Tunaposema Sera za CCM zimeshindwa hatutanii, mfano hai huu..


mwanakijiji sema neno lolote kwenye mada hii ukizingatia kipindi hiki cha uchaguzi.
 
Last edited by a moderator:

tehteh........
cc: Pasco,TeamLowassa,[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=60503"]VUTA-NKUVUTE,[/URL]Ocampo four,[URL="https://www.jamiiforums.com/member.php?u=138049"]Lizaboni, [/URL]Kibo10,
 
umewahi kujiuliza ni kwanini wabunge wa upinzani wanatimuliwa bungeni na kubaki chama tawala kikipitisha hoja???
 
MM amesahau haya tayari ameshabadilika
 
Hapa ndipo ninaposimamia, Cha kushangaza na kusikitisha!, washindani wakubwa ni wawili tuu!, Edward Lowassa na JPM, ukishauri watu wasimchague Lowassa, hata bila kusema wamchague nani, unamanisha wamchague JPM, hivyo sasa ni heri uchague wale wale kuliko kubadilika?!.

Pasco
 
Tuseme huyu mzee wetu kuja na sera ya elimu kwanza inaweza kuwa na msaada mkubwa sana au mnaonaje kwa hili?
 
hapa ndipo ninapokubaliana na mfanyabiashara Mengi kuwa 'tuwe na akiba ya maneno' unaweza kuumbuka siku moja
 
mwisho chechemea ni 25/10/2015 magufuli arudi chato kupalilia karanga na maharage yake, ni upumbavu mkubwa sanavkuendelea kuipigia kura ya ndiyo ccm. swali langu: Kahama, Geita, na hadi Buzwagi hivi sasa zinaelea juu kutokana na kazi kubwa mno inayoendelea chini ya uchimbaji wa dhahabu katika eneo hilo: Je hivi watanzania wenzagu tutalifukia na nini hilo shimo kubwa kama jehanamu? je unaweza kutuambia ni faida gani Tanzania yetu imepata kutokana na dhahabu inayochimbwa eneo hilo? je ulishamsikia magufuli analiongelea swala hilo ndani ya bunge ukizingatia dhahabu inachimbwa karibu kabisa na nyumba kwao?

je hivi wewe unakubali kabisa eti Mkapa pamoja na usomi wake huo alisain serikali ipate Tsh 3 katika 100? je bado unadanganywa kuwa ccm inahuruma na watanzania waliopo sasa na wale watakao ishi miaka 100 ijayo; na je umewahi kujiuliza ni kwanini Mkapa alisaini mpaka miaka 100 ijayo? je unafikiri dhahabu ya Geita na Kahama itakuwa bado ipo mpaka mda huo ukizingatia wazungu wameteremsha mashine mpya na zenye nguvu na zina fanyakazi 24hrs? je umewahi kujiuliza ni kwa nini Rais wetu Kikwete amesaini haraka sana mikataba ya gase?

Sisi tunaoshuhudia haya tunabaki tunalia usiku na mchana tukijililia sisi wenyewe na watanzania watakao ishi miaka 80 ijayo; je ni kwanini serikali inalipa deni la dowans huku ikijipiga kifua kuwa kamwe haimjui mmiliki wake? zinduka!! ihurumie nchi yako inayobakwa na watawala wetu tokea enzi ya uhuru: jitokeze kupiga kura ya ndiyo kwa Ukwa ili angalau tuondoe kabisa mfumo wa kifisadi uliojengwa na watawala wetu; tunahitaji kuondoa ile nadharia ya uchama tawala maana kupitia huo Watanzania tunaibiwa hasa ukizingatia wengi wetu hatuna uwezo wa kuujua utajiri wa Taifa letu hii ni kutokana na ukweli kwamba wengi wetu hatukuenda shule; maana ni shule pekee ndiyo itampa mtu kujua geografia ya nchi yake: Sema ndiyo kwa LOWASSA kwa ajili ya mabadiliko na utaiokoa nchi yako.
 

Kama wangekuwa na sera nzuri tungeona uzuri huo unajitokeza pia kwenye kuandika katiba mpya maana idadi kubwa ya wajumbe walikuwa ni kutoka ccm na wenyeviti wa kamati pia wengi walikuwa kutoka ccm. Utaalamu huo tungeuona pia ukijitokeza bungeni wakati wa kujadili na kupitisha bajeti na sheria. Lakini badala yake kulikuwa mbwembwe na kupitisha sheria kiubabe! Kuendelea kuamini kuwa chini ya ccm nchi hii itabadilika na kuwa ya asali na maziwa ni kujidanganya kwa hali ya juu. Mfumo chakavu wa ccm unatakiwa uachwe na badala yake tuwe na mfumo mpya usiotokana na ccm. Wanaoogopa mabadiliko wafikirie pia kama waasisi wetu wangeogopa kujitawala tungekuwa bado tuko chini ya wakoloni. Kila mabadiliko yanaleta changamoto zake - inabidi tuzikabili na hatimaye tuanze kuona matunda ya mabadiliko. Kuna msemo unasema: "Cowards die many times before their real death." Hivyo, kuogopa kubadilika ni sawa na kufa kabla ya kufa kwenyewe hakujafika.
 
sera za ccm ni kuua tembo,vifaru,na kupandisha twiga kwenye ndege na kupeleka udongo ulaya ili kufanya utafiti wa madini ,tumebakiwa na mahandaki makubwa.
 
Acha ulofa wewe mtoa maada kama sio ccm ungekua hapo ulipo we we?
 
sera za ccm ni kuua tembo,vifaru,na kupandisha twiga kwenye ndege na kupeleka udongo ulaya ili kufanya utafiti wa madini ,tumebakiwa na mahandaki makubwa.

Kwa nini sasa Chadema wachukue mtu aliyetoka hukohuko na kushiliki hayo yote ndo awe mgombea? Huyo si ataibadilisha Chadema kuwa CCM nyingine?
 

Hii biashara mwisho wake ni October 25.
 
MM njoo huku maana jamaa wanapekuwa makabrasha.
 
M.M.M Akiwa Katika Ubora Wake, Kabla Ya Kukutana Padri Muasi Usa. Sasa Unayameza Matapishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…