Tunapoichukulia poa Ebola hata kuiita majina yasiyojulikana ni hatari

Hawataki kusema ebola wanataka kusema Marburg Ili atakaye hoji waseme google. Eti kwamba hilo ni jina jingine wakiita "kisawe."

Cc: Ruble

Kaka una uhakika ni ebola? i mean ww ni mtaalam wa afya ambae uko eneo husika na una uzoefu wa magonjwa ya mlipuko?
 

Mkuu nilitaka kukupuuza lakini nikadhani sitakuwa nimekutendea haki. Ikizingatiwa waungwana wanasema elimu haina mwisho.

Kwamba badala ya hoja umetokea kumshambulia mleta mada? Tena bila ya msingi wowote ila kwa perception zako tu?

"Kwani wewe ni malaika, Mungu, Jini au shetani?"

Kwamba:

________
"Nimechelewa kuuona huu uzi.

Ila nilipofungua kabla sijasoma nikakuta mwandishi Ni brazaj nikatabasamu Kisha nikaanza kusoma na kupitia maoni ya watu."

----------

Na hivyo ndiyo sasa unataka ueleweke kuwa wewe ni mwerevu sana?

"Huo si ndiyo wenda wazimu wenyewe sasa? Au?"

Kwamba unasema ulikuwa biased na preconceived kabla ya yote? Hadi hapo bado ungependa kuchukuliwa seriously ndugu? Labda na mamburula wenzio tu.

Kumbe huenda hata mada hukuisoma wala kuelewa ila ukaanza ku comment ukilenga kumshambulia mleta mada kwa vyovyote na kwa lolote? Yaani alimradi itakavyokupendeza wewe?

"Hiki si ni kituko cha kufungia mwaka kabisa?"

Huku sasa si ndiko kule kukimbilia kwenu kuripoti tukio la ajali kwenye social media unakokuongelea? Tena mkionyesha na mapicha picha mliyokuwa mkipiga badala ya kuwasaidia wahanga ili mlete mnachoita unyunyu?

Hamna uchungu wala hisia zozote za kiutu. Ni kama ilivyoainishwa kwenye mada na hata ilivyokuwa kwenye corona.

Ona japo aibu kidogo ndugu kwa kutaka kuyahamishia mapungufu yako kwa watu wengine ambao hata haufahamiani nao.

Kwamba uliwahi kutofautiana nami kimawazo? Wajameni, hilo linahusika vipi hapa na mlipuko wa gonjwa hili hatari Kagera huko?

"Wanatofautiana watoto mapacha, sembuse miye na wewe Neema?" -- Chidumule.

Si angalau ungekuwa umeweka basi hapa japo tulichokuwa tumetofautiana ili kuhalalisha tuhuma zako kwangu na kuwaacha wengine ikiwapendeza kujiridhisha?

Haya mengine kwamba uliwahi kuona video ya serikali nyuma huko ya namma ya kujikinga na ebola? Kwani huko nyuma uliwahi kuona taarifa hata moja ya kujikinga na Marburg? Au unarejea kuniunga mkono kwenye mada yangu bila kujua?

"Mengine (kama yalivyo) nimekupuuza, kwa maana ya nini kukimbizana na mwenda wazimu?"

Nimalizie kwa kukupa angalizo tokea kwenye mila na desturi za JF:

"Huku tunako thubutu kuongea waziwazi huwa tunapambana na mada si mleta mada."

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Nitapingana na ww, dunia imebadilika sana na info za magonjwa mengi ziko online.
accessible na watu wote duniani. Difference is experience ya ku deal na jambo lenyewe

Hapa unapingana na miye kuhusu nini ndugu?
 

Kulikuwa na post #289 iliyo summarize mliyoyakimbia kimya kimya.

Kwa tija ipi kuikimbia mada ili kumsakama mleta mada tena kwa allegations zenu ambazo hata ni very much unfounded?
 
Unayasomaga wapi hayo ndugu? Mbona wengine hatuyaonagi?

Ama kweli JF raha sana 🤣🤣
Hivi nchi iitangaze Marburg kuificha Ebola kwa faida gani, si yote ni magonjwa mabaya yanayoambukizwa kwa namna sawa na hayana dawa? Unakuwa unaepusha nini ukiyataja maambukizi ya Ebola kama Marburg? Huoni umekuwa mjuaji katika hili? Na after all ukisha declare uwepo wa magonjwa ya namna hii si issue inakuwa handled kwa kushirikiana na WHO! Kwahiyo kwa mawazo yako WHO nao hawajagundua kwamba kilochopo Bukoba ni Ebola sio Marburg?
Kwani Bavicha mna tatizo gani kiasili?

 

Uko nje ya mada mkuu.

Wapi nimesema Ebola ni Marburg? Wapi nimesema Marburg ni neno jipya?

"Kwamba wakati Unasomea afya siyo ..."🤣🤣

Huko tulishaondoka muda mkuu.
 

Kumbe ulikuwa na bandiko jingine jeupe hapa?

#344 itakuwa imejibu pamoja na hili ndani yake.
 
Hii comment inatosha kuonyesha ni mtu wa aina gani tunajadiriana naye hapa.

Ukiulizwa wapi, ustaarabu ni kuonyesha "pale" kwa kuleta kuleta ushahidi.
 
Rejea title ya maada yako... Na comments zako za mwanzo mwanzo wa thread..

Unajua maana ya title mjomba? Unajua Mod wana mamlaka hata ya kubadili titles hizi ?

Kwa Taarifa yako mods tagged kwenye post hii waliikarabati title hiyo kuwa hivyo unavyoiona.

Hata hivyo hakuna kilicho haribika kwani maelezo kamili kuhusu hoja huwa yapo yote kwenye mada, siyo kwenye title.

Comments zangu za mwanzo mwanzo ni zipi?

"Weka muziki wacha maneno!"

Ninakazia:

"Wapi nimesema ni ebola ndugu?"
 
Mwenyewe unajiona umeandiiika hadi bhaas. Yaani Serikali ifiche ugonjwa kwa maslahi ya nani!? Hivi Ebola unaijua unaisikia, tema mate chini usiombe hilo gonjwa likaitokea katika jamii yetu.

Ugonjwa ulioripotiwa Kagera ni wa Maburg na ni wa virusi wa jamii ile ile ya Ebola lakini wa ukoo tofauti. Huu hauna ukali ule wa Ebola, tahadhari zikichukuliwa vizuri waathirika wake huweza kupona hata kwa 100% na maambukizi yake yanawweza kudhibitiwa kwa muda mfupi tofauti na wa Ebola yenyewe.

Tuwe na utamaduni wa kuheshimu maelekezo ya Serikali hasa inapotokea suala la Magonjwa. Ugonjwa ukifichwa fichwa maana yake kutakuwa na athari kubwa sana na za kijamii na kiuchumi ambapo pamoja na wananchi kuathirika, Nchi kama Nchi itaathirika pakubwa zaidi kwa kuwa itashindwa hata kupata misaada kutoka mashirika ya Kimataifa katika kuudhibiti ugonjwa. So hakuna sababu yoyote ya sreikali kuficha linapotokea janga kama hilo.

Wakati mwingine kabla hujatoka hadharani na kutupa hoja yako, jaribu kujiridhisha kwa kufanya utafiti kidogo
 
Hata hao Plasmodium wako tofauti. Ukishikwa na malaria iliyyosababishwa na Plasmodium malariae, vivax au falsparium unakutana na mziki tofauti kabisa. Mziki wa Ebola ni moto wa kuotea mbali, hawa Maburgs wana tabia zinazofanana kwa mbali na ebola lakini hawatishi. Japo wakikupata bila usaidizi wa kitabibu wanakutoa roho ndani ya muda mfupi.
 
Ugonjwa huu si wa kwanza kwetu. Umekuwapo mataifa mengine. Ni mjinga kweli kweli anayeweza kuamini kuwa hadi sasa hakuna taarifa mpya eti kwamba ni wagonjwa wale 8 na vifo vile 5 vilivyotokea na tatizo liliishia hapo.
Tatizo lako ni kwamba unadandia taaluma za watu. Ungeijua epidemiolojia ya Maburg na Ebola wala usingeendeleza hii hoja. Jambo kama hulijui usilikomalie kwa hoja za hisia, ulizia kwa wanaofahamu wakupe ufafanuzi ndg.
 

Wapi unaposoma ya kuwa nimeona nimeandika mpaka bhaaas? Au wewe ndiyo unaona umeandika mpaka bhaaas?

Hiiiiiii bagosha!

Povu la nini ndugu? Kwani wewe ni katika wakusanya sample za mbuzi, oil na mapapai kupimwa corona kwenye zama za giza?

Kwani ni mgeni wewe kwenye usugu wa ficha ficha magonjwa zetu?

Au ndiyo kuwasili kutokea sayari nyingine ndugu?
 
Tatizo lako ni kwamba unadandia taaluma za watu. Ungeijua epidemiolojia ya Maburg na Ebola wala usingeendeleza hii hoja. Jambo kama hulijui usilikomalie kwa hoja za hisia, ulizia kwa wanaofahamu wakupe ufafanuzi ndg.

Tatizo lako ni kuwa unaona huna tatizo. Tufanye wewe uko vizuri. Kwani kuna taabu hapo ndugu?
 
Ni bahati mbaya sana kuwa kama nchi tumekumbwa na gonjwa baya hili.

"Wakazi wa Kagera mlioko jikoni mola awatie nguvu. Yaliyowakuta yametukuta sote."

Hayupo aliye salama. Mola atufanyie wepesi.

------------

Hii si mara ya kwanza kama nchi kupata magonjwa hatari kama haya.

Hata hivyo ni kwa bahati mbaya sana kuwa magonjwa kama haya yakitokea pana watu hudhani uzalendo ni kuuficha ukweli au ni kuupaka rangi urongo. Wakijinasibu kuwa huwa wako kwenye kuzuia wanachokiita taharuki.

Kwenye agenda hiyo ya kuzuia taharuki tegemea vitisho, kejeli, matusi nk kwa ambalo kwao ni jinai kubwa, kuhoji.

Yataka stamina ya kutosha kuwahimili wajumbe hao ambao wengi wao ID zao ni zile za msaada. ID Ina miaka 10 lakini ina posts 20 na katika hizo 12 ni za kwenye mada yenye kuhoji huo uzalendo wao.

Kwa salama ya maisha yetu na watoto wetu tunapaswa kuona ni ibada kuhoji, tena kwa nguvu zetu zote.

Tuliyaona kwenye corona na hata ya sasa yanajirudia. Kwa hakika inataka ujasiri wa kupindukia au uzezeta wa kutosha, kuweza kuwaamini ndugu zetu hawa kwani wana roho ngumu kweli kweli.

Ieleweke kuwa lengo la mada hii ni kuwaangazia wazalendo uchwara hawa wenye kutaka kutupelekesha kama mbuzi tu, huku wakiyaweka maisha yetu na wanetu hatarini.

Ni haki yetu kupata na hata kutafuta habari. Tujiulize tokea tulipotaarifiwa wenzetu 193 Kagera kuwekwa karantini juzi, ziko wapi taarifa mpya?

News Alert: - Watu 193 wawekwa Karantini Kagera kuchunguzwa kama wana Ugonjwa wa Marburg

Post inayofuata nitajielekeza kuandika mwenendo wa wazalendo hawa wenye kuwafanya wenye kuwaamini, kuwa ni majasiri au mazezeta kweli kweli.

Kwa hakika haiwezekani kuwa katikati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…