Tunaposema Sera za CCM zimeshindwa hatutanii, mfano hai huu..

Kuanzia leo nitakua ninakuita kwa jina hili; "Mhe. Mkata tama" na watu wa jinsi hi tukiwa nao walau 10,000 tu basi kuumaliza umasikini utahitajika muujiza wa Mungu mwenyewe na sio akili zetu hizi alizotupa Mungu.

Mazindu utakuwa hujanitendea haki kwa sababu hujasoma katikati ya mistari ya mchango wangu kwenye bandiko la Mzee Mwanakijiji.
 
Ndo anacho advote Mwanakijiji. Mambo ya nchi hii ni ya hovyo maana hayajapangiliwa hatujui nini kianze na nini kifuatie. Shida tupu

 
Last edited by a moderator:
Angalia jinsi katiba ya Chenge inavyopambwa. Eti ndo bora kuliko katiba zote zilizowahi kuwapo. Kwani tulishawahi kuwa na katiba ya wananchi. Saa tulitaka angalao hii iwe na ridhaa ya wananchi, lakn watawala wakaiteka wakaondoa kila oni la wananchi wakaweka ya kwao tu. Futa tunu za taifa, futa miiko, futa, uzalenzo na kila kilichokuwa kizuri

Halafu mtu anaibuka anasema ni nzuri sana, wakati hatujui hata kama inaweza kutumika ndani ya Zanzibar kwenyewe. Ni katiba ya JK na genge lake la wezi
 
Pengine ibadilishwe lakini tarehe ya uchaguzi ikajulikana kwani inatoka katika katiba. Ni Jumapili ya mwisho ya mwezi Oktoba, tarehe 25! Tanzania ni moja ya nchi chache Afrika ambayo tarehe yake ya uchaguzi mkuu inajulikana kwani iko ndani ya Katiba.
 
Duh! Una hakika na ulichokiandika? Kwamba kwa sababu jimbo lina mbunge wa upinzani basi serikali, mfumo na sera zinazoongoza jimbo hilo ni za chama cha upinzani. Je wanakusanya kodi na wanachagua watendaji wao? Nafikiria mfumo wa chama kimoja kwa muda mrefu ulitupotosha. Ninashangaa watu wanajenga hoja za 'ni walewale wataleta mabadiliko gani?'! Kumbuka mwanakijiji akajaribu kuzungumzia sera na hakika sera zinazotekelezeka ni za chama kilicho madarakani.
 
Uzi huu moto sana kwa CCM.. wanajua kuwa nchi hii haina tofauti na headless chicken! Hatuna dira! Hatujui nchi hii inaelekea wapi ingawa tumejaaliwa fursa za kila aina!!! Imefikia mahala Viongozi wote wanaiba mchana kweupe, hakuna mwenye kuona future ya Tanzania iliyojaa neema kedekede ... Bila CCM kuondolewa Maendeleo ya nchi hii itabakia kuwa Ndoto ya alinacha ....
 
Mojawapo ya maeneo ambayo yanazidi kuthibitisha kuwa sera za CCM zimeshindwa ni ile ya kujiandaa na majanga na uokoaji. HIvi ni taifa gani la watu ambao hawafikirii njia bora za kujiandaa na kujiokoa na majanga? NI kama tuna usahaulifu wa makusudi hivi...
 
Mm wakenya nazd kusema wAko saw a acha wasonge mbele. Wakat Uhuru anapunguza mishahara ya mawazir kwenda kuberesha huduma za jamii kuku kwetu wabunge wanaongezeana posho and they talk ravish in the house shame upon us.
 
sasa kama hata rais wa nchi anapingana na taasisi alizoziunda mwenyewe mfano TAKUKURU, CAG , T.R.A, na kamati za uchunguzi kwa kusema pesa sio za umma kinyume na taarifa za wateule wake huoni kwamba si tu kuwa sera alizopangiwa na chama chake zimeshindwa, bali zimekufa nyang'anyang'a

wanaotarajia kuona sera za CCM kuwa zitafanya kazi au kuwa ni nzuri basi watarajie siku moja manii ya paka yataoteshwa kwa mbwa yazae chui.
 

Wewe unayeuliza wabunge wa upinzani wamefanya nini uliwahi kuona kuna budget inayokabidhiwa wabunge zaidi ya mfuko wa jimbo? Wapinzani wamechangamsha wananchi waone wanavyoibiwa na kuifanya serikali ipunguze wizi! Kazi ya wabunge ni kuishinikiza serikali itekeleze shughuli za maendeleo ila kwa Tanzania kuna ujinga wa serikali kususia baadhi ya majimbo yanayotawaliwa na upinzani....pia ukumbuke mbunge kazi yake ni kuwawakilisha wananchi wake bungeni na cyo kujenga barabara wala kuleta maji
 

Nikisoma maandiko yako napata taabu sana ya kukuelewa kuwa huo ndio uwezo wako wa kuelewa au unafanya makusudi? Hayo maeneo uliyotaja serikali inaongozwa na Chadema au kuna uwakilishi wa wabunge tuu? Tundu kusema watoto wake hawezi kuwapeleka shule za kata hata hilo umeshindwa kumwelewa anamaanisha nini? Tumia muda wako zaidi katika kujisomea ili ukuze uwezo wa kuelewa ili baadae hata michango yako iwe constructive.
 
Sera nyingi zimefeli kubwa ni ya Elimu,jamaa watoto wakifeli sana,wanatanua goli ili watoto wafaulu kisha utasikia ufaulu umeongezeka,uliona wapi GPA ya 0,3 mtu anakwea kidato cha tatu?
Kioja subirini matokeo ya mwaka huu mtanikumbuka!, yameandaliwa kupigia kampeni.

Uliona wapi unaanzisha ujenzi wa maabara wakati walimu ulionao hawakujifunza vyuoni real practical?, je utawapeleka vyuoni tena? Jamaa sikui hawana long plan,wanaibuka tu
 

Lakini wao wanapouza "mafanikio" wanasema "wameandikishwa watoto wengi kwa asilimia 101" na kuwa sasa hivi kuna "shule nyingi" na "vyuo vingi"....
 

Unajua watu wengine wana imani za kisiasa ambazo hazina tofauti kabisa na imani za kishirikina.
 
Kuna watu wanaona kuiondoa CCM ni kama kutoitendea haki fulani hivi. Wanaona ni kama ina haki yankutawalana CCM kutotawala ni kuivunjia haki hiyo.
 
Ujuha tu unawasumbua! watu kama hao nina wafananisha na Mwanamke mwenye kuteseka kwa kipigo, njaa, manyanyaso ya kila aina na wakati mwingine anazindukia ICU kutokana na kipigo cha Mume ------- LAKINI bado anaendelea kung'ang'ania kwenye uhusiano ambao hauna manufaa kwake... Tusi wahukumu sana maana Watu wa namna hiyo wakikutana na wenza wenye kujua thamani ya mahusiano huwa wanajutia sana muda waliopoteza kwenye ndoa yake ya awali iliyogubikwa na machungu tele... Nawauliza Swali Moja tu la Msingi:- CCM imeshindwa kuwaletea Watanzania Maendeleo toka tumepata Uhuru hadi leo, Je Bado wanaamini kuwa Inaweza kupatia Maji safi na Salama, Huduma Bora za Afya, Elimu, Miundombinu, hali nzuri ya Maisha?... Kama jibu ni ndiyo the LINI watafanikiwa? kama jibu ni HAPANA then Mnasubiri nini Kuwaondoa??? ... Shame kuwa Tanzania is the only place ambapo Wazawa wanaonekana Second class citizens na wageni wanaonekana Raia number moja wenye opportunities kibao ...
Kuna watu wanaona kuiondoa CCM ni kama kutoitendea haki fulani hivi. Wanaona ni kama ina haki yankutawalana CCM kutotawala ni kuivunjia haki hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…