicha picha mliyokuwa mkipiga badala ya kuwasaidia wahanga ili mlete mnachoita unyunyu?

Hamna uchungu wala hisia zozote za kiutu. Ni kama ilivyoainishwa kwenye mada na hata ilivyokuwa kwenye corona.

Ona japo aibu kidogo ndugu kwa kutaka kuyahamishia mapungufu yako kwa watu wengine ambao hata haufahamiani nao.

Kwamba uliwahi kutofautiana nami kimawazo? Wajameni, hilo linahusika vipi hapa na mlipuko wa gonjwa hili hatari Kagera huko?

"Wanatofautiana watoto mapacha, sembuse miye na wewe Neema?" -- Chidumule.

Si angalau ungekuwa umeweka basi hapa japo tulichokuwa tumetofautiana ili kuhalalisha tuhuma zako kwangu na kuwaacha wengine ikiwapendeza kujiridhisha?

Haya mengine kwamba uliwahi kuona video ya serikali nyuma huko ya namma ya kujikinga na ebola? Kwani huko nyuma uliwahi kuona taarifa hata moja ya kujikinga na Marburg? Au unarejea kuniunga mkono kwenye mada yangu bila kujua?

"Mengine (kama yalivyo) nimekupuuza, kwa maana ya nini kukimbizana na mwenda wazimu?"

Nimalizie kwa kukupa angalizo tokea kwenye mila na desturi za JF:

"Huku tunako thubutu kuongea waziwazi huwa tunapambana na mada si mleta mada."

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Nitapingana na ww, dunia imebadilika sana na info za magonjwa mengi ziko online.
accessible na watu wote duniani. Difference is experience ya ku deal na jambo lenyewe

Hapa unapingana na miye kuhusu nini ndugu?
 
Ni changamoto kidogo kujadiliana naye,maana anakuja na wazo lake ambalo si sahihi,afu analazimisha wote mkubaliane naye,akikosolewa na kujiona amekosea anapindisha hoja ionekane kwamba yeye yupo sahihi hata kwa kukataa hoja zake mwenyewe alizoandika awali.Ni mbishi kwa lengo la kushinda sio kueleweshana.

Kulikuwa na post #289 iliyo summarize mliyoyakimbia kimya kimya.

Kwa tija ipi kuikimbia mada ili kumsakama mleta mada tena kwa allegations zenu ambazo hata ni very much unfounded?
 
Unayasomaga wapi hayo ndugu? Mbona wengine hatuyaonagi?

Ama kweli JF raha sana 🤣🤣
Hivi nchi iitangaze Marburg kuificha Ebola kwa faida gani, si yote ni magonjwa mabaya yanayoambukizwa kwa namna sawa na hayana dawa? Unakuwa unaepusha nini ukiyataja maambukizi ya Ebola kama Marburg? Huoni umekuwa mjuaji katika hili? Na after all ukisha declare uwepo wa magonjwa ya namna hii si issue inakuwa handled kwa kushirikiana na WHO! Kwahiyo kwa mawazo yako WHO nao hawajagundua kwamba kilochopo Bukoba ni Ebola sio Marburg?
Kwani Bavicha mna tatizo gani kiasili?

 
Mkuu umetoa taadhari nzuri... Ila jaribu kujielimisha zaidi juu ya magonjwa mbali mbali, watu waliosomea afya wanakushangaa, unapotaka kuaminisha Ebola ni Marburg... kisa msamiati Marburg kwenye kiswahili haupo,.... Sasa Kama ugonjwa wenyewe haujawahi tokea kabla uswahilini watu wangejuaje huo msamiati....... Kiufupi Mimi Neno Marburg nimekutana nalo 2007 wakati nasomea afya, magonjwa mengine yanayofanana na Marburg ni Ebola, chikungunya na dengue yote haya yaitwa hemorrhagic disease , hivyo neno Marburg sio jipya ....

Uko nje ya mada mkuu.

Wapi nimesema Ebola ni Marburg? Wapi nimesema Marburg ni neno jipya?

"Kwamba wakati Unasomea afya siyo ..."🤣🤣

Huko tulishaondoka muda mkuu.
 
Watu wa siasa Hawa,wasikusumbue kichwa mkuu.

Hawa ndiyo wakishika madaraka wanawalazimisha wataalamu waseme wanavyofeel wao na siyo Hali halisi ilivyo. Na Mara nyingi hawapendi kushindwa au kuonekana hawaju

Hawa wakiwahi kwenye tukio la ajali ndiyo umfunika khanga Hadi kichwani kila mtu ambae amelala kimya na kuandika mtandaoni RIP. Serikali ikija kutangaza idadi ya vifo Ni watu watatu wanaibuka Tena kwa nguvu mishipa ya shingo umesimama " serikali iache kudanganya,nimeshuhudia kwa macho yangu wamekufa watu 13 tena Mimi nilikuwa nimeshiriki kuwasitiri" Kumbe Kuna mambo ya kitaalamu yalifanyika Kama CPR na Kuna ambao walizimia tu wakaamka baadae.

Hawa watu hawapendi kuwasikiliza wataalamu wanasema nini. Wao wanashikilia misimamo isiyo na mantiki na kucreate attention mitandaoni.

"serikali ijitokeze kusemaa ukweli kwamba huu ugonjwa ni Ebola na si kufichaficha,mbona nchi fulani jirani wamenyooka na kutoa tahadhari kwa raia wao"

"serikali iache kulishughulikia hili Jambo Kama enzi ya Corona. Jiwe hayupo,Sasa kwa Nini inaendesha mambo ya hovyo Kama enzi zile za Corona?"

Kumbe ulikuwa na bandiko jingine jeupe hapa?

#344 itakuwa imejibu pamoja na hili ndani yake.
 
Rejea title ya maada yako... Na comments zako za mwanzo mwanzo wa thread..

Unajua maana ya title mjomba? Unajua Mod wana mamlaka hata ya kubadili titles hizi ?

Kwa Taarifa yako mods tagged kwenye post hii waliikarabati title hiyo kuwa hivyo unavyoiona.

Hata hivyo hakuna kilicho haribika kwani maelezo kamili kuhusu hoja huwa yapo yote kwenye mada, siyo kwenye title.

Comments zangu za mwanzo mwanzo ni zipi?

"Weka muziki wacha maneno!"

Ninakazia:

"Wapi nimesema ni ebola ndugu?"
 
Tumekumbwa gonjwa hatari lenye kuuwa hadi 90% ya wahanga.

Sisi kwa tunachoita kuondoa taharuki tumependelea kuliita Marburg badala ya jina lake linalofahamika uswahilini, yaani Ebola.

View attachment 2562190

"Kwamba tumependa kutoliita koleo kwa jina lake."

Maajabu ya Mussa.

Tangu lini uswahilini neno Marburg likafahamika? Kwani gonjwa hili lilipokuwa Congo, Uganda, Guinea, Gabon, Sierra Leone au Liberia tuliwahi liita Marburg?

Katika kinachoitwa kuepuka taharuki gonjwa halipewi umuhimu wala coverage yoyote ya maana kwenye media zetu. Kwetu Simba au Yanga kwenda robo fainali ni habari kubwa, Lakini si gonjwa hili.

Maisha yanaendelea kama vile kila kitu ni sawa.

Ya nini kutoambiana ukweli wote tukajipanga kukabiliana nalo ana kwa ana kama nchi?

Kwenye tahadhali zilizotolewa na wizara katika namna za kujikinga, kutogusana nayo imo. Inawezekana namna gani kwenye maisha yetu ya kawaida watu kutokugusana masokoni, magulioni, mashuleni, makanisani, misikitini, kwenye mabasi au kwenye madala dala?

Ebola si ya maji tiririka, barakoa, michaichai, matango pori wala upigaji nyungu.

Walioyasikia ya kwetu wameshtuka kuliko sisi wakati sisi tukichukulia poa. Dhidi ya gonjwa hili dunia tayari inatunyanyapaa.

Angalia Rwanda, The New Times - Rwanda on Marburg alert after Tanzania outbreak

Angalia mabeberu, BBC News - Ebola-like Marburg virus kills five people in Tanzania

Coverage zao ni makini na kamilifu (extensive and focussed). Kwetu wenge la awamu ile na njama za mabeberu bado lingalipo.

Kwanini watu wasiambiwe ukweli wote kukiwa kungali mapema? Ya nini kujidanganya?

Magonjwa haya si vita (vya kiuchumi). Ebola si corona ambayo kuuwa kwake kulikuwa hadi 2%. Hiyo hata ikihusianisha uzee na uwepo wa magonjwa mengine pia.

Kwa hakika kwenye ugonjwa huu tusipoamka mapema, usanii wetu uliozoeleka utatuumbua.
Mwenyewe unajiona umeandiiika hadi bhaas. Yaani Serikali ifiche ugonjwa kwa maslahi ya nani!? Hivi Ebola unaijua unaisikia, tema mate chini usiombe hilo gonjwa likaitokea katika jamii yetu.

Ugonjwa ulioripotiwa Kagera ni wa Maburg na ni wa virusi wa jamii ile ile ya Ebola lakini wa ukoo tofauti. Huu hauna ukali ule wa Ebola, tahadhari zikichukuliwa vizuri waathirika wake huweza kupona hata kwa 100% na maambukizi yake yanawweza kudhibitiwa kwa muda mfupi tofauti na wa Ebola yenyewe.

Tuwe na utamaduni wa kuheshimu maelekezo ya Serikali hasa inapotokea suala la Magonjwa. Ugonjwa ukifichwa fichwa maana yake kutakuwa na athari kubwa sana na za kijamii na kiuchumi ambapo pamoja na wananchi kuathirika, Nchi kama Nchi itaathirika pakubwa zaidi kwa kuwa itashindwa hata kupata misaada kutoka mashirika ya Kimataifa katika kuudhibiti ugonjwa. So hakuna sababu yoyote ya sreikali kuficha linapotokea janga kama hilo.

Wakati mwingine kabla hujatoka hadharani na kutupa hoja yako, jaribu kujiridhisha kwa kufanya utafiti kidogo
 
Ebola na Marburg kisayansi (yaani in scientific details) ni magonjwa mawili tofauti. Malaria na Plasmodium kisayansi ni vitu viwili tofauti. Uswahilini plasmodium haina maana yoyote ila malaria.

"Marburg and Ebola viruses are filamentous filoviruses that are distinct from each other but that cause clinically similar diseases characterized by hemorrhagic fevers and capillary leakage. Ebola virus infection is slightly more virulent than Marburg virus infection."

Ninakazia uswahilini neno Marburg halina maana yoyote ila ebola linalofahamika kuhusiana na huu ugonjwa.

Ya nini kujikinga mvua chini ya mwembe wakati nyumba za bati zipo?

Zingatia ugonjwa huu umekuwapo katika mataifa kadhaa kabla. Ni kwa mara hii tu Tanzania imeuita Marburg kwa watanzania. Kulikoni?

Mwongozo wako tafadhali.
Hata hao Plasmodium wako tofauti. Ukishikwa na malaria iliyyosababishwa na Plasmodium malariae, vivax au falsparium unakutana na mziki tofauti kabisa. Mziki wa Ebola ni moto wa kuotea mbali, hawa Maburgs wana tabia zinazofanana kwa mbali na ebola lakini hawatishi. Japo wakikupata bila usaidizi wa kitabibu wanakutoa roho ndani ya muda mfupi.
 
Ugonjwa huu si wa kwanza kwetu. Umekuwapo mataifa mengine. Ni mjinga kweli kweli anayeweza kuamini kuwa hadi sasa hakuna taarifa mpya eti kwamba ni wagonjwa wale 8 na vifo vile 5 vilivyotokea na tatizo liliishia hapo.
Tatizo lako ni kwamba unadandia taaluma za watu. Ungeijua epidemiolojia ya Maburg na Ebola wala usingeendeleza hii hoja. Jambo kama hulijui usilikomalie kwa hoja za hisia, ulizia kwa wanaofahamu wakupe ufafanuzi ndg.
 
Mwenyewe unajiona umeandiiika hadi bhaas. Yaani Serikali ifiche ugonjwa kwa maslahi ya nani!? Hivi Ebola unaijua unaisikia, tema mate chini usiombe hilo gonjwa likaitokea katika jamii yetu.

Ugonjwa ulioripotiwa Kagera ni wa Maburg na ni wa virusi wa jamii ile ile ya Ebola lakini wa ukoo tofauti. Huu hauna ukali ule wa Ebola, tahadhari zikichukuliwa vizuri waathirika wake huweza kupona hata kwa 100% na maambukizi yake yanawweza kudhibitiwa kwa muda mfupi tofauti na wa Ebola yenyewe.

Tuwe na utamaduni wa kuheshimu maelekezo ya Serikali hasa inapotokea suala la Magonjwa. Ugonjwa ukifichwa fichwa maana yake kutakuwa na athari kubwa sana na za kijamii na kiuchumi ambapo pamoja na wananchi kuathirika, Nchi kama Nchi itaathirika pakubwa zaidi kwa kuwa itashindwa hata kupata misaada kutoka mashirika ya Kimataifa katika kuudhibiti ugonjwa. So hakuna sababu yoyote ya sreikali kuficha linapotokea janga kama hilo.

Wakati mwingine kabla hujatoka hadharani na kutupa hoja yako, jaribu kujiridhisha kwa kufanya utafiti kidogo

Wapi unaposoma ya kuwa nimeona nimeandika mpaka bhaaas? Au wewe ndiyo unaona umeandika mpaka bhaaas?

Hiiiiiii bagosha!

Povu la nini ndugu? Kwani wewe ni katika wakusanya sample za mbuzi, oil na mapapai kupimwa corona kwenye zama za giza?

Kwani ni mgeni wewe kwenye usugu wa ficha ficha magonjwa zetu?

Au ndiyo kuwasili kutokea sayari nyingine ndugu?
 
Tatizo lako ni kwamba unadandia taaluma za watu. Ungeijua epidemiolojia ya Maburg na Ebola wala usingeendeleza hii hoja. Jambo kama hulijui usilikomalie kwa hoja za hisia, ulizia kwa wanaofahamu wakupe ufafanuzi ndg.

Tatizo lako ni kuwa unaona huna tatizo. Tufanye wewe uko vizuri. Kwani kuna taabu hapo ndugu?
 
Ni bahati mbaya sana kuwa kama nchi tumekumbwa na gonjwa baya hili.

"Wakazi wa Kagera mlioko jikoni mola awatie nguvu. Yaliyowakuta yametukuta sote."

Hayupo aliye salama. Mola atufanyie wepesi.

------------

Hii si mara ya kwanza kama nchi kupata magonjwa hatari kama haya.

Hata hivyo ni kwa bahati mbaya sana kuwa magonjwa kama haya yakitokea pana watu hudhani uzalendo ni kuuficha ukweli au ni kuupaka rangi urongo. Wakijinasibu kuwa huwa wako kwenye kuzuia wanachokiita taharuki.

Kwenye agenda hiyo ya kuzuia taharuki tegemea vitisho, kejeli, matusi nk kwa ambalo kwao ni jinai kubwa, kuhoji.

Yataka stamina ya kutosha kuwahimili wajumbe hao ambao wengi wao ID zao ni zile za msaada. ID Ina miaka 10 lakini ina posts 20 na katika hizo 12 ni za kwenye mada yenye kuhoji huo uzalendo wao.

Kwa salama ya maisha yetu na watoto wetu tunapaswa kuona ni ibada kuhoji, tena kwa nguvu zetu zote.

Tuliyaona kwenye corona na hata ya sasa yanajirudia. Kwa hakika inataka ujasiri wa kupindukia au uzezeta wa kutosha, kuweza kuwaamini ndugu zetu hawa kwani wana roho ngumu kweli kweli.

Ieleweke kuwa lengo la mada hii ni kuwaangazia wazalendo uchwara hawa wenye kutaka kutupelekesha kama mbuzi tu, huku wakiyaweka maisha yetu na wanetu hatarini.

Ni haki yetu kupata na hata kutafuta habari. Tujiulize tokea tulipotaarifiwa wenzetu 193 Kagera kuwekwa karantini juzi, ziko wapi taarifa mpya?

News Alert: - Watu 193 wawekwa Karantini Kagera kuchunguzwa kama wana Ugonjwa wa Marburg

Post inayofuata nitajielekeza kuandika mwenendo wa wazalendo hawa wenye kuwafanya wenye kuwaamini, kuwa ni majasiri au mazezeta kweli kweli.

Kwa hakika haiwezekani kuwa katikati.
 
Back
Top Bottom