GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kila mara alipokuwa akihojiwa na Waandishi wa Habari mbalimbali alisema tena kwa Nyodo zote kuwa Yanga SC itakuwa Bingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania ( TPL ) na kwamba hata Kombe la ASFC pia itabeba na kwamba hajaona Timu ya Kuizua Klabu yake. Ushahidi wa haya ' Majigambo ' yake upo wazi tu na nitashangaa kama Wewe huna au hujawahi Kumsikia.
Leo baada ya ' Kufurumushwa ' Mashindanoni kwa Kufungwa kwa aibu na Klabu ya Lipuli ya Mkoani Iringa Kocha wa Yanga SC ( ambaye Uzi huu ndiyo unamuhusu kwa 100% ) Mwinyi Zahera amejitetea kwa Kubadili haya maneno yake na hizo Kauli zake alizozitoa awali ambapo sasa amesema kuwa Malengo ya Yanga SC kwa mwaka huu hayakuwa Kuchukua Ubingwa wowote ule uwe wa Ligi au Kombe hili la FA isipokuwa Yeye kama Kocha na hata Klabu ya Yanga walikuwa na Malengo tu ya Kuhakikisha wanakuwa ndani ya Sita Bora katika Ligi.
Kama kuna Kocha ambaye nina uhakika ana matatizo makubwa ya Akili basi ni huyu Kocha wa Yanga SC na pia kama kuna Kocha ambaye anawachezea Akili Yanga SC huku akiwafanya atakavyo na hawawezi Kumfanya lolote kwakuwa ameshawashika pabaya ni Mwinyi Zahera. Nina uhakika mpaka Yanga SC wakija Kumshtukia basi atakuwa ' amewagharimu ' mno na watanikumbuka na kuyakumbuka haya maneno yangu na huu Uzi wangu.
Nawasilisha.